
SIKU: JUMAMOSI (30/4/2011)
MUDA: SAA 3:30 ASB – SAA 8:00 MCH
MAHALI: UKUMBI WA NKRUMAH-UDSM
KAULI – MBIU: “Tafakuri ya kina juu ya Azimio la Arusha. Je, Lina Nafasi katika Mjadala wa Katiba Mpya?”
MTOA MADA: Prof. ISSA G. SHIVJI
WAANDAAJI: SAUTI YA VIJANA TANZANIA (SAVITA – UDSM)
& PHILOSOPHY CLUB


Azimio la Arusha kwa sasa halifai tena kwani lilikuwa ni mawazo ya mtu mmoja. Ushauri wangu ni kuwa liwekwe kwenye vitabu vya historia na watu kulisahau rasmi. Mawazo yake sasa hayatekelezeki.
ReplyDeleteHata hayo unayoyasema ni mawazo yako. Ni ya mtu mmoja. Hoja ya kufaa au kutofaa kwa kitu ni usahihi na ubora wake, haijalishi yametolewa na nani? Nakushauri kasome vema historia, Azimio lilipitishwa na halmashauri kuu ya TANU, mwaka 1967? Swali: Je, Halmashauri kuu ya TANU ilikuwa na mtu mmoja? Nakushauri uhudhurie Kongamano hilo, au uangalie live ITV, kujua Azimio la Arusha ni nini hasa; lilianzia wapi, kwa nini... Nakushauri ulitafute na kulisoma. Huko Ughaibuni, watu hulichambua na kulichukulia Phd. Hapa nchini, watu wa aina yako, mnalidharau - pengine pasi na kulisoma. Huko Ughaibuni, Tanzania iliheshimika kutokana na misingi ya utu, usawa na uadilifu chini ya Azimio la Arusha. Hapa nchini, tunalitukana Azimio, tewna kwa hoja dhaifu, zisizo na mantiki.
ReplyDelete