good morning.
Nimerejea bongo na kupata fursa ya kwenda mikoa ya kusini kukagua maendeleo ya wananchi kwa juhudi “binafsi”
Ila nikakutana na mambo ambayo nilishindwa kuyaelewa labda wanablog wanaweza kunisaidia
Tunapata picha gani kutoka kaika hizi picha?
Naomba wanablog ya jamii wanisaidie
Nawasililisha
Picha zote kwa hisani ya Hildebrand shayo
Kuvua viatu huenda ni ktkt juhudi za kulinusuru zulia ama kompyuta iliyopo ofisini humo.
ReplyDeletePia asishangae gari ya serikali kubeba mkaa maanani sehemu ya kunusurumaisha kama huko aliko toka kuna unaunafuu basi aelewe kwamba huko ndio uhalisia
hiyo ni jinsi gani inaonyesha serikari inaleta udini mpaka kwenye ofisi za umma,gari ya serikari usishangae.Shemeji Tanzania Kikwete(S.T.K.)
ReplyDeleteYaani usishangae hapo mimi nilikwenda Mtwara wakati fulani nikashangaa kumuona secretary wa mkuu wa mkoa kila anapoingia kwa boss wake anavua viatu nilishangaa ilipofika wakati wa kuingia sisi tukauchuna lakini nadhani hawakuwa na furaha maana hata huyo boss alikuwa kavua viatu.
ReplyDeleteGari la serikali kubeba mkaa!! sina la kusema; Watu kutakiwa kuingia na viatu katika ofisi ya serikali, hii inawezekana imeamuliwa na PS na wahudumu tu..bossi hajui.Kama anajua na kubariki,inawezekana anaweka imani za kidini katika ofisi ya serikali, ama ni msafi sana, anaogopa vumbi.Na ninaamini huyu atakuwa mwanamke(samahani kwa akina mama).Naomba aache mara moja kwani hii haikubaliki hata kidogo.
ReplyDeleteEnter your reply...na yeye avua au ni kwa wale tu ambao co ofic yao
DeleteHuyo mtu ni msafi, fikiria umetoka nyumbani kwako Tandale kwa Mtogole au Buguruni Marapa, na unakwenda ofisini Kariakoo au Posta, huko njiani ulikopita umekutana na mifereji mingapi inayotoa maji chooni na kutiririsha barabarani?, umekanyaga makohozi mangapi yenye TB na yasiyokuwa na TB?, umekanyaga mikojo mingapi ya watu wanaokojoa hovyo barabarani ukitoa vinyesi vya mbwa na paka wanaodhurura hovyo barabarani?. Hiyo ni katika kuweka mazingira ya ofisi yake safi, kama ungeambiwa vua nguo zako mlangoni ndio ulipaswa ulipaswa ushangae.
ReplyDeletetatizo barabara zetu zimejaa vumbi na tope. wadhani ni watu wangapi wanaingia humo ofisini? tukilekebisha miundo mbinu yetu mambo yatakuwa safi tu na pia kama wanazuri ni waza hawana machine maarumu ya kufanyia usafi so ps inabisi ajiwahi ili kila siku mgongo usimuume. sidhanni kama ni udini ila wazi barabara na tunapotoka ndo tatizo la kwanza.
ReplyDeletemkaa na gari za serikali du hilo ni moja ya shida za kibongo maana hatujawa na usimamizi wa mali zetu kwa maadili. siku zaja may be mambo yatabadilika.
sasa mkuu wa wilaya anageuza ofisi ya umma kuwa msikiti?
ReplyDeleteHuu ni upuuzi tu ambao watanzania tunaulea katika secta mbali mbali kila kukicha
ReplyDeletewewe ukienda field kwa gari la ofisi hununui zawadi kwa familia yako? hivi akina obama na cameroon wanaposafiri sehemu mbalimbali duniani hawanunui zawadi kwa familia zao? km ndiyo, wanaweka wapi mizigo hiyo kama si kwenye ndege za serikali wanazosafiria? wakati mwingine tuache kulaumu na kulalamikia mambo ambayo hata wewe utafanya ukiwa katika nafasi hizo.
