Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na baadhi ya viongozi wa soko la Tandale alipotembelea sokoni hapo.
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Tandale alipotembelea sokoni hapo.

Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Mhandisi Christopher Chiza amesema lengo la serikali kuingiza mahindi sokoni tani elfu 50 kutoka Wakala wa Taifa wa Hifahi ya Chakula (NFRA) wakati huu wa uhaba wa mahindi ni kutaka kushusha bei ili kumpunguzia makali kwa mraji.

Mheshimiwa Chiza amesema hayo hivi karibuni alipotembelea soko la Tandale kujionea hali halisi ya uhaba wa mahindi katika soko kwa sasa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Soko la Tandale Sultani Kiyumbo amesmweleza Naibu Waziri kuwa bei ya mahindi kwa sasa ipo juu sana, kilo moja ya mahindi ni kati ya 495 na 500 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo bei zilikuwa ni kati ya 240 na 280.

Bw. Kiyumbo amesema kupanda kwa bei katika soko hilo imetokana na kukosekana kwa mahindi ya vuli kutoka Handeni, Mkoani Tanga kutokana na mvua za vuli kutonyesha.

Aidha Mheshimiwa Chiza amesema Serikali imeamua kutouza mahindi hayo kwa njia ya Tenda na badala yake kuyauza kwa wafanyabiashara wadogo wanaosaga unga na kuwauzia waraji moja kwa moja ili kuhakikisha walengwa wananufaika uamuzi huo serikali na sio wafanyabiashara wakubwa wenye mitaji mikubwa.

Mheshimiwa Chiza amewataka wafanyabiashara wanaomiliki vinu vya kusaga nafaka watakaohitaji kununua mahindi kutoka NFRA waende kujiorodhesha kwa Mkuu wa Wilaya ili waweze kupewa vibali ili wapatiwe mahindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...