Mdau Yohana Benjamin akiwa na kigari cha mbao alichotengeneza yeye mwenyewe kumsaidia kutoka sehemu moja hadi ingine. Anaomba msaada wa 'wheel chair' ili aweze kuendelea na masomo shule ya Sekondari Pugu
Mdau Yohana na kigari chake
Kigari cha mdau Yohana

Naitwa Yohana Benjamin, nimezaliwa mwaka 1993 Kigoma. Nimesoma shule ya msingi Kabanga mazoezi, Kigoma wilaya ya Kasulu. Mimi nina ulemavu wa miguu, hata hivyo nimebahatika kumaliza na kufaulu vizuri mtihani wa darasa la saba (7) mwaka 2010.

Nilibahatika kupangiwa Shule ya Sekondari Mwadui , Shinyanga. Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Mwadui alinipokea vizuri sana lakini akawa na wasiwasi mkubwa sana juu ya mahitaji muhimu kwangu kutokana na aina ya ulemavu wangu. Kwa mfano, mazingira ya pale shule kama vile kupanga ngazi, au kwenda kujisaidia ndio ilikuwa changamoto kwa Mwl Mkuu wangu na mimi mwenyewe. Ilifika mahali nikajipangia kula mlo mmoja wa jioni tuu, ili nisije kuhitaji kujisaidia mchana.

Ikifika usiku nawaomba wenzangu wanisaidie kunisindikiza kwenye vichaka ndio nipate kujistiri. Hali hii ilinisumbua mimi na mwl mkuu wangu, ikabidi nifanye uamuzi wa kwenda kuomba msaada kwa afisa elimu wa wilaya na hatimae afisa elimu mkoa, lakini kwa bahati mbaya wote walishindwa jinsi ya kuniwekea mazingira yakuniwezesha kuendelea na masomo. Nikarudi nyumbani. Siku kata tamaa, nikaamua kuja DSM kuonana na Idara ya Elimu Maalum, Wizara ya Elimu na Ufundi.

Mungu si Athumani, nimemkuta Bwana Mwiga Afisa katika Idara hii, ndio amekubali kunipa barua nikajiunge na Shule ya Sekondari Pugu. Ndugu zangu mtakaojaaliwa kuona taarifa hii, ninacho omba kwenu nisaidiwe kupata wheel chair inayonifaa kujisukuma kwenda darasani kutoka bweni na kwengineko.

Katika picha hii, kigari kinacho nisaidia nimebuni na kutengeneza mwenyewe baada ya kusaidiwa kuletewa vifaa kama mnavyoona. Najiendesha kwa kutumia mkono mmoja kuendesha usukani na mkono wa kulia ndio najisukumia chini. Nina penda na kumudu masomo ya sayansi, hisabati na maarifa ya jamii. Malengo yangu ni kusoma hadi chuo kikuu. Nikiwezeshwa nitaweza.

Hapa DSM nimepokewa na ndugu yangu Bw. Robert Revocatus

Simu namba 0763 299960 au 0714 495951

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. mungu mkubwa! UNCLE kama kaiwada tutaftie bank detail ili tuweze changia chochote, thanx

    ReplyDelete
  2. pole sana mwanangu ni kweli tuwekee hata m pesa namba tutatuma umenigusa saaana na Mungu akutie nguvu. Nimependa una juhudi na unapenda masomo na ndio yatakayokutoa kimaisha

    ReplyDelete
  3. Jamani Watanzania hata wheel chair tunashindwa kitu ambacho hata kwenye ndege unasafirisha bure na mahali popote duniani vinapatikana bure hii ikoje???????????????????????.

    ReplyDelete
  4. KWELI INABIDI TUWAULIZE HAO VIONGOZI TULIWACHAGUA BWANA MDOGO AMETOKA SHINYANGA,SHINYANGA HALMASHAURI YA UKO HAINA PESA YA KUWASAIDIA WALEMAVU?AMEENDA WIZARANI HAKUNA FUNGU AU WIZARA INAYOWASAIDIA WALEMAVU?MTU MWINGINE ATASEMA SERIKALI INA MAMBO MENGI,HIVI JAMANI SERIKALI KUWA NA MATUMIZI MAKUBWA WIZARANI RAIS KUPAA MAJUU NA KUTUMIA NDEGE YA BEI KUBWA NA KUWAACHA WALEMAVU KUTESEKA HIVI NI HAKI HIYO?
    KWELI SERIKALI INATESA WALEMAVU KWA KUSEMA WAZAZI WAO WAWAHUDUMIE WAKATI WAZAZI HAWANA UWEZO.
    JAMANI TUNAWALEMAVU WANGAPI TANZANIA WASISAIDIWE NA SERIKALI?SASA WAZIRI HUSIKA ANAKULA PESA ZA SERIKALI BASI TUSIWE NA WIZARA INAYOUSIKA NA WALEMAVU.
    NILIONA PICHA SIKU MOJA YA MLEMAVU WA AKILI AKIWA AMEFUNGWA KAMBA MKOA WA TANGA HIVIB HUYO SI JUKUMU LA SERIKALI KUWATUNZA MAANA MZAZI AJUI LOLOTE KUUSIANA NA ELIMU YA KUWATUNZA WALEMAVU WA AKILI SERIKALI IMEWAFUNDISHA WATAALAMU WA KUWATUNZA WALEMAVU.
    NACHUKUA NAFASI HII KUWAAMBIA WANANCHI WAWAULIZE WABUNGE NA WATOE HOJA YA KUUWASIDIA WALEMAVU WOTE NA WAWE NA IDADI YAO NA WASAIDIWE

