Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mh. Jenista Muhagama(katikati) akiongea na maafisa Habari,Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na wakala wa serikali ndani ya Ukumbi wa Pius Msekwa leo mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Uhusiano na Elimu kwa Umma Bungeni Bw. Jossey Mwakasyuka (kulia).
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda(kushoto) akisalimiana na mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana mara baada ya kuzungumza na maafisa habari, Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara, Taasisi za serikali, Mikoa na wakala leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Clement Mshana nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka nje ya ukumbi wa bunge, leo mjini Dodoma.Katikati ni Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeye.
Spikawa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda(wa nne kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na maafisa Habari,Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na wakala wa serikali nje ya Ukumbi wa Pius Msekwa mara baada ya kuzungumza nao.Viongozi wengine ni Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mkangara (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana(wa tano kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Uhusiano na Elimu kwa Umma Bungeni Bw. Jossey Mwakasyuka(wa pili kutoka kushoto).Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mnapikwa

    ReplyDelete
  2. Huyu Mkurugenzi wa Habari wa Bunge, ni mchapakazi! Nimekuwa nikisoma semina zinazofanywa na kitengo cha habari cha bunge. Hii inaashiria kujenga uhusiano mzuri kati ya bunge na vyombo vya habari. Hongereni sana.
    Mdau, UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...