Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk. Thomas Kashililah akiongea leo na wanahabari jijini Dar

Wabunge wengi kutofahamu vyema kanuni za uendeshaji wa Bunge, ndiyo chanzo cha mivutano na vijembe kutawala vikao vya Bunge la 10, na imedaiwa kuwa kuwepo kwa wabunge wengi vijana, kumelifanya Bunge hilo kuonekana kama la wanafunzi.

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah kayasema haya leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar, kufuatia wadau na wananchi kukosoa mambo yaliyokuwa yakifanyika wakati wa Bunge hilo.

Katika Bunge hilo, baadhi ya wabunge walionekana kwenda kinyume cha kanuni na kuzusha majibizano yaliyoambatana na vijembe bila kuheshimu kiti. Wabunge hao walikwenda mbali zaidi pale baadhi walipotaka milango ya ukumbi ifungwe ili wachapane makonde kufuatia kushindwa kuafikiana katika baadhi ya mambo.

Dk. Kashililah alisema Bunge la 10 mkutano wa tatu linapaswa kuwa na wabunge 357 na kwamba, waliopo kwa sasa ni 350 huku asilimia 70 wakiwa ni wageni na vijana, ambao hawana uzoefu na mijadala.

Hata hivyo, alisema kuwa yaliyotokea katika Bunge hilo hayakusababishwa na udhaifu wa Spika Anne Makinda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu. Pia, alisema kuwa Spika Anne alitumia busara na uzoefu wa hali ya juu katika kuweka sawa mambo yaliyokuwa yakijitokeza. Spika ana mamlaka ya kumsimamisha mbunge asihudhurie vikao 10, iwapo atakiuka kanuni, lakini hakufanya hivyo kwa kuwa wabunge wengi bado wanajifunza," alisema.

Alisema kanuni imeweka wazi kuwa Spika wa Bunge anaposimama, mbunge anayezungumza anapaswa kuacha kuongea na kukaa, lakini hilo lilikuwa likikiukwa. Alisema kuna wakati Spika Anne alikuwa akisimama kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali, lakini wabunge nao wanasimama kwa kutofahamu taratibu.

"Hivi katika bunge la namna hiyo, utatoa adhabu kwa watu ambao unajua wapo darasa la kwanza, na mwingine anaibuka na kusema funga mlango tupigane, hawa wanapswa kufundishwa," alisema Kashillilah.

Akizungumzia Muswada wa Marejeo ya Katiba, alisema vurugu zilizojitokeza katika vituo vya kukusanyia maoni ya wananchi, Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar zilisababishwa na upotoshwaji wa muswada huo.

"Naomba ieleweke kuwa Rais Jakaya Kikwete alitoa heshima kwa wananchi kutoa maoni yao katika mchakato wa kuunda kamisheni ya kukusanya maoni, lakini baadhi ya wachangiaji walifikiri ndio muswada wa katiba mpya," alisema.

Alisema katika mkutano huo, miswada sita ilipelekwa bungeni, lakini wa katiba na ule wa marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma haikupitishwa kutokana na muda mdogo wa kuijadili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hata mimi nilishangaa kusikia Mbunge aliyetumwa kuwawakilisha wananchi anadiriki kusema "Funga milango tupigane" hii ni hatari kwa Taifa letu. Bunge lolote Ulimwenguni lina heshima, kanuni na taratibu zake zinazopaswa kuheshimiwa. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

    ReplyDelete
  2. Kwakifupi sijaona kama hiyo point ya kuwepo wabunge vijana ndio tija...wabunge vijana wanauliza maswali na wanataka majibu, hakuna mambo ya kuweka chini ya carpet na kwenda kuyanzungumza mafichoni....maana hayo ndio yanayofanyika siku zote na hakuna la maana tunaloliona nchini. Watanzania tuamke, this is point does not hold! Wenzetu wanachapana makonde na mambo yanafanyika, haya mambo yakujifanya tunadumisha amani na tamaduni wakati tuna chuki moyoni ni upuuzi mtupu. Kama wameona kuna wabunge vijana wawape taratibu na kanuni, kwani hakuna orientation? na hizo taratibu ziwe zinazoenda na wakati. Tukumbuke this is 2011 na sio 1967! Things need to change, we take it or leave it, what's best is to accept and accomodate those changes!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...