
WATANZANIA: SEATTLE, WA NA PORTLAND, OR
Kwa niaba ya Mwenyekiti TANZASEATTLE nawakumbusha kuwa sherehe zetu za Muungano ni Jumamosi
hii tar. 30/4/2011 katika ukumbi wa Eritrean Association Hall (1528 Valentine
Place South, Seattle, WA, 98144).
Sherehe zitaanza saa kumi jioni.
Kiingilio ni dola 15 (utapata chakula, utaburudika kwa fashion show, utapata
burudani ya ngoma, utacheza muziki mpaka majogoo). Vinywaji vitauzwa ukumbini (maji na soda ni dola moja moja, bia dola 3). Tutapokea cash au check tu.
Niwakumbushe tu kuwa Fashion show itaongozwa na dada ASIA IDOROUS- KHAMSIN
kutoka Texas, Ngoma na Mr. Kedmon Mapana (Jiandae kucheza ngoma, usisahau khanga za kujifunga) , Muziki na DJ Dully).
Tafadhali usikose, alika jamaa na marafiki
(wageni wote watalipa kiingilio kama
kawaida)
================= NJOO TUSELEBUKE ==============
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...