Clement Mshana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Clement Senzota Mwete Mshana kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Clement Senzota Mwete Mshana alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).
Bwana Mshana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Dunstun Tido Mhando ambaye amemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa mkataba wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Aprili, 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Pamoja na uteuzi huo mpya, ni ukweli usiopingika kuwa Tido Mhando amefanya kazi nzuri kuifikisha TBC hapo ilipofikia sasa. Kilichomwondoa Mhando TBC ni Politics tu za Tanzania. Tido aliipanga vizuri sana timu yake.

    ReplyDelete
  2. He is oportunistic, all the best!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Hongera Mshana! Watanzania tunategemea makubwa kutoka kwako.Kutokuwa na upendeleo wa kisiasa, kuonesha matukio ya kitaifa live; ikiwa ni pamoja na kuonesha mechi za timu yetu ya taifa (mpira wa mguu. Hongera sana. Tunaomba ufanye kazi kwa manufaa ya watanzania.

    ReplyDelete
  4. Mimi Nam miss sana TIDO MUHANDO...
    Mtanzania Halisi-Kwa BIBI

    ReplyDelete
  5. Mshahara na marupurupu ni vilevile au kapunguziwa? Kwanini? Furaha iliyoje.

    ReplyDelete
  6. Hi Mwadhu,Hongera mwana wedu, Chedi havae! nedhina mburiiiii...wale jogoo kule ushanani watakiona cha moto mtani, du! nafikiri mpaka sasa hivi wameshakufa kadhaa hivi!

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Bw. Mshana kwa uteuzi huu, ila sijajua tu vizuri kuwa hapa umepanda cheo au umeshuka, naamini waliofanya uteuzi huu walilizingatia hilo pia. Kazi njema Mkurugenzi.

    ReplyDelete
  8. hongera bwana mshana kwa uteuzi ila ukifika TBC punguza kwaya maana sio wote wasikilizaji wa kwaya za kanisa waisilamu wapewe muda sawa na wakiristo

    ReplyDelete
  9. Ni mafanikio yaliyoje? Hongera sana ndg mshana. Ushauri, ukifika TBC jitahidi kupunguza makundi hasa yanayojipendekeza kuchongea wafanyakazi wengine. Keep it up.

    ReplyDelete
  10. Tido Muhando, one and only

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...