Na Nurdin Ndimbe
Mwanza
Waziri wa Maji Mh. Mark Mwandosya amezindua mradi wa Maji katika kitongoji cha UsagaraWilayani Misungwi Mkoani Mwnza.
Akitoa taarifa ya mradi huo Mhandisi wa maji wilayani Misugnwi Injinia Samwel Chago
alimueleza Mh.Waziri kuwa, mradi wa maji wa Usagara ulianzishwa rasmi mwaka 1961 na ndio ulikuwa wa kwanza katika kitogoji hicho.Alieleza kuwa hali ya maji katika Wialaya ya Misungwi si mzuri sana na inahudumiwa na visima virefu na vifupi,matanki ya kuvunia maji ya mvua, mabwawa,,na maji toka ziwa Victoria. ‘’Mh.Waziri huduma ya maji katika Wilaya yetu kwa sasa ni aslimia 39.7% vijijini na kwa mijini ni 55%’’ kwa wakazi wapatao124,381 kati ya wakaizi 319,457’’alisema Mhandisi huyo wa maji.
Akijibu risala ya Wananchi wa Wilaya ya Misungwi walioataka kuunganishwa katika maradi mkubwa wa Kahama Shinyangwa pamoja na Wakazi wa Usagara kuunganishwa katika mtandao wa Mamlaka ya maji safi na majitaka (MWAUWASA) Mh.Waziri aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kupitia bajeti yake ya mawaka ujao kuungeza visima vigine nine ili kupunguza tatizo la maji katika kitongoji hicho cha Usagara kabla ya mipango ya kuunganishwa katika matandao wa MWAUWASA.kufikiriwa.
‘’ Ndugu zangu najua Misungwi ina shida kubwa ya maji na mimi nasema kuwa kama tulivyohadi maji sasa yamefika Misungwi kilichobaki sasa ni kujenga mtambo wa kusafisha maji hayo na Wizara yangu itafanya kazi hiyo’’ alisema Mh. Mmwandosya. Hata hivyo, Mh. Waziri aliwashukuru Wakazi wa Usagara kwa kukitunza kisima hicho maana tangu mwaka 1961 bado kinatoa maji. ‘’ natoa shukurani zangu za dhati kwa Wanachi wa Usagara kisima hiki ni zamani sana sidhani kuna kisima kingine cha aina hii ina maana mnakitunza ndio maana kipo mpaka hii leo kwa hilo nawapongeza sana’’ alisisitiza
Mradi wa kisima cha Maji Usagara kimekarabatiwa kupitia mpango wa Shinda haraka (Quick Wins)kupitia Wizara ya Maji na kwa Wilaya ya Miungwi vimekarabatiwa visima vipatavyo 40 kwa gharama ya Tsh 197,482,140.70

KERO YA MAJI MASAKI, DAR ES SALAAM
ReplyDeletePamoja na jitihada sehemu zingine zinazofanyika kuwapatia wananchi maji, eneo la Masaki katika Jiji la Dar es Salaam hatujawahi kuona hata miundo mbinu ya maji licha ya wengine kusema maji hayatoki. Mabomba yenyewe hatuna. Viongozi kuanzia wa Mtaa, Diwani na hata Mbunge sijasikia mikakati yoyote inayofanyika kuleta maji. Tumechoka kununua maji ya magari ambayo hayafai. Mhe Mwandosya tembelea Masaki usikie kilio cha wananchi. Kumbuka 2015 sio mbali. Ikamba