ReplyDeleteAnon Apr 06 11:33:00 AM
ReplyDeleteAcha utoto wewe ndiye MDINI. Hapa wanabajeti zuria ndo maana wanataka uvue viatu wajua kule kuna udongo mwekundu hivyo hawataki uchafu, Sasa wewe wewe unakimbilia udini
Je kama soksi zimetoboka au zinanuka si itakuwa kituko humo ofisini? Nadhani sio sahihi kuvua viatu ofisini. Kama ni zulia la sufi si watasafisha bwana!! Kwa nini waweke zulia kwenye public ofisi kama halisafishiki? Basi waweke tiles kama wanataka netness kwenye ofisi. Gari la serikali kubeba mkaa ni hali tu ya maisha. Dreva mshahara wake ni Tshs 80, 000/ na gunia la mkaa mjini ni Tshs 20,000= mpaka 30, 000= lakini akipata trip ya kupitia maporini gunia la mkaa linauzwa Tshs 5,000= Je kwanini asinunue? Kisa gari la serikali wakati hali ya maisha kwa Tshs 80,000= hayaendi? Mimi sina tatizo kwenye hilo la mkaa kwenye gari la serikali!
ReplyDeleteMdau
Kwa gari la serikali huu unatosha kuwa ushaidi wa kufukuza m2 kazi ila kwa hapa kwetu haiwezekani. Kuvua viatu ni ushamba tu ila kama ni mambo ya dini Mungu apishe mbali
ReplyDeleteKuna vifaa vinaharibika kwa vumbi jamani. Ufinyu wa fikra unawapelekea watu kufikiria ni dini kwa sababu tu watu huvua viatu wakiingia msikitini. Watu wengi tu waliostaarabika huvua viatu hata majumbani kwao, pengine hata wewe unayeongea dini hapa unavua viatu kwa sababu ya zulia uliloweka nyumbani kwako! Mimi naishi huku Scandinavia, Mashuleni kote wanafunzi na walimu wanavua viatu wanapoingia darasani kwa ajili ya kukwepa tope na maji!
ReplyDeleteNa mie naomba kuuliza swali kwa wataosoma maoni, hivi kama umepewa gari la ofisi kwenda kijijini wakati unarudi unakutana na mkaa wa bei nafuu kuliko mjini, hivi ukuchukua gunia moja na ukaweka kwenye gari la serikali ni dhambi? mbona magari ya serikali yakishiriki kwenye shughuli za msiba huwa hatulalamiki maana zote ni shughuli binafsi?Mie naona vibaya mtu katoa gari ofisini linakwenda kwa shughuli ya kubeba mkaa au sokoni lakini kama ni unatoka kijijini kikazi alafu ukakuta mkaa nadhani si dhambi lakini iwe kwa kiasi.
ReplyDeleteTanzania hakuna vifaa vya kusafishia zulia na barabara zetu hazina pavement, kufuga kuku na mbuzi ni jambo la kawaida, kwahivyo kukataza watu kuganyaga zulia na viatu ni kumnusuru mwenye ofisi na vumbi, mavi ya kuku na bata, pia tarishi kuhangaika kulisafisha zulia ni bora watu wavue viatu. Ndio maana Bush alipigwa kiatu. Maana kiatu ni kitu kichafu.
ReplyDeleteAcheni upumbavu. Mimi nimesoma Mzumbe A'level na tulikuwa hatuingii bwenini na viatu.Bweni la Mzumbe ni la serikali pia. Mzumbe ni sehemu yenye udongo mwekundu na matope sugu. Kutoingia na viatu bwenini haikuwa sera ya serikali, lakini kwa sababu za kiusafi tuu wanafunzi wakakubaliana kutoingia na viatu bwenini.
ReplyDeleteSiyajui mazingira ya huko "N"twara, lakini kuvua viatu huko inawezekana ni kwa sababu za kiusafi tuu.
Acheni ujinga.
hildebrand shayo ama kweli hukati tamaa, kulikoni kusini? kwa nini usiende kwenu Moshi? au unafikiria utakubalika huko? juhudi zako za kutembelea maendeleo ya wananchi wa kusini zimewashinda wao wenyewe, wewe ndugu yangu utaweza kuwasaidia?
