Clement Mshana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Clement Senzota Mwete Mshana kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Clement Senzota Mwete Mshana alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).
Bwana Mshana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Dunstun Tido Mhando ambaye amemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa mkataba wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Aprili, 2011



Pamoja na uteuzi huo mpya, ni ukweli usiopingika kuwa Tido Mhando amefanya kazi nzuri kuifikisha TBC hapo ilipofikia sasa. Kilichomwondoa Mhando TBC ni Politics tu za Tanzania. Tido aliipanga vizuri sana timu yake.
ReplyDeleteHe is oportunistic, all the best!!!!!!
ReplyDeleteHongera Mshana! Watanzania tunategemea makubwa kutoka kwako.Kutokuwa na upendeleo wa kisiasa, kuonesha matukio ya kitaifa live; ikiwa ni pamoja na kuonesha mechi za timu yetu ya taifa (mpira wa mguu. Hongera sana. Tunaomba ufanye kazi kwa manufaa ya watanzania.
ReplyDeleteMimi Nam miss sana TIDO MUHANDO...
ReplyDeleteMtanzania Halisi-Kwa BIBI
Mshahara na marupurupu ni vilevile au kapunguziwa? Kwanini? Furaha iliyoje.
ReplyDeleteHi Mwadhu,Hongera mwana wedu, Chedi havae! nedhina mburiiiii...wale jogoo kule ushanani watakiona cha moto mtani, du! nafikiri mpaka sasa hivi wameshakufa kadhaa hivi!
ReplyDeleteHongera sana Bw. Mshana kwa uteuzi huu, ila sijajua tu vizuri kuwa hapa umepanda cheo au umeshuka, naamini waliofanya uteuzi huu walilizingatia hilo pia. Kazi njema Mkurugenzi.
ReplyDeletehongera bwana mshana kwa uteuzi ila ukifika TBC punguza kwaya maana sio wote wasikilizaji wa kwaya za kanisa waisilamu wapewe muda sawa na wakiristo
ReplyDeleteNi mafanikio yaliyoje? Hongera sana ndg mshana. Ushauri, ukifika TBC jitahidi kupunguza makundi hasa yanayojipendekeza kuchongea wafanyakazi wengine. Keep it up.
ReplyDeleteTido Muhando, one and only
ReplyDelete