Asalam alykum ankal michuzi,
Napenda kutoa dukuduku kifuani mwangu.
Hivi majuzi nilikwenda kwa watani wetu wa jadi kwa ajili ya sikukuu ya pasaka.wakati wa kurudi pale mpaka wa tanzania ,nilikuwa kwenye foleni nikisubiria wakati wangu ufike ili nigongewe pasi yangu. K
wa wale msiyo na taarifa,siku hizi mpaka wa tz mbali na kupigwa picha (kwa wenye pasi ya kitabu) wameanzisha kuchukuliwa finger prints.
Nilipofikia kwa afisa uhamiaji,mara akaibuka mkaka mmoja (sijui alikuwa ni conda wa gari la abiria fulani au ni agenti) aliyekuwa na pasi za kitabu kama 6 hivi akaingia kwenye kizimba cha afisa uhamiaji huyu ambaye nilikuwa namsubiria anigongee muhuri pasi yangu pamoja na kuchukuliwa finger prints.
Basi yule afisa uhamiaji alizigonga pasi zile 6 kwa haraka sana (mind you wenye pasi hawakuwepo hapo) na akamkabidhi yule kaka huku nikitafakari kulikoni?then akaichukuwa pasi yangu na kuigonga muhuri akaniamuru niweke vidole vya mkono wa kulia kwenye kile kimachini cha finger prints. Sikuwahi kumalizia mkono wa kushoto wala kupigwa picha...akaniamuru niende zangu na pasi yangu.(nadhani alitahayari sana kwa alichokifanya kwani ningemuuliza maswali mengi sana.)
kweli tutafika kwa staili hii?so ina maana hawa maafisa wetu wa uhamiaji wamechoka na kazi, coz lazima wanapewa 'chai' kugonga mihuri na hawafuatilii kanuni zilizowekwa za nchi. Swali ni jee, kuna wangapi ambao wanagongewa tu pasi zao bila hata kuonekana na kufatilia sheria zilizowekwa???
naomba mkuu wa uhamiaji aliangilie swala hili kwa kina.
nb.siku yenyewe ilikuwa Muungano Day!
mdau mwenye hasira Dar


BORA WEWE KAKA!! MIMI NILITISHIWA KUPOKONYWA PASI YANGU NA MKUU WA HAPO MPAKANI,KISA NILIULIZA ITAKUWAJE WAO WATU WA UHAMIAJI NDIO WANAKAGUA KITABU CHA CHANJO KWANI WAO SIO MAAFISA WA AFYA LOO!!! MOTO ULIONISHUKIA HAPO WE ACHA TU!!!!! NAMIMI NIKAWA MKALI NDIO SALAMA YANGU. NADHANI HAPO KUNA MRADI WA WATU KUHUSIANA NA VITABU HIZO KWANI HAPO HAPO UTALAZIMISHWA KUKINUNUA KWA ELFU ISHIRINI.
ReplyDeleteaaaaah hii nchi imekwiesha siku nyingi sana, hakuna kufuata taratibu kweye mambo yanayohusu usalama. Mimi mwenyewe wakati wa kujiandikisha kupiga kura nilijiaandaa na passport yangu wala sikuulizwa kithibitisho chochote, sasa hapo unategemea nini? Ndio maana nasema swala la mgombea binafsi kwa nafasi ya urais tusijaribu kuliruhusu hata mara moja, maana nchi inaweza kuchukuliwa hivi hivi....mifumo yetu ya usalama imekufa kabisa.....soooooooooo sad.
ReplyDeletepengine hao wenye pasi ni majambazi au watu wabaya wanakwepa kitu maana kama walishachuliwa fingerprint huko nya kwa uhalifu basi wakienda tu watalambwa.majina sio issue yanaweza kufanana ila vidole hapana,nahisi hao kuna kitu wanakiruka.
ReplyDeleteHawa watani wa jadi ni nchi gani? Mnapoandika habari msisahau kwamba tupo watu wengine tunaishi ughaibuni miaka mingi na misamiati ya kileo hatuijui.Please tuwekeeni wazi ili nasi tuelewe nini kinachoendelea
ReplyDeleteUnategemea nini unapomlipa mtu mshahara laki tatu na kumkabidhi kazi nyeti. Mwache atafute ela ya school fees ya watoto. Kwani yeye hataki watoto wake wasome english media? Tatua kiini cha tatizo siyo kukamata vidagaa.
ReplyDeleteTunashukuru sana kwa kukerwa na tabia a ya hao jamaa kugonga pasi bila kuona wenyewe.Lakini utaratibu wa wa kuchukua alama za vidole na kupiga picha wananchi wa afrika mashariki wa nini?kawaida utaratibu huu unatumika kwa nchi za ulaya kwa madai ya kuwazuia wahamiaji haramu kutoka nchi masikini hasa za bara laAfrika.Nadhani utaratibu huu ungetumika kwa watu kutoka nje ya jumuuia ya Afrika mashariki hasa watu kutoka bara la ulaya na asia ili na wao waonje joto ya jiwe.Kutakua hakuna umuhimu wa kuwa na jumuia ya afrika mashariki iwapo wananchi husika wanawekewa vikwazo vya kutembea wanavyotaka.Nadhani muhuli wa kuingia na kutoka unatosha.
ReplyDeleteMdau wa glob toka ugaibuni
watani wa jadi nadhani ni wakenya
ReplyDeleteTatizo kubwa ni elimu ya ubabaisha ambayo haimjengi mwanafunzi (ambaye in future ndio mfanyakazi) kwa maadili mema. Pili ni ubinafsi tuliojawa wa Tz.Mara ngapi mahala pako pa kazi unamsaidia mtu kwa sababu tuu ya pesa au kujuana? Je hio ni sahihi? Ni vizuri sana tukianza kujirekebisha kabla hatujaanza kuwanyooshea wengine vidole. Kama wewe unaweza kufoji risiti, kushawishi au kutunga safari ambayo haina tija kwa ajili ya kutengeneza pesa ambayo si halali, then huyu afisa uhamiaji ana kosa gani? Maana wote mnatengeneza pesa kwa njia haramu, tofauti ni mechanism tuu!
ReplyDeleteNamjibu aliyeuliza watani zetu ni akina nani? Hao ni Wakenya. Ni watani kwa sababu wamekuwa wakipinga kila tunachotaka kufanya tanzania na kujiita eti wao wanajua zaidi kuliko sie. Hapo ndipo utani umeanzia manake nimeishi nao huko kwao na hata huko ulaya sijaona cha zaidi walicho nacho kutuzidi. Wanachotuzidi nacho sanasana kwa uddhulumishi unnesessarily.
ReplyDeleteNaomba aliyetaka kujua kwa nini pasi inagongwa muhuri wakati sisi ni wamoja, afute kauli yake. sisi si wamoja. Tuna tamaduni tofauti na hulka tofauti. Waliosema Tanzania kukataa hiyo freelance walishaona hilo heshimuni walichoamua. Huenda tukawa wamoja baada ya kuchanganyikana kidogokidogo kupitia soko la pamoja lakini si haraka kama mnavyodhani. Italeta matatizo mengi. Hata umoja wa ulaya ulianza kuongelewa mda mrefu sana lakini walifanikiwa baadae sana. Na bado ukiongea na wajerumani bado wanaulalamika kuwa umoja huo.
ReplyDeleteHuu utaratibu wa kuchukua vidole umeanza lini? Mimi nimesafiri kutoka Dar Int. mbona sijachukuliwa vidole na form za kujaza sasa pia zimeondolewa kwa waTz. Vidole wanachukua kwa wageni. Labda wewe una pasi ya mama au mnyamwezi.
ReplyDeleteMSAADA TUTANI NDUGU ZANGU ingawa nimetuma kama comment
ReplyDeleteMimi ni kijana wakati na miaka 17 niliishi uingereza tatizo linalonisumbua ni uchawi baada ya kukaa uingereza kwa miaka kadhaa sikufanikiwa kuendelea kukaa nikarudi nyumbani kutokana na maisha ya uingereza nikahisi na ugonjwa wa depression nilivyorudi nyumbani niliendelea kuhisi kuwa na depression(kufikiri sana na low in confidence)mambo yakaanza nikapata kama ukichaa nikapelekwa muhimbili halafu ikatulia baada ya mda inaanza tena (kama kuna doctor atoe kama hizi ni outcome za depression)ilipotulia safari hii nikapata chance ya kurudi ulaya nikasema sitoacha kutumia vidonge usije ugonjwa ukanirudia CHA kushangaza mwaka mmoja na nusu baada ya kufika huku ugonjwa ukarudi tena lakini safari hii nikagundua ni uchawi kwasababu sauti za watu nikikaa nikama naongea na watu mara naota naingiliwa kinyume na maumbile,mara naota naingizwa vidole sehemu zangu za siri nilitaka kunywa sumu sauti zinasema samahani tunakuheshimu wazungu wamenipa vidonge mtu anayejua vidonge vya vichaa vinavyonenepesha wapi sauti ziko pale pale sauti mara zinasema tuna wivu ndugu zangu nimewaambia haya wananiambia natumia madawa ya kulevya mi nashangaa mi ndo nnae umwa najua niko vipi kwanini waning`ang`anize natumia madawa ya kulevya mtu anayenifanyia hivi mi namjua nimekuja kwenu labda wadau wanaweza kunisaidia niondokane na dhahama hii nimeenda kwa pastor hawa ma pastor wa kinigeria wanayao tu ndugu zangu naomba MSAADA JAMANI KAMA SIO TUTANI KWENYE KONA
mdau
asante
lakini ili kupiga hatua ningeshauri mdau uliport kwenye vyombo husika otherwise hakuna kitakachobadilika. suala la mshahara kuwa ni kidogo limekuwa kisingizio cha siku nyingi lakini isiwe njia ya mtu kutenda maovu. wafanyakazi wengi wamekuwa na tamaa sana. Mf. Mbona TRA wanalipwa vizuri lakini ni wara rushwa wakubwa? hivyo hivyo na sehemu nyingine. wanaofanya vibaya walipotiwe!!!!! hiyo ndiyo kuonyesha hasira sio kulalamikia siasa
ReplyDeleteMdau wa hapa juu namba 12 pole sana,swala lako linasikitisha sana lakini dawa yake ni ndogo.kumbuka kwamba swala la uchawi limeandikwa hata kwenye bibilia.kama umekwenda kwenye maombi, lakini bado mimi kwa ushauri wangu tafuta waganga wa jadi watakusaidia.ulaya hapa kuna watanzania wachawi kuliko huko bongo.ugonjwa ulionao, umewapata wengi hapa ughaibuni, na wengine wamepoteza maisha yao.samahani mdau kama nitakuuthi lakini huo ndio ukweli wenyewe.wako mdau london.
ReplyDeletendugu unayeomba msaada tutani pole sana na mambo yaliyokusibu..inaonyesha unasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa schizophrenia na si uchawi kama unavyodhani wewe. hayo uliyoyasema ndio kabisa symptoms za ugonjwa huo. tafadhali fuata link hii itakupa maelezo zaidi ya ugonjwa huo na tiba zinazotumika http://www.nhs.uk/Conditions/Schizophrenia/Pages/Introduction.aspx na usiache kutumia madawa unayopewa hata siku moja. hujarogwa na mtu yeyote.
ReplyDeleteMdau hapo juu uliyeomba ushauri wa maradhi. Watu wengi waliokwenda Ughaibuni wamepata matatizo ya depression. Dalili zote unasosema ni za depression. Watu wa Ughaibuni huo mara nyingi hawana watu wa kuzungumza na kupata nafasi ya kubadilishana mawazo na kucheka. Wengi zaidi ni wale ambao hawana makaratasi ya kuishi huko. Sasa inakuwa hawawezi kuja Bongo kutembea au kuchukua wake zao. Wanapofikwa na matatizo yoyote yake mfano nyumbani Bongo kama kuna mzazi au mtoto wake mgonjwa huwa hana wa kumuhadithia matatizo yake na kupata ushauri nini cha kufanya, pia hawezi kurudi nyumbani, maana visa tena ndio hivyo na yeye ameshazidisha muda. sasa huwa anasumbuka kimya kimya. Watu wengi wakutoka TZ ni kuwa wanapotokea matatizo ya mmoja wao huwa hakuna msaada zaidi ya kuchekana. Kwa mfano wenye makaratasi wanawacheka waliokuwa hawana. Kila mtu anaficha ukweli wake. Matokeo yake ni kuwa mtu anachofanya ni kazi na kujichimbia ndani. Sasa kwa mwaka mmoja au miwili mpaka mitano anakuwa OK. Lakini kila muda ukizidi anaanza sasa akipata tatizo dogo tu anakuwa hawezi kula, kuanza kusema pekee yake, na kuanza kuota kutaka kujiuwa. Hii ni dalili za depression. Na hii sio tu kwa watanzania bali hata wazungu wenyewe. Na hawa wazungu wao huwa hatari sana wanapopata depression. Wanaweza kuuwa mtu mara moja au wenyewe kujiuwa. Sasa mdau, inabidi uende kwa GP akupe dawa zinaitwa Prozac. Hivi dawa ni nzuri sana, na dozi yake ni miezi sita. Pia jaribu kujichanganya na watu sana, akija Msanii kutoka bongo jaribu kwenda. Punguza kuwa pekee yako, lazima ujichanganye na watu. Hata kama wazungu, nenda pub ukazungumze na watu japo habari za mpira. Nimeona watu wengi wanarudi Afrika kwa depression. Pia achana na mawazo ya Bongo.
ReplyDeleteWewe hujarogwa chochote. Wadau wameshasema una depression. Fuata ushauri wa wadau. Nami nakuongezea huu. Tafuta mzungu wa kula naye hata mara moja moja atakupunguzia makali ya maisha.
ReplyDeleteHata muandika habari unahitaji help. kama unataka kusaidia taifa si unakamera. Ungepiga picha ya yule mtualiyekuapo hapo na ukija kuandika unaandika na jina kama uliliona ndio hivyo . Kuficha ficha haitasaidia.
ReplyDeleteHuku uukifanya uzembe wanakuendea na kukuweka kwa TV help me howard...Hamna cha kusema sijui basi naniniii ....kafanya hivi...Toeni majina yao huadharani iliwatu wajue siku hizi camera ziko kila mahali. Si mna simu zenye camera kazi yake ni ya nini?
Mdau mwenye shida wala hujalogwa ...hiyo ni maniac depression. Inapata watu wenye umri kuanzia 16 to early 20. na the more unatibu mapema the more unapona kabisa. Je kuna kitu unakiogopa hapo unapoishi? Kaa na watu wenye positive thinkings, halafu fanya mazoezi sana, kula vitamins kuna some madini yanamiss.Make sure unapata usingizi. Dawa hizo ni nzuri lakini utaishia kuwