MASIKITIKO KWA AJALI ILIYOSABABISHA VIFO VYA WASANII WA KUNDI LA FIVE STAR MODERN TAARAB

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali iliyotokea Usiku wa Saa 2 Tarehe 21/02/2011 katika barabara kuu ya Iringa-Morogoro kwenye eneo la Hifadhi ya Wanyama ya Mikumi na kusababisha vifo vya watu 13 wakiwemo wasanii wa Kundi la Muziki la Five Stars Modern Taarab na kusababishwa wengine kadhaa kujeruhiwa.
BASATA linaungana na familia za wafiwa na wasanii wote nchini kwa maombolezo ya msiba huu mkubwa na wa kihistoria. Kufiwa kwa wasanii hawa ni pengo kubwa kwa familia na Sekta ya sanaa nchini, kwani kupungukiwa na wasanii (wabunifu) 13 kumerudisha nyuma kimaendeleo sekta ya sanaa nchini na pengo hilo haliwezi kuzibika kwa njia yoyote iwayo.
Aidha,Baraza linawapa pole majeruhi na kuwaombea wapone haraka ili hatimaye waweze kurudi katika hali yao ya awali na kushiriki shughuli za sanaa.
Kwa tukio hili tunaungana na familia za wafiwa na wana Five Star Modern Taarabu kuwapa pole sana kwa msiba huu.Baraza linajua ni kipindi kigumu sana kwa wanafamilia na wadau wote wa Sanaa kwa Ujumla ingawa hatuna budi kuheshimu maamuzi ya Mungu kwani muda wote hayana makosa.
Baraza linatoa kiasi cha Tshs 500,000/= kama rambiwambi kwa Kundi la Five Star Modern Taarab ili zigawanywe kwa wafiwa na kusaidia shughuli mbalimbali za msiba huu mkubwa katika tasnia ya sanaa nchini.
Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi Amen
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI

mungu hausiki na ajali hiyo watanzania tusipende sana kumsingizia mungu kwa kila linalo tokea mungu anatupenda sana watanzania.Tatizo bongo tunaishi maisha ya kale saaana .madereva walevi,sheria za barabarani hazifuatwi,rushwa na kadhalika.Binafsi naamini sana tena sana asilimia tisini ya "crush" zinazotokea barabarani si ajali-taafsiri ya ajali ni ile ambayo haikuwa inaweza kuzuilika sasa utakuta hilo roli lililokuwa hapo halikuweka alama zozote kuwa limeharibika na yawezekana lipo hapo kwa siku kadhaa sasa utasema hilo ni ajali????????????????????????TUBADILIKE ,SERIKALI BADIRIKA
ReplyDeleteNi kweli hapo juu ajali zingine ni za kujitakia...halafu uatasikia watu wanasema ni mipango ya mungu...Mungu hapangi haya maajali...Mipango ya Mungu pale mmejitahidi kweli na ikashindikana...lakini hizi ajali za kila siku hata hujui ipi ni uzembe na ipi ni ajali ambayo haikuweza kuzuilika.
ReplyDeletehalafu angalia hao waliopoteza maisha ni watu ambao woote umri wao unaonyesha ni wakutegemewa na ndugu zao...Ni watoto wangapi hapo wamepoteza wazazi, ni watu wangapi hapo wamepoteza kaka , dada watoto ...Inasikitisha sana...Ukisoma hizi ajali halafu kesho utakuta huyo aliyepack gari kiuzembe au kama ni zembe wa dereva kesho upo barabarani kama kawaida vile....