ReplyDeletePili hiyo picha ya kutoa viatu kidogo imenipa wasiwasi hivi watumishi wa huko hawajali afya za wafanyakazi wao? je kitendo hicho chaweza kufanyiak katika ofisi za mkoa wa Arusha? au nayo hii mikoa ina tofautiana?
Je mkuu wa mkoa ambaye sasa hivi anakaimu huko Dar es salaam anaielewa hii hali? au ni maamuzi ya waliocko chini yake?
Mbunge wa Lindi mjini (CUF) anaweza kutupa maoni yake kuhusu hili la kuvua viatu? je hawaoni kama wanadhalilisha watu na wafanyakazi wa kusini?
Je mlengwa ni mwanachi anayekuja kutoa au kupata masaada hapo ofisini au ni wafanyakazi wa ofisi hiyo? anayetakiwa kuvua viatu ni nani hasa?
Tusipoangalia sababu kama hizi zitawafanya vijana wetu wamalizapo vyuo wakatae kwenda kufanya kazi katika mikoa kama hii!
Nashauri wahusika hapo mkoani na wilayani waliangalie
Kuhusu gari la mkaa, hapo ni sina cha kusema kwani kila dereva wa magari ya serikali wanakula urefu wa kamba yake
wengine wala katika:
mafuta kuchakachua mafuta
tyre kubadilisha magurudumu
kupakia mikaa
kupeleka receipt za kugushi
nk nk.
ila namshukuru hildebrand shayo kwa kutupa vile vitu ambavyo pengine sisi tulioko huku na kwingineko vinaonekana ndiyo hali halisi ya Bongo
Mie sirudi ngooooooooooooooooooooooooo!
pole mliorudi!
Aksante Hildebrand shayo
ReplyDeletehadi lindi unafika? kumbe umekusudia kufanya kweli? kazi kweli kweli!
mwaka 2015 sijui watakunyima kwa pingamizi gani!
ndugu yako January makamba yumo mjengoni, wewe unakagua maendeleo ya watu wa kusini kwani waheshimiwa wa huko wako wapiiiiiiiiii?
ila nikuombe kitu kimoja wewe unauchungu gani hata uende huko kuangalia maendeleo ya wananchi?
kakutuma nani?
na taarifa unampatia nani? CCM? Chadema?, CUF? au wafadili?
Anagalia usije ukawa unatumika ( kitu ambacho naamini huwezi kufanya)
ila kuna haja ya kutupia jicho huko kusini manake wafadhili wamefanya mkoa wa "kusini mradi" kuna program hadi za kumfundisha mkulima namna ya kufuga "mbuzi wa kisasa"
mimi siamini kama hicho ndicho wanachi wa kusini wanahitaji! Fo Gods sake they need more than that, ila karne hii kuambiwa kuvua viatu tena ofisi ihusiyo mahakama katika ngazi ya wilaya inanipa shida kidogo.
hivi, swali la kizushi, viongozi wanapokwenda huko hawalioni hili? au watu wa kusini hawana haki ya kujilinda?
Wabunge wa kusini kazi ipo kweli kweli
Mheshimiwa Membe kazi unayooooooooooooooooo!
hii kungekuwa na data bank ya number za magari ya serikali, hapa moja kwa moja tungeelewa gari hili ni la mradi gani,
ReplyDeleteofisi gani,
dereva wake ni nani lilikuwa
katika safari gani,
nk nk
ila kwa vile miundo mbinu hiyo ni kama siri, basi hakuna nji tumshukuru tu hildebrand shayo kutulisha mismanagment ya hela za walipa kodi tanzania> what can we do!
nasailisha
acheni kuweka hisia za kidini, hakuna udini hapo ila ni fikra finyu kuhusu utunzaji wa kompyuta nimeona office nyingi hata ngara kagera ambako hata waislam niwakuhesabu,
ReplyDeleteAnkal namshukuru sana huyu mdau aliyeleta hizi taswira. Kwa kweli kuna makosa makubwa sana hapo. Kuvua viatu???kwa nini kuvua viatu?Kwanza si afya kuvua viatu. Pili hiyo ishu ya Mkaa wala usishangae sana fedha za walipa kodi zikichezewa hivyo. Hii picha mpelekee Pinda atajua kodi za wananchi zinakwenda wapi.
