Hadi wakati wa mapumziko huko Lubumbashi katika uwanja wa Stade de la Kenya ambapo TP Mazembe ilikuwa inaiongoza Simba SC kwa bao 2-0, katika mchezo wao wa klabu binga Afrika na myama kakaliwa shingoni toka kipyenga cha kwanza ambapo wa-Congo wamefunga kambi ndani ya 18 za Msimbazi.
Hata hivyo Simba wanachomoa kamoja dakika ya 76 ya kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Emanuel Okwi. Walibaki nako hako kagoli hadi kipyenga cha mwisho ambapo umeisha bao 3-1. Na Mpira Umekwisha huku simba wakihitaji kushinda 2-0 nyumbani ili kusonga mbele
Mazembe 3-Simba 1; dk ya 80.
ReplyDeleteSimba waenyimbwa Lubumbashi!
ReplyDeletebadooooo shambani kwa bibi simba mweleke tuuuuuuuuuuuuuu
ReplyDeleteTatizo lako U CCM umekutawala sana! Utalijua jiji, wakija tutawatoa tena kwa goli nyingi tu! Simba Oyeeee.....!
ReplyDeleteSio mbaya kihivyo Simba wakijitahidi katika mchezo wa marudiano DSM na kuwafunga 2-0 watakuwa wamewatoa. Mchezo tumeuona, Mazembe sio timu ya kutisha sana, ila washangiliaji wao karibu robo tatu ya uwanja walikuwa wanawashangilia kwa nguvu zote kuanzia mwanzo hadi mwisho, hivyo hii iliwapa wasi wasi Simba. Kwa kweli Simba walicheza mchezo mzuri.
ReplyDeletedah mtu unatoa taarifa kwa unazi kiasi chote hicho kama simba haitoki Tz!!!!!
ReplyDeleteNdiyo maana mpira wa Tanzania hautaendelea..poor home team supporting..angalia tuu hizi habari zilivyoandikwa kinazi..! Ndiyo maana naombea Simba na Yanga siku moja tuwe hatunazo kabisa ..tuwe na timu zenye kucheza soccer na sio fitna na majungu!
ReplyDeleteTulijua tu siyo watapokea bakora na itakuwa hivyo hivyo DSM.
ReplyDeleteMdau
Lubumbashi
Watu wasikose uzalendo na kuzibeza timu zetu. WaCongoman sio kwamba wanajua mpira saana bali wanakuwa na uzalendo wa kuzipenda timu zao na kuzipa moyo kuanzia waandishi wa habari, viongozi mpaka wapenzi na washabiki wote hukuti wanazomea timu zao, hii inawafanya wapate ushindi. Mfano mzuri tu jana timu ya AC VITA ya Congo- Kinshasa ilifungwa 1-0 na Canon Sports Club ya Cameroon nyumbani kwao Kinshasa bado wakienda huko Cameroon ugenini uwezekano wa kushinda ugenini wakati nyumbani kwako umefungwa ni mdogo. Licha ya kufungwa nyumbani kwao Wacongoman hawakuwavunja moyo wachezaji wa VITA bado wana matumaini ya kushinda ugenini, wamekuwa wakiwapa moyo wachezaji wa VITA hawakuwazomea wala vyombo vya habari havikutoa lawama wa kuandika maneno ya kukatisha tamaa, huu ndio ustaarabu na uzalendo amabo sisi TZ tunaukosa. Mwaka jana hiyo TP MAZEMBE ilifungwa 1-0 na APR ya Rwanda mjini Kigali, waliporudi Lubumbashi waliungwa mkono na mashabiki wao na kuwatoa APR kwa bao 2-0.
ReplyDelete