    ReplyDelete
  5. Kweli hii inasikitisha sana kaka Michuzi; maana serikali yetu ingepaswa kuwa imetatua tatizo lake la wheel chair kupitia wizara husika siku nyingi tu ila ndio hivyo tena walio katika nafasi hizo wanajali maslahi yao binafsi kwa asilimia kubwa!! Tupatie akaunti namba tuweze kumchangia; tuambie ni shilingi ngapi hiyo wheel chair na michango ikikamilika kununua basi itekelezwe (usiwepo ufisadi katika hili)na kijana huyu atutumie picha akiw katika wheel chair yake katika blog hii baadae. twasubiri akaunti namba hiyo kaka

    ReplyDelete
  6. Hii imenigusa, manake kijana kajieleza kwa marefu na mapana kwa usahihi mkubwa kabisa, kweli inaonekana unabidii ya kusonga mbele,nakusahauri usikate tamaa ndugu yangu na Mungu atazidi kuwa nawe, sasa huo msaada unaweza kutumwa kwa nani?

    ReplyDelete
  7. Uncle michuzi hii imenitouch sana wekeni bei ya wheelchair,hata sisi wabeba box tuchangie.

    ReplyDelete
  8. kaka michuzi mimi naona nime elewa vingine,hapa kina chotakiwa ni msaada wa kumsaidia ndugu yetu kwa wakati huu mdau wa kwanza na pili mumefahamu vizuri,lakini ndugu zetu wengine naomba mufahamu sio time ya lawama au nani afanye au katoka wapi,tutizame jinsi ya kumsaidia huyu nduyu yetu basi hilo ndio muhimu.

    ReplyDelete
  9. Mmewahi kumsikia Dr. Prof. Stephen Hawking? Yuko kwenye wheelchair na hali yake ni mbaya kuliko wa huyo kijana. Jamaa ana akili sana. Huyo kijana wetu Yohana Benjamin naye inaelekea ana akili sana. Kwa nini ateseke hivyo? Yaani kweli viongozi wa Shinyanga wanatembea na mashangingi safi na huyo kijana wanashindwa kumpati wheelchair? Priorities ziko wapi au hawaoni walemavu kama si binadamu? Siku moja huyo kijana atapelekwa nje ya Tanzania na kufanya maajabu!

    ReplyDelete
  10. Serikali haiwezi kufanya kila kitu na ndio maana kijana ameotuomba mimi na wewe. Acheni excuses za kichoyo za kuilaumu serikali badala ya wewe kusema utachangia nini.

    Uwekwe utaratibu na kuwapo na akaunti za nje ya nchi ili wengine tuchangie. Ama uundwe utaratibu wa Michuzi Fund na iwe na akaunti nchi za nje (kwakuwa Michuzi anawawakilishi wengi kila nchi) ili ikitokea shida tuwe tunachangia.

    Wachowo wote tutatafuta wa kulaumu especially serikali-Kutoa ni moyo na toa leo na si kusema nani hajafanya

    NAomba kuwasilisha

    ReplyDelete
  11. Jamani ndugu zangu watanzania mbona tumezidi kulalamika kwa kila kitu jamaa anaomba msaada wa wheelchair sasa baada ya kudiscuss tutamsaidiaje tunaanza kuilamu serikali. Sidhani kama itasaidia kwa sasa kinachoitajika ni msaada si kila eneo tunaingiza tofauti zetu za KISIASA.

    Kijana weka account # hiyo wheel chair utaipata very soon.

    ReplyDelete
  12. Kijana weka au tupe account number hiyo wheel chair utaipata, uendelee na masomo yako, cha msingi usikate tamaa soma sana utafanikiwa "your dream will come true" kitu kingine na chamuhimu ni sali sana usimsahau Mungu wako,pls tafuta a/c no watu tukuchangie......

    ReplyDelete
  13. rahisisha zoezi kwa kuweka njia za kutoa msaada !

    ReplyDelete
  14. Wheel chair nzuri ni laki nne na nusu! Michuzi utatusaidia account number tuchangie. Mimi naenda dukani hapo Morogoro rd kuangalia hivyo viti nimeongea na ndugu yake as mentioned kwenye hii blog, i hope hakuna utapeli maana hapa bongo, Michuzi how would you cover this ili kuwe na regitimacy!

    ReplyDelete
  15. Ndugu Michuzi kwanza nikushukru kwa kazi nzuri unayoifanya kwa faida ya jamii. Hongera sana. Pichani (nimetuma kwenye gmail yako) nimemkubidhi bwana Robert Revocatus – 0763 299960 Whell Chair kwa ajili ya kijana Yohana Benjamin kama ulivyo onyesha umma kwenye blog yako na TBC1 kwenye taarifa ya habari yao ya hapo jana. Nimehakikishiwa kuwa kesho Robert atapelekwa Pugu Secondary ili akaendelee na masomo yake. Misaada zaidi itatikiwa ukizingatia hali yake na hali harisi ya shule zetu za umma. Kwa nyongeza tu nimekuja kujua kuwa Robert na Yohana ni watu wa Manyovu Kasulu. Zaidi mnaweza kuwasiliana naye.
    Asante sana kwa kazi nzuri. TEGETA OYEEE!.

    ReplyDelete
  16. Hongereni sana wadau wa Tegeta kwa kumfanikishia kijana jasiri ili aendelee na harakati zake. Mungu awabariki sana sana na awazidishie mara 100 pale palipopungua.

    ReplyDelete
  17. Ubarikiwe sana mdau uliyejitoa kumnunulia kijana wetu wheelchair!

    ReplyDelete
  18. ISLAM MPOSSOMay 01, 2011

    tunashukuru kama amepata maana ni kijana mkweli na muwazi wengi huwa wanajificha kama yeye

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...