ReplyDeleteNa ukitaka fanya ziara rasmi tembelea Mabaa huko Sinza, Kinondoni, Tabata, Kimara, Mbezi hata siku na saa za kazi uone. Utakuta STK , STJ yakiwemo yale ma Masangingi ya Pinda yameegesha huku watumishi wa Umma wakikata kilaji;
Heshima na Maadili Serikalini vimeshuka sana...sina hata la kusema
duh ukisikia majungu ni hayo hata wewe kama una nafasi kazini ya kupata gari utabeba mkaa ila kwakua kabeba bossi yamekua hayo nyie mnaesiba mpa madaftari mkawapa watoto waende nao shule hamsemikingine kuvua viatu kinausiono gani na udiniunapotaka kusema kitu fikiri mara mbili ongea kwanini tunavua viatu sio udini naona umekereka sana na dini ya mwenzio jichunguze kwanza wewe ndioutoe kasfa kwa mwenzio duh binadamu hatupendani kabisa bado sijajua unataka nini hasa.
ReplyDeletedu! huyu jamaa juzi nilikutana naye pale Bond st, tarehe 4/4/2011 saa 8.30 mchana akiingia duka moja kama sikosei debehnham, kweli kuna watu wenye moyo na maendeleo ya wabongo!
ReplyDeletehildebrand bongo hapakufai! rudi kwa malkia babaaaaaaa
Kitu kidogo udini, mmefanya utafiti mkaona hivyo? mbona mmekuwa too emotional jamani! hebu ulizeni kwanza halafu ndio mseme! mbona mnaleta chuki zisizo na mantiki yeyote hapa?
ReplyDeleteHii ya mkaa imeniuma sana! yaani kodi yetu hivihivi bila sababu Jamani inauma sana, ingawa kwao ni kawaida na si serikalini tu hata kwenye mashirika hiyo ipo tena sana.
ReplyDeleteKuhusu kuvua viatu kila ofisi ina utaratibu wake
Mdau Usa river
Hatujui sababu za kuvua viatu, lakini sidhani kama ni hoja sana.
ReplyDeleteHivi kama mimi dereva wa gari la serikali nilitumwa mahali then wakati wa kurudi nikabeba kuku wanne na mananasi sita na nyanya tatu itaandikwa sawasawa na kubeba mkaa?
jamani wapendwa naomba niwakumbushe kuwa kuvua viatu si swala la kidini ila ni swala la usafi kama mtu anajali usafi sio lazima uambiwe uvue viatu wewe mwenyewe utavua tu.mbona tukiingia kwenye majumba yetu tunavua viatu mlangoni?
ReplyDeletemijini ni rahisi kuingia na viatu kwa kuwa sehemu nyingi hasa za mijini kuna lami hivyo sio rahisi kuwa na tope kwenye viatu, lakini kwa vijijini sehemu nyingi wananchi huwa na tope kwenye viatu vyake hasa kipindi cha mvua hivyo ni rahisi kuharibu usafi wa ofisi ukiruhusu kila mwenye tope mguuni asafishie viatu vyake kwenye zulia la ofisi ya serikali au wenzangu mnapenda ofisi za kutoa huduma za serikali kuwa chafu kila mara?
kuhusu gari la serikali kubeba mkaa mimi binafsi naona si tatatizo kwa kwa kuwa aliyebeba huo mkaa ni mwananchi wa tanzania na anakatwa kodi japo ni mtumishi wa serikali.hivyo basi kwa kuwa ugumu wa maisha ni kwa kila mtanzania mkaa kijijini ni bei rahisi na mjini ni marambili ya bei ya kijijini hivi mtu kubeba mkaa kwaajili ya familia yake na majirani zake ni kosa au kwa kuwa gari lililobeba nila jamuhuri na yeye ni mtumiaji wa gari hilo mtu anakula kazini kwake ahsanteni
OK, it may be very inconvenient to bend down and take off your shoes when you enter the office, but are you sure, huna matope au dog poo kwenye nyayo za viatu? Shoes are dirty,period'
ReplyDeleteHuyo ni msafi analinda mazingira yake, fikiria umetokea Tandale kwa Mtogole au Buguruni kwa mnyamani unakwenda Kariakoo au Posta, huko njiani utakanyaga mifereji mingapi ya maji yanayotoka chooni?, utakanyanga makohozi na mate yenye TB na yasiyo na TB!!, utakanyaga mikojo ya wanaokojoa hovyo barabarani bila kusahau vinyesi vya mbwa, paka na mbuzi wanaotembea hovyo barabarani. Analinda mazingira yake, shangaa kama ungeambiwa vua nguo zako mlangoni.
