Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia) akizungumza na wataalam wa uchumi leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano ulioandaliwa na wataalam hao kwa lengo la kuwakutanisha na serikali ili kuzungungumzia masuala mbalimbali ya uchumi yakiwemo nafasi za uwekezaji,matatizo yanayoikabili sekta ya biashara nchini, tatizo la mgao wa umeme na athari zake katika uwekezaji na namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na changamoto hizo.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Mkutano huo Bi. Pratibha Thaker.
Waziri mkuu Mizengo Pinda (kulia) akizungumza jambo na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Jacques Champagne de LABRIOLLE (katikati) na Balozi wa Uingereza Diane Corner (kushoto) wakati wa mkutano wa wataalam wa uchumi leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wataalam wa uchumi na viongozi mbalimbali wa makampuni ya Biashara wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa waziri mkuu Mizengo Pinda wakati wa mkutano wa wataalam wa uchumi leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifafanua masuala mbalimbali kwa waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha majadiliano ya maswali na majibu ya wataalam wa uchumi kwa serikali leo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni nafasi nzuri ya kueleza ukweli kuhusu ubovu wa huduma za Bandari na TRA zinazosababisha mizigo kulipiwa storage fee kubwa baada ya kuwekewa mizengwe mingi wakati wa kulipia ushuru.

    ReplyDelete
  2. Chadema waendelea kulia na Dowans


    Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilifanya maandamano yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Shinyanga na kusisitiza kuwa kitaendelea na maandamano yake licha ya Serikali kudai kuwa kina mpango wa kuleta vurugu nchini na kuwataka wananchi wapuuze madai hayo.

    Akizungumza katika mkutano wa hadharani katika uwanja wa Joshoni jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema kuwa pamoja na kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya jana usiku kuwa chama hicho kina lengo la kuleta vurugu, hawana nia ya kuleta vurugu ila wanaandamana kupinga kulipwa fidia ya Sh. bilioni 94 kwa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Limited na maisha magumu kwa wananchi.

    Mbowe alisema kuwa Chadema sio wendawazimu kuitisha maandamano hayo, kwani lengo lao ni kuishinikiza serikali kutoilipa Dowans na kupinga kupanda kwa gharama ya maisha na bei ya umeme.

    “…tatizo kubwa la Watanzania si kupanda kwa gharama za maisha tu, lakini kuna mambo mengi yanayosababisha ugumu wa maisha,” alisema Mbowe huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

    Mbowe alimshauri Rais Kikwete kujitahidi kutatua matatizo ya Watanzania na kama hatafanya hivyo, chama hicho kitaendelea kuandamana.

    Alisema kuwa kama yeye (Mbowe), Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilibrod Dk. Slaa na Wabunge wake wanafanya makosa kufanya maandamano serikali iwakamate.

    Awali, akizungumza katika mkutano huo, Dk. Slaa alisema kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, hana haki ya kuikemea Chadema kwa kuwa yeye (Tendwa), ndiye chanzo cha matatizo yote katika vyama vya siasa nchini.

    Dk. Slaa aliyasema hayo kufuatia taarifa iliyotolewa na Tendwa katika vyombo vya habari akikemea maandamano hayo ya Chadema na kauli za viongozi wake kuwa zinaleta uchochezi.

    Akizungumzia kuhusu Dowans, Dk. Slaa alisema kuwa Serikali haipaswi kuilipa kampuni hiyo kwani ni kampuni ya kitapeli tangu ile ya awali ya Ricmond iliyoizaa Dowans.

    Alimtaka Rais Kikwete kuwachukulia hatua mara moja wote walioliingiza taifa katika matatizo ya kukumbwa na giza na matatizo mengine yote, ambayo yanawafanya Watanzania kuwa na hali ngumu ya maisha kutokana na gharama ya maisha kupanda.

    Pia, Dk. Slaa, alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, kutowanyanyasa madiwani wa Chadema katika vikao vya Halmashauri.

    Maandamano hayo ya jana mjini hapa yalipambwa na waendesha pikipiki, baiskeli huku baadhi yao yakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, ukiwemo wa kutolipwa Dowans.

    Baadhi ya wananchi walisema jana kuwa hawajawahi kuona watu wengi kujitokeza katika uwanja huo kwa kiasi hicho, hata wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...