Jumuiya ya watanzania ugiriki inasikitika kutangaza kifo cha mwenzetu OWEN SIRIPALA NANAYAKKARA kilichotokea ghafla J’pili 24/04/2011 jijini Piraeus.

Kabla ya kuja Ugiriki,Marehemu alikuwa mkaazi wa Kinondoni Dar mtaa wa Ikungi na Kanazi.

Alizaliwa 14/10/1972.

Hivi sasa tupo katika harakati za kumsafirisha akazikwe nyumbani.

Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin

INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN

- KAYU LIGOPORA

KATIBU MKUU

Juu na chini ni baadhi ya wadau wa Ugiriki wakiwa wamejikusanya msibani kuweza kutoa misaada ya hali na mali ili kufanikisha kusafirishwa kwa mwili wa marehemu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. RIP. Je huyu ana undugu na Mwalimu Mrs Nanayakara ambaye alikuwa Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Muhimbili kwa miaka mingi?

    ReplyDelete
  2. ndio ni Mtoto wa Mwl Sanura Nanayakara huyo huyo...
    Innalilah wa Innailahi Rajoon Msiba mkubwa muda si muda mrefu umepita Mr Nanayakara nae alitutoka, Pole mama Nanayakara

    ReplyDelete
  3. Mwenyezi Mungu amweke mahala pema peponi.. Poleni washkaji wa Umangani na mimi nilikuwepo hapo na nawajueni jinsi mnavyosaidiana katika hali kama hii.Endeleeni hivyo hivyo

    ReplyDelete
  4. Pole Mwalimu Nanayakara, Mungu aifariji familia ya marehemu.

    ReplyDelete
  5. Pole Sana Shangazi Bi:Sanura aka Mwalimu Sanura Nanayakara, pamoja na familia yote kule Mtaa wa Togo,na Mtaa wa Kanazi,Kinondoni kwa msiba huu mkubwa.Innalilah wa Innailahi Rajoon.
    mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi.
    AMIN

    Wadau
    Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja
    na Ngoma Africa band aka FFU

    ReplyDelete
  6. Poleni sana Ndugu, jamaa na marafiki (Mama Nanayakara). You are in my thoughts and prayers. May his soul rest in peace.

    ReplyDelete
  7. kwa habari zaidi tembeleeni website ya jumuiya http://www.tanzaniansingreece.org/matangazo.htm kupata update ya mipango ya mazishi

    ReplyDelete
  8. Mie nimeitembelea hadi nikaandika na email lakini sijapata majibu kutoka kwa mtu yeyote. ninafanya kazi huku katika kampuni kubwa hadi nikaelezea kwamba nataka niwasaidie watanzania na ajira na misaada mingi tu. nilichuniwa. haya, poleni na msiba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...