ReplyDeleteHilo la kuvua viatu kuingia ofisini nakubaliana na wewe ni issue lakini hilo la kubeba mkaa kwenye gari la serikali tukijadili hapa na kupinga tutakuwa wanafiki tu. Wewe mtoa mada ukisafiri na gari la serikali toka Iringa kwenda Dar ukakuta mkaa na mchele njiani na gari lina nafasi utaacha kubeba? Kupoteza muda kujadili hili ni unafiki tu.
ReplyDeleteEbu watanzania acheni ulimbukeni na ushamba!! Kuvua viatu ni taratibu kama nyingine!! Inawezekana humo ndani ya ofisi kuna zulia na kama mnavyojua kufanya usafi wake ni ngumu na ukizingatia mazingira ya kusini!! Pia kuna uwezekano wa kukwepa mafua yanayoweze kutokea kwa sababu ya vumbi!! Mbona majumbani mwenu mnavua viatu?? hilo sio swala la kujadili na wengine kuleta udini humu!! hivi hakuna maswala ya muhimu ya kujadili mnapiga picha za kuvua viatu ofisini?? Mmesahau katiba ambayo pengine inaweza kuwa inasababisha yote haya!!! ndio maana mnakimbilia Loliondo kama watu wa Karne ya 10!! Tuamke tuachane na fikira mgando!! kwa swala la gari la serikali kubeba mkaa! hata wewe leo ukipelekwa huko uwe kiongozi unafikiri utakwenda kukagua miradi ya maendeleo na ukutane na mkaa usiubebe na unajua hapo wilayani unapokaa haupatikani na umeme ni wa mgao!! Na kama angepewa zawadi ingekuwaje au asingebeba zawadi hiyo!!?? Au Rais na Waziri mkuu wanapokwenda sehemu na kupewa zawadi zinasafirishwa vipi kupelekwa Dar!!?? Tena usikute hata mbuzi anapandishwa kwenye ndege ya serikali(Rais)!! Tatizo ingekuwa gari iliyobeba mkaa haistahili kubeba mzigo kama huo kwa mfano gari ambayo ni SUV isiyo pick up!!!
ReplyDeleteManeno mengine mnaongea hamjapata hizo nafasi!! kama angekua anafanyia biashara gari sawa hapo tungeweza kupiga kelele!!!
Mdau ughaibuni!!
Zile nyimbo za kwaya ofisini. Hivi na yale mapambo ya Krismasi tena kwa budget ya serikali ni nini? Msichokoze nyuki. Bora hiyo katiba ije maana hivi vitu lazima viondoke. Udini upo tena mzito upande mmoja. Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni. Wenzetu huku Marekani, wanaogopa kusalimiana Happy Christmas, wanasema Happy holidays, wanaogopa kuwa sued. Kwetu ah mambo kinyume nyume. Halafu usiibanie hii Michuzi, ukiona vitu vinavyohusiana na udini usivirushe humu kama hutaki malumbano.
ReplyDeleteHakuna swala la dini hapo acheni ujinga, kwani dini gani ni safi kuliko nyingine?
ReplyDeleteNi swala la usafi tu, vumbi ikiingia kwenye kapeti au kompyuta hela ya service au vacum cleaning nani atatoa na serikali yetu ndio hii
Kuhusu swala la mkaa wewe ulitaka anunue huko atokako halafu akodishe gari kupeleka nyumbani anapokwenda, is it economical?
Halafu nyie mnaotoka utumwani huko ulaya / India kwanini mnafikiri wanavyoishi Masters wenu huko ndio sawa? this is Africa, especially Tanzania tuna njia zetu za kuishi na kama mkirudi tuangalieni tu msijione nyie ndio mko sawa
Mngekuwa Japan sijui mngesema nini? hizi ndio tabia tunatakiwa wa Africa kuwa nazo Sio Ndula limekanyaga mitope uchafu unakanyagia ma ofisi ya watu tusiweke sababu za Udini hata kidogo Miaka ya Nyuma ofisi za kina Nyerere watu nasikia wlaikuwa wakiingia wamevua viatu. Mkurya halisi Mwita. Tabia zenu za zunguni pelekeni hukohuko USA na UK. Mr Mwita.
ReplyDeleteWANA BLOG! NISAIDIENI. HIVI KWELI KWELI WILAYA ZILIZOKO MKOANI KILIMANJARO WAWEZA KUONA KITU KAMA HIKI CHA KUTOA VIATU?????
ReplyDeleteHIVI TUKO KARNE YA NGAPI? JAMANI TUNAJIDHALILISHA SISI WENYEWE NA HATA TUKICHEKWA HATUNA BUDI KUKAA KIMYA
ASANTE HILDEBRAND KWA KUTUAMSHA. NIMESONONEKA SANA NA KITENDO HIKI KINATUDHALILISHA SISI WATU WA KUSINI
SWALI NI KUWA KWELI UNAHITAJI MTU KUTOKA LONDON, DAR ES SALAAM KUONA HILI TANGAZO SISI WATU WA KUSINI KWA NINI JAMANI HATUJIJALI?
TUTAKAA HIVI MPAKA LINI?
NAUMIA HADI NINALIA
WATOTO WETU WATATUELEWAJE?
do, ama kweli in this world there is a "BIG BROTHER" nilikuwa siamini lakini sasa naelewa. hii gari nilikutana nayo sehemu moja inaitwa KIBITI ikiwa imepakiwa karibu na petrol station, kama sikosei!
ReplyDeletekumbe when you think uko mwenyewe kuna mtu anakuona
"Big brother concept"
Gari kubeba mkaa wala siyo tatizo. Mkaa siyo bidhaa haramu nchini na gari limetolewa kumsaidia mfanyakazi wa cheo fulani. Mkaa ni nishati anayoitegemea sasa abebe kwa kichwa?
ReplyDeleteKuvua viatu ni AIBU na lazima mwenye hiyo ofisi ana matatizo ya kielimu. Hajafikia kiwango cha elimu kinachotakiwa maana angejua kuwa "public office" haitakiwi kuwa na masharti kama haya. Shame!! Nitaenda huko kusini nikiambiwa nivue viatu I file a court case nilipwe fidia kwa kuwa psychologically mistreated kwenye ofisi ya umma. OR is this a mosque???
Hata Japan kuna utaratibu huu wa kuvua viatu, ni suali la usafi. Tembeeni muone.
ReplyDeleteLa kubeba mkaa ni dereva na maafisa au wafanyakazi wenzao wamewatuma na wamebeba kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kupikia.
ReplyDeleteHili la kuvua viatu ndo la kijinga. Hizo Computer na Air Conditioner bado tuna ile mambo ya zamani kwamba vumbi inaviharibu, kwa hiyo solution ni kuvua viatu.haaaaaaaaaaaaaaa, Lindi tambarare!!!!
wewe anon wa 11.41.00am, naona una mfumo dume, but wanawake tunashukuru kwa kukubali kwako kuwa wanaume ni wachafu.
ReplyDeleteUkivua Viatu ndio Mwanzo wa kuambukizana FUNZA na FANGAS, nawasihi WASIVUE na gari ya serikali kubebea mkaa mimi naona sawa tu angalau kuna mama karahisishiwa kazi moja ...sasa atabakia kwenda kuchota MAJI.
