Ankali habari za leo,

Nimeona wadau kibao wanaomba msaada kwenye tuta na wengi inaonesha wanafanikiwa. Nami nipe japo nafasi nitoe la kwanza huenda nikasaidiwa. Ntashukuru kweli ikiwa hivyo maana dah!

Mie ni mwanamke wa makamo kiasi (miaka 36) nimeolewa na nna watoto watatu, na ndoa yetu ina miaka tisa sasa. Uwongo, pamoja na mikwaruzo ya kawaida (shemejio kuchelewa kurudi, hasa siku za mechi za ulaya ikicheza Manchesta, ama jumapili akiaga kwenda msondo etc.) kuwepo, sie bwana tunapendana na sioni kibaya kwa sasa wala siku za karibuni. Sijui lakini... watu huenda wakabadilika.

Ankali shida yangu mie sio malavidavi bali ni maumbile yetu. Yeye (ni mtu wa laga ile mbaya) ana kifriji kikubwa na tu. Nami, baada ya mtoto wa pili nikazembea kufunga tumbo. Hivyo likawa kubwa na alipokuja wa tatu ndio ikawa balaa, Kwa lugha ingine wote tuna vifriji, tena vikubwa hasa kiasi tukikaa 'mezani' kupata 'chakula cha usiku' kwa mujibu wa katiba ya nchi, mambo huwa si sawa. Kila staili ya 'mlo' inakuwa shida na piga ua dawa hapa ni kupunguza vifriji.

Hivyo baso, kwa heshima na taadhima naomba wadau wa hii blog ya jamii wanisaidie tufanyeje mie na mme wangu ili maisha yapendeze kama wengine?

Mdau Kinyerezi
(Email kapuni tafazali, jamaa akijua ataua mtu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Nendeni Jimu, Viwanja bwerere vya bure kufanya mazoezi kila siku. Acheni ulafi kula vyakula vya mafuta na kilaji (Chui Chui ) Serengeti iwe sehemu ya maisha yenu. Hakuna cha kusikizia eti nilisahau kufunga tumbo mambo sio ya kisasa. mambo yanaenda kisomi.Kisomo cha ngumbalu cha mwl kilikuwa kinafaa.

    ReplyDelete
  2. Ushauri huu ni wa kitaalamu.

    Ili uzito upungue, inabidi uingize kidogo zaidi ya unachotumia. Au uchome calories kwa spidi ya ajabu. Watu wembamba wengi, mwili wao unachoma calorie kwa spidi kubwa mno, hao hawahitaji tizi. Kwa wewe kibonge, inabidi uingie Gym na ujizoeshe tabia za kufanya mazoezi. Tafuta treadmill, tembea kwa dakika 90 mara tatu kwa wiki. Halafu kula misosi ya ukweli, sio vyakula vyenye mafuta. Asubuhi kunywa chai chukuchuku mpaka lunch hiyo. Achana na askrimu za Baresa zinakulostisha.

    Ukienda kwenye ofisi za watu panda ngazi usichukue lift. Achana na vibajaj kutoka kituo cha basi mpaka nyumbani. Tembea zako ndogo ndogo. Ukifuata huu ushauri miezi 3 tu, kifriji kwishnei.

    ReplyDelete
  3. pole sana, huo mtihani kweli, najua watatokea wengi kukushauri na kila mtu na mawazo yake, lakni mimi ningekushauri kwanza punguza kula mafuta, sukari including vinywaji vya sukari, kama mnywaji wa mabia dada pia fanya kama huzioni vile zinachangia pia. vilvile kama utaweza jiwekee kula yako mwisho saa kumi na mbili jioni usile tena chakula kizito, kama utaweza inapofika mda huo jaribu kunywa maji sana ili kuyeyusha chakula uulichokula mchana mzima, vilevile kama uwezo upo kwa mda huo jaribu kula fruit au vyakula vyepesi, epukana na kula halafu kulala hio pia inachangia, NA SOME TIMES WANASEMA RED MEAT INACHANGIA) samaki ni wazuri. na pia mazoezi ya sit up kila asubuhi na jioni, na kila unapoapta mda. inaumiza lakni hio itakusaidia. na kuhusu chakula usile mlo mkubwa kwa mara moja bora ule kidogo then badae ule tena, hio mimi ilinisaidia kwa sbabu na mimi nna watoto 3 kama wewe na umri wangu ni 30 lakni nimweza kujicontrol. NAWAACHIA WENGINE

    ReplyDelete
  4. Inabidi wewe na mumeo muanze mazoezi na kuangalia diet yenu kwa undani zaidi la sivyo hio "chakula cha usiku hamta enjoy" anzeni mazoezi hio mi-laga mnajitakia mi blood pressure na magonjwa yanayokuja kutokana na unene

    ReplyDelete
  5. Rukeni kichura chura kwa dakika 30 siku tano kwa weki ndani ya Miezi 3 mtakua byeeee...

