Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru linaloendelea kujengwa katika kijiji cha Arumeru Mkoani Arusha, wakati alipokuwa akiendelea na ziara yake ya siku nne ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo, jumla ya shilingi Bilioni 3.6 zinategemewa kutumika hadi kukamilika kwa ujenzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kiliopo Arumeru Mkoani Arusha, wakati alipotembelea Taasisi ya Chuo hicho kuangalia maendeleo ya ujenzi wa majengo yanayoendelea kujengwa leo, Makamu wa Rais yupo Mkoani Arusha katika ziara ya siku nne kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimfariji Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Parseko Vincent Ole-Konne wakati alipokwenda nyumbani kwake mjini Arusha kwa ajili ya kumpa pole na kumfariji kutokana na msiba wa kufiliwa na mkewe leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimia na Mzee Sungura Andrea (103) mkaazi wa kijiji cha Mlanganini Wilayani Meru Mkoani Arusha wakati alipowasili katika uwanja wa Shule ya Sekondari Mlanganini kwa ajili ya kuhutubia Wananchi mkutano wa Hadhara leo, Makamu wa Rais yupo Mkoani Arusha kwa ajili ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknoloji cha Nelson Mandela Arumeru Mkoani Arusha Profesa Mwamila katikati, akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Mohamed Gharib Bilal, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Taasisi ya Chuo hicho wakati alikuwa katika ziara ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo. kushoto Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mhe. Charse Kitwanga, kulia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Isidori Shirima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Namuona Mzee Mabrouk hapo, safi sana kijana unaonesha upo serious na kazi na hutaki mchezo kabisa. Aliyekuwa jirani yako Mza road

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...