Nakuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati na za kipekee kwa wafanyakazi wenzangu wote na uongozi mzima wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) kwa kunisupport na kunifariji katika kipindi hiki kigumu cha msiba mzito wa mama yangu mpendwa Asha Nassibu Shefa kilichotokea tarehe 7 March 2011. Inshallah MwenyeziMungu atawalipa kwa hilo.
Pia napenda kuwashukuru wafanyakazi wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambapo marehemu ndio alipokuwa anafanya kazi wakati wa uhai wake. Pia nawashukuru wafanyakazi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege(TAA) kwa msaada wao wa hali na mali.
Pia nawashukuru sana watanzania wote waishio stochkhom(Sweden) kwa kuandaa na kusoma kisomo cha kumuombea mama yetu mpendwa kilichofanyika tar 19 mwezi huu huko Sweden.
Nawashukuru marafiki zangu wote wa hapa nyumbani Tanzania pamoja na marafiki zangu waishio uingereza na wengine wote popote pale walipo. Bila ya kuwasahau majirani zangu.Nawashukuru sana.
ASANTENI SANA NYOTE, NA MUNGU AWABARIKI
Fatma Shefa


Poleni sana Fatma, Mungu azidi kuwatia nguvu.
ReplyDeletePole sana Fatma, sisi tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi.
ReplyDelete