Hakuna zawadi ukiweza kung'amua kwikwi
iliyoko katika taswira hii iliyochukuliwa leo mjini Bagamoyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Jibu la kitendawilini kwamba: Hilo Bango kubwa linaonyesha tangazo la conference iliyofanyika 2002 lakini bado lipo hewani mpaka leo hii. Yaani ni takribani miaka 9 bado lipo hapo na hakuna mshusika yeyote aliyeshtuka kwa muda wote huo na kuja kulotoa. kweli bongo tambarare.
    Mdau
    Uppsala,Sweden

    ReplyDelete
  2. Ni hilo bango la the international conference lipo hapo tangu september 2002 na ujumbe uleule, kweli ipo kazi hadi mie nishashangaa!

    mdau majuu

    ReplyDelete
  3. IN BAGAMOYO SIO ON BAGAMOYO

    ReplyDelete
  4. Tarehe inasema 12th September 2002...!!!!

    ReplyDelete
  5. Jamani hii picha haina tarehe ...haijaonyeshwa imechukuliwa tarehe ngapi...inawezekana hii picha ilipigwa mwezi wa nane 2002!!

    ReplyDelete
  6. Bagamoyo ni mji wa mambo ya kale. nyie ndo mnashangaa ila sisi tumeliacha pale kama sehemu ya makumbusho ya tukio lililotokea miaka ya nyuma.vilevile pia kwakuwa bagamoyo tuna mabango machache na hili bango linavutia zaidi ni vema likaendelea kubakia pale ili kuongeza mvuto wa muonekano wa mji wetu bagamoyo.

    ReplyDelete
  7. Huyo mdau wa bango angeandika 'AT Bagamoyo' sio 'ON Bagamoyo'!! Duh! kaazi kwelikweli. Tatizo watu wanaopewa kuweka mabango hayo huwa wanakasimu madaraka kwa madalali, ambao wengi wao hawana uelewa mzuri wa lugha hii ya kigeni. Si unajua tena kila kitu hapa bongo bila udalali hakiendi??!!Lakini cha muhimu ni kwamba, pamoja na kuchapia, ujumbe umefika.

    ReplyDelete
  8. Mdau wa tano kutoka juu hiyo picha ina tarehe ya kimazingira na tarahe halisi.

    Tarehe ya kimazingira ni hilo tangazo la Airtel. Mwaka 2002 hakukuwa na Airtel, bali Zain au Celtel. Airtel imekuja mwaka jana mwishoni.

    Na tarehe halisi right-click halafu check properties.

    ReplyDelete
  9. anonymous at06:43:00 AM - In Bagamoyo means held in ..., On Bagamoyo means the conference was discussing or was about Bagamoyo .....hilo si kosa kwenye bango... I'm just saying!

    ReplyDelete
  10. DILI HILOOOOO - SCAP METAL YA NJE NJE maana JAMAA kashajua Bango halina mwenyewe. toka 2002 kweli halina mwenyewe. Sasa hesabuni siku nne kuanzia leo alafu nenda kapige Picha kama utalikuta. alexbura dar;

    ReplyDelete
  11. Kingine ni kwamba mabango hayo kwa jinsi yalivyowekwa sehemu moja, ni ngumu sana kwa dereva wa gari kuweza kuona gari zingine anapokuwa ktk barabara moja na kutaka kuingia nyingine.

    ReplyDelete
  12. mwanaccm na wewe umechemsha ni "in" na sio "at"

    ReplyDelete
  13. Bango la 2002 na yawezekana ni la kuhusu Bagamoyo hivyo hilo la "on" tulikosoe sababu it could have been one of the conferences discussing the history or the reconstruction of history sites of Bagamoyo lakini muda sasa ndo kikwazo. Je hakuna wenye mabango ambao wangeweza kuweka ya kwao na kulitoa hilo so that the district could get more revenue kutokana na mabango, au hilo halipoBwagamoyo ndo maana wameacha hilo lipendezeshe mji?

    ReplyDelete
  14. anamaanisha BAGAMOYO INTERNATIONAL CONFERENCE

    ReplyDelete
  15. Msisito wa ushahidi wa tarehe ya kimazingira kama mdau alivyoweka sawa hapo juu.Kitu kingine kinachoonyesha picha hii imepigwa hivi karibuni ni
    kwamba kwenye bango la kitambaa hapo chini linaonyesha tukuo lingine la 2011 uonyesha kuwa picha hii ni ya hivi karibuni.
    Mdau
    Uppsala, Sweden

    ReplyDelete
  16. Tumwombw CAG akague ili kujua TRA wilaya ya Chalinze ni kiasi gani cha kodi wamekusanya ktk bango hilo na kwa kipindi gani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...