ReplyDeleteKusema ukweli nilifika huko kusini kuna sehemu kuna tope sana sehemu nyingine. pia sidhani kama wakti wa juwa kali kuna haja ya kuvuwa viatu, kwa kuwa wote hatujui kwa nini watu wa kusini wanfanya hivyo, ninaamini siyo dini.Nimetembea nchi nyingi sana lakini nilivuwa viatu nilipoingia offisi moja mkowa wa kilimanjaro, hiyo offisi ilikuwa na kapeti safi sana na viatu vyangu vilikuwa vimejaa tope, nilivuwa kwa kujuwa jinsi gani ilivyo kazi kusafisha kapeti haswa kwa sehemu ambazo hakuna vifaa maalumu vya haraka haraka. Sasa hizo offisi za kusini labda zina capeti au zina taile, sasa ukija mzungu hutaambiwa uvuwe viatu kwa sababu wewe ni muwekezaji ukienda mswahili, utaptata jibu wewe mwenyewe. Nadhani ni vyema kuheshimu utaratibu wa watu, kila mtu anutaratibu wake kwenye offisi zao. Kuna wengine hwataki secretaty kwani ni gasia tu kuna wengine ukienda offisini kwao huwezi kuwaona ni utamuona secretaty tu. Hiao ni taratibu za watu na inabid tuzikubali. Ukienda sehemu hangaikia kilichokupeleka huko na kitekeleze lakini mambo ya kuchokonowa wanaishi namnagani is not your business. Watoto wa kudini wanhitjai mwanga zaidi na huduma bora za kimaisha.
ReplyDeletekuvua viatu kunaweza kusababisha transmission of hidden infections ni bora wavae tu(more hygienic).
ReplyDeleteKuhusu vumbi ni bora waweke sakafu kwani ni rahisi kupiga deki kama tufanyavyo majumbani. Mhudumu anatakiwa kubuni mbinu zaidi za kutunza mazingira ya ofisi katika hali ya usafi. lakini pia hiyo karatasi inaonekana kama ni tangazo ambalo si la kudumu hivyo lets hope kwamba siku hiyo mdau aliyopita walikuwa wanaoperesheni usafi.
God Bless My Dear Country
JAMANI EEE MBONA MNAPIGA KELELE HIVI? SIKU HIZI HALI YA SIASA IMECHAFUKA SANA. NA HAPA OFISINI NI MTU ANAJIOGOPEA ASIJE AKAPIGWA NA KIATU KAMA ALIVYOPIGWA GEORGE BUSH KULE IRAQ.
ReplyDeleteHALAFU NAWAOMBENI MSIINGILIE SANA KUHUSU UTUMIAJI WA GARI MAANA HATA NYINYI MKIPATA HIYO NAFASI HAMUIACHI JAMANI.KAMA MTU KATOKA NJE YA MJI KIDOGO NA KAKUTANA NA MUUZA MKAA AU BIDHAA YEYOTE ILE LAZIMA ATAJICHUKULIA AU ATAMCHUKULIA MZEE WAKE JAMANI EEEEEEEE.PUNGUZENI JAZBA PAMOJA NA MAMBO YA DINI MUYAACHE.
Hilo la kuvua viatu hatutapata jibu sahihi labda mdau ungejaribu kutupa jina la bosi hata kwa kuforge hapo tungapata jibu sahihi.
ReplyDeleteLakini kuna sehemu wanavua viatu na ni sehemu za umma, nilishaenda Kariakoo mitaa wanayouza madila ya kina mama kule maduka mengi unavua viatu, njie nendeni mtajionea, na sisi ambao dini zetu hazituambii kutoa viatu huwa hatuingii hayo maduka maana ni kama usumbufu kuanza kutoa viatu kisa unataka kanga au dila na wakati duka la jirani hutoi viatu na bei ni ileile.
Swala la kutunza vifaa halina mashiko kwa sababu kama wanataka kuinusuru jamii na udini/matabaka hawapaswi kujali hela ya vifaa, maana ni kodi zetu, ningekuwa kiongozi ningewashauri waache kuwavulisha watu viatu na kama vifaa vitaharibika au kuchafuka vinunuliwe upya au kusafishwa mara kwa mara.
Hilo la mkaa hata mimi ningebeba, tena mengi haswaaaaaaaaa!!!!!
Nilisafiri kwa ndege kutoka Ntwara kwenda DSM 1991. Ndege tulipofika DSM zaidi ya nusu wa abiria waliokuwa kwenye ndege walitoka miguu tupu (bare feet). Wengi waliacha viatu kwenye ndege, sasa sijui ni mazoea au walisahau!!
ReplyDeleteila siaelewa we ni nani uende kukagua maendeleo.halafu kuvua viatu na kuingi ofisini mbona hata majumbani tunafanya. bana viatu hukanyaga mavi ya paka,sasa ni vipi uingie offisi zetu zina heshima bana
ReplyDelete