Jumuiya ya watanzania ugiriki inasikitika kutangaza kifo cha mwenzetu OWEN SIRIPALA NANAYAKKARA kilichotokea ghafla J’pili 24/04/2011 jijini Piraeus.
Kabla ya kuja Ugiriki,Marehemu alikuwa mkaazi wa Kinondoni Dar mtaa wa Ikungi na Kanazi.
Alizaliwa 14/10/1972.
Hivi sasa tupo katika harakati za kumsafirisha akazikwe nyumbani.
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN
- KAYU LIGOPORA
KATIBU MKUU




RIP. Je huyu ana undugu na Mwalimu Mrs Nanayakara ambaye alikuwa Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Muhimbili kwa miaka mingi?
ReplyDeletendio ni Mtoto wa Mwl Sanura Nanayakara huyo huyo...
ReplyDeleteInnalilah wa Innailahi Rajoon Msiba mkubwa muda si muda mrefu umepita Mr Nanayakara nae alitutoka, Pole mama Nanayakara
Mwenyezi Mungu amweke mahala pema peponi.. Poleni washkaji wa Umangani na mimi nilikuwepo hapo na nawajueni jinsi mnavyosaidiana katika hali kama hii.Endeleeni hivyo hivyo
ReplyDeletePole Mwalimu Nanayakara, Mungu aifariji familia ya marehemu.
ReplyDeletePole Sana Shangazi Bi:Sanura aka Mwalimu Sanura Nanayakara, pamoja na familia yote kule Mtaa wa Togo,na Mtaa wa Kanazi,Kinondoni kwa msiba huu mkubwa.Innalilah wa Innailahi Rajoon.
ReplyDeletemwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi.
AMIN
Wadau
Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja
na Ngoma Africa band aka FFU
Poleni sana Ndugu, jamaa na marafiki (Mama Nanayakara). You are in my thoughts and prayers. May his soul rest in peace.
ReplyDeletekwa habari zaidi tembeleeni website ya jumuiya http://www.tanzaniansingreece.org/matangazo.htm kupata update ya mipango ya mazishi
ReplyDeleteMie nimeitembelea hadi nikaandika na email lakini sijapata majibu kutoka kwa mtu yeyote. ninafanya kazi huku katika kampuni kubwa hadi nikaelezea kwamba nataka niwasaidie watanzania na ajira na misaada mingi tu. nilichuniwa. haya, poleni na msiba.
ReplyDelete