Kocha Jamhuri Kihwelo ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi chake cha U23 kwa lengo la kukiimarisha kabla ya mechi ya marudiano ya michuano ya Olimpiki dhidi ya Cameroon itakayofanyika Jumamosi (Aprili 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni Kigi Makasi kutoka Yanga, David Luhende (Kagera Sugar), Jabir Aziz (Azam), Kelvin Chale (Simba), Ali Lundenga (Kagera Sugar), Mrisho Ngasa (Azam) na Juma Abdul (Mtibwa Sugar).
Baada ya uamuzi huo wa kocha, baadhi ya washabiki na vyombo vya habari
vimeonesha mashaka juu ya umri wa Ngasa. Kwanza TFF inapenda kuweka wazi kuwa umri chini ya miaka 23 ndiyo sifa ya msingi ya kuchezea timu hiyo.
Hivyo uamuzi wa kocha kuita wachezaji hao mbali ya vigezo vingine, cha umri pia kimezingatiwa. Umri wa Ngasa aliyezaliwa Aprili 12, 1989 ni miaka 22. Wachezaji wengine walioongezwa na tarehe zao za kuzaliwa ni Makasi (Februari 2, 1990), Luhende (Januari 21, 1989), Aziz (Januari 1, 1989), Chale (Juni 19, 1992), Lundenga (Septemba 12, 1990) na Abdul (Novemba 10, 1992).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Mmh..sijui kuhusu ngasa..lakn huyo Kevin Chale hajazaliwa 1992..tumesoma naye sekondari, na tunalingana umri. kupunguza miaka mi5 hapo..!
ReplyDeleteMuangalie tu msije mkatuletea aibu ya Serengeti Boys.
ReplyDeletehakuna sababu ya kuchakachua umri kama wameshapita umri unaotakiwa. Michezo ni Furaha hata hivyo.
Mbona hilo jambo la kawaida sana bongo. Hao wote wanaopinga wote waulize umri wao uone jinsi utakavyorushiwa marungu..Rafiki zangu kibao kwanye FB wanadanganya umri zao. Halafu mimi ninachoshangaa FB in option ya kuficha umri sasa kuliko kuachia umri wako wa uongo hadharani uonekane kama mjinga vile kwanini usifiche? Unamdanganya nani? Wengi nilisoma nao na walikua wakubwa kwangu leo unaona wadogo kuliko mimi miaka mitano...Agrrrrrrrr....
ReplyDeleteKosa la serikali inaachia age discrimination ndio maana watu wanadanganya umri zao hivyo. Kila kazi lazima kuonyesha umri nani ataacha kudanganya???
Lets start from the top sio kuwaonea hawa kama game bado wanalo who cares?
UMRI WA MTU WEWE UNAKUHUSU NINI KAMA YUKO FIT NA WEWE UMECHO HUWEZI UKALINGANA NAE,KWANI NI KAWAIDA TU WATU KUSHUSHA UMRI WAO,HATA HIVYO STILL YOUNG BWANA,KUSHUSHA MIAKA MITANO SIO HOJA WATU WANASHUSHA MIAKA 20 UNASEMA MITANO!!!!!1MKIWAANDAMA SANA NYIE WENYEWE KWA WENYEWE WATASTUKIWA KISHA TUTATOLEWA KATIKA MASHINDANO,,,AHLAM UK
ReplyDeleteIli kujiridhisha haitokei aibu kama ile ya Serengeti boys tena, basi nafikiri hao vijana wanaowekewa mashaka wakaapae mahakamani. Nafikiri mashaka ya wadau kama huyo anaedai alisoma na Kevin Chale ni vizuri yakafanyiwa kazi hata baada ya ufafanuzi huu wa Katibu. Maana watu wanaishi pamoja na wanafahamiana na mara nyingine wanaambiana ukweli, lakini baadae wahusika wanaficha ukweli huo ili kuweza kufanikisha malengo au maslahi fulani (kama kuchezea timu ya taifa au kupita mchujo wowote wenye ukomo wa umri). Wazo langu ni kwamba, TFF inaweza kuomba ushirikiano wao ili ijiridhishe hakuna majungu katika swala hili, maana wote tunajenga nyumba moja na hatuna haja ya kunyang'anyana fito.
ReplyDeleteSina kumbukumbu kama kuna mtu aliyewajibika au wajibishwa wakati ule wa aibu ile (Ya Nurdin Bakari), lakini tunaomba katu swala lile lisijirudie, na ikitokea kwa makusudi likajirudia, basi itakuwa ni vigumu kuwaelewa TFF na itabidi watu wawajibike. Kwa hiyo tunaomba mjiridhishe wakati bado ni mapema na sio baada. Dadisi
ankala,hoja zingne bwana cdhan km znaumuhimu sana ktk maendeleo yetu cc km watanzania,mpira una miaka yake,namaanisha mpira ni biashara na biashara ya mpira ni uwezo + umri,ss inasikitisha kuona mpaka leo mtanzania wa sasa anataka mchezaji wa tanzania acpunguze umri,co kweli na haiwezekani hata cku moja!wenzetu waliotutangua wa magharibi wana ,iundo mbinu ktk soka miaka nenda rudi lkn bdo wanapunguza,je cc ambao hata accademy zetu ni km sehemu tu yenye mkusanyiko wa vjana,hv akina eto'o,drogba,essien,gyan wana miaka ya kweli??,tuache ushamba na kutoa ushuhuda uco na msingi hapa,hata km umesoma na mtu au ndguyo cc hatujali,LA MSINGI NI KUSHINDA BASI,ONDOENI ROHO ZENU MBAYA HAPA!HAKUNA MTOTO WA MIAKA 16 ANAWEZA KUKIMBIA DAK.90 TOKA AFRICA.MAKOSA YA AKINA NURDIN YANATAOKEA TU,WATZ AMKENI JAMANI.
ReplyDeletehata ulaya wanadanganya umri,huy kijana km angekuwaa na faida ktk nchi hii wasingemchoma,je documents za kupunguza miaka kazitoa wapi km wao hawafoji miaka??,somen link hii nyie waosha vinywa na c kukalia nani kupunguza miaka au nn cjui kimefika wapi http://rivals.yahoo.com/highschool/blog/prep_rally/post/21-year-old-poses-as-middle-school-football-
ReplyDeleteWaswahili husema kosa si kutenda kosa bali ni kurudia kosa. Ndicho tunachokifanya hapa. Kwa vile Cameroon walichezesha vijeba haina maana kwamba na sisi tuchezeshe vijeba. Tuchezeshe chipukizi wakomae, hata wasiposhinda mashindano ya chipukizi watakuwa hodari watakapofikia kucheza kwenye mashindano ya wakubwa wenzao kwa sababu ya uzoefu wa kucheza na vijeba.
ReplyDeleteMrisho Ngassa alianza lini kucheza ligi kuu? Alianza kuchezea timu za Dar (Yanga kisha Azam) miaka angalau mitano iliyopita. Kabla ya hapo aliichezea Kagera Sugar. Leo unasema ana miaka 22. Ina maana alianza kucheza ligi kuu akiwa na chini ya umri wa miaka 17? Watanzania wenye umri wa miaka 17 mnawafahamu? Ni kama vijana wa Form III. Kwa umbo la Ngassa angecheza ligi kuu na umri huo?
TFF tunaomba msitudhalilishe na kututia aibu tena. Chonde chonde tunawaombeni jamani. Bora tufungwe na chipukizi kuliko kupigwa bao licha ya kuchakachua umri wa wachezaji.
Sikieni kilio cha wadau, chonde chonde!