    ReplyDelete
  6. I have a solution for them(friji), naomba aniandikie through laurynlaura84@yahoo.co.uk. pia facebook LAURA TURUKA na namba yangu ya simu ni +60104337773 nipo Kuala Lumpur, Malaysia ila nitakuwa Bongo ndani ya mwezi. au kama naweza kupata contact zake nipo ready kumpa ushauri. I am a personal wellness coach huku

    ReplyDelete
  7. hiyo kali

    ReplyDelete
  8. Usinye soda pia dada sina sukari nyingi sana. Kuwa mtu wa maji na natural juice

    ReplyDelete
  9. UZOEFU WANGU:

    mimi ni kijana wa miaka 36. Mnamo mwezi February tarehe 8, nikiwa nimelala usiku saa sita, ghafla nikaanza kuishiwa pumzi, kifua kinabana na jasho jingi. Nikakimbizwa hospitali usiku huo huo, ikagundulika nina hypertension (BP?). Nikafanya vipimo vyote (ECG, cholesterol, sugar) vyote vikaonekana ni kawaida. Daktari akashauri nipunguze uzito kwani alisema ndiyo chanzo cha tatizo langu(nilikuwa na kilo 92; urefu 171cm. Immediately nikaanza shughuli kama ifuatavyo:

    - Asubuhi walking/jogging/running kilometa 5, siku 5 kwa wiki
    - break fast ya matunda tu
    - No lunch
    - Dinner kama kawa ( ila smaller portion, no red meat, no chips, no michemsho, no kiti moto )
    - No beer

    Huwezi amini kwa miezi miwili tu nimepungua kutoka 92kg mpaka74kg. hakuna cha presha, wala kitambi wala nini. Kwa hiyo hujachelewa dada yangu, anza. Ingawa inataka moyo sana, kwani mwanzoni inakuwa mateso sana, ila baada ya wiki 2 utaona kawaida tu

    ReplyDelete
  10. cha msingi hapo ni mazoezi ya kufa mtu muache uvivu kabisa jueni kuwa ni kwa faida yenu wenyewe. so bidii inatakiwa sana ukiambiwa kupunguza mlo yaani maanisha kweli kwa vitendo,pia jifunzeni kufunga, mkifunga kwa muda wa mwezi mmoja kula ni saa moja jioni na ni mlo laini msile daku ,mkimaliza tu huo mlo laini ni mpaka kesho yake saa moja jioni tena mtapungua vifriji.baada ya mwezi mnatakiwa kujicontrol ulaji wenu.

    ReplyDelete
  11. Dawa ya kifriji ni kuachana na vyakula vitamu na vyenye mafuta. Mawali, ugari, makeki, chips kuku, masoda, mabia, majuice, maji baridi, masteki na kujaza sahani kwa vyakula. Pendelea kula chakula kidogo kwa wakati. Matunda na mboga ndio ule kwa wingi. Kunywa maji moto hata siku za joto. Kuku kula kipande kimoja tu kwa siku, yai moja. Pendelea samaki zaidi kuliko nyama za ng'ombe. Sukari weka kijiko kimoja tu kwenye kikombe. Safari ndogo ndogo nenda kwa miguu. Punguza kulala lala sana, pendelea kuamka mapema. Kuku wa kienyeji ni bora zaidi. Na mazoezi ni mazuri, kama uko serious basi ukifanya mazoezi ya nguvu kila asubuhi hususan sit-up basi kifriji kitaondoka miezi mitatu tu.

    ReplyDelete
  12. Kwa ushauri wangu ni hivi:
    Asubuhi kunywa juice ya maji ya moto yanasaidia kuondoa gesi tumboni.Na baadae kunywa juice ya machungwa bila ya sukari.Halafu unaweza kula brown bread toast mbili na matunda kidogo na chai bila sukari hiyo ndio breakfast.Na baada ya hapo kunywa maji mengi mpaka mchana unaweza ukapata ugali na samaki na mboga za majani lakini usitumie mafuta wala nazi.Ni chakula cha afya na sio cha kunenepesha kutokana na vitamins ni muhimu kwetu.Haimaanishi kama unajaribu kupungua uzito au unene ndio usile hapana unaweza ukajiumiza badala ya kujiponesha.Na usiku chakula chako kiwe ni matunda unaweza ukatengeneza "fruit salad"ikawa ni kivutio zaidi na bila kusahau kunywa maji kwa wingi at list 2lt kwa siku.Na pia jitahidi kunywa maji ya moto usiku pia kabla ya kulala kwa sababu inasaidia sana kuondoa gesi ya tumboni ambayo ni moja ya kutoa kitambi.Sikunyingine kwa mchana pia unaweza kutengeneza salad ukalia na ugali.Ugali ni chakula kizuri hakina chumvi wala mafuta kwahio usiogope.

    Naomba uwache kutumia SODA,BEER,MAFUTA,NAZI,SUKARI NYINGI,CHUMVI NYINGI.NA KUCHAKUA CHAKUA HOVYO.

    Naomba usikae kwa muda mrefu au kutumia gari mara kwa mara.Jizoeshe mazoezi hasa kwa jioni kwa kua ni muda muafaka japo kwa kutembea kwa muda mrefu kidogo au kama utajiweza kukimbia kidogo ili utokwe na jasho mwilini.Na kua mtu wa kujishughulisha mara kwa mara.Nadhani hayo yatakusaidia bila shaka kupungua kidogo kidogo na inataka moyo.

    ReplyDelete
  13. kupunguza kifriji:
    Doze:nyo:
    1. Usinywe yote mara moja, tumia polepole toka asubuhi saa 12 mpaka saa 12 jioni.
    2.Usichanganye na kitu chochote.
    3.Au iweke kwenye friji
    4.Ukisahau kutumia siku moja, umeharibu tiba anza upya
    siku idadi
    1 4
    2 8
    3 12
    4 16
    5 20
    6 20
    7 16
    8 12
    9 8
    10 4
    jumla 120

    ReplyDelete
  14. Acha kusumbua watu,hakuna lolote hapo ni porojo zako tu.Kama ni kweli kwa nini usieleze kwa lugha sanifu kabisa ueleweke hadi unaficha nini kwa kuzunguka mbuyu?

    Huyo hamna kitu ameamua kuchokoza watu ili wazuge kidogo hapo.Wabongo hamna kazi kweli za kufanya du!!

    ReplyDelete
  15. UWE UNALALA KIFUDI FUDI MARA KWA MARA

    ReplyDelete
  16. Google ina majibu yote.just visit it

    ReplyDelete
  17. Nakushauri mfanye mazoezi ya tumbo. Unala chali (ukiangalia juu), mikono yako ikiwa chini ya kichwa(kisogo), miguu imenyooka. Halafu wakati unanyanyua mwili, hakikisha unakunja mguu mmoja, na kukutanisha uso na goti. kwa mwili wenu zoezi hili ni gumu kwa mnaweza kuanza kwa mmoja wenu kusimama mbele yako wakati umelala chali, anaishika miguu yako miwili tumboni kwake na wewe unafanya kunyanyua mwili wako ili ushike vidole vya miguu yako. Vilevile ukiwa umelala chali, anasimama nyuma ya kichwa chako(akikuangalia), ikamate miguu yake vizuri(ili upate balance) halafu inyanyue miguu yako kuja kwake, yeye atakua kila inapokuja anaisukuma kurudi chini, na wewe kazi yako itakua kuirudisha. fanya kadri mwili unavyoruhusu, kwa kawaida unaanza kidogo na kila siku mazoezi huongezeka kwa sababu misuli itazoea na mwili utaanza kuwa mwepesi. Ukimaliza hapo kunya maji ya vuguvugu. Misuli itapata moto, mafuta yatayeyuka na hatimaye tumbo litakaza.
    Zingatia pia aina ya vyakula mnavyotumia. Mafuta machache, vyenye sukari kidogo, protin ya kutosha. Pia salads na matunda vyaweza kuwa mlo mzuri kwa mchana. Pia, jaribuni namna mbalimbali ambazo mwaweza kupata lishe ya usiku hasahasa mkifanya matumizi makubwa ya stuli(kiti cha kukalia) Asante na pole sana. Mazoezi ni Afya, na Afya ni Uhai, kwa hio mazoezi ni uhai.

    ReplyDelete
  18. hei kila staili inagoma teh! teh! hata chuma nanihii inagoma.
    basi kazi iko hapo.

    ReplyDelete
  19. we "anon" Apr28,11:56 am duuuu .... hufai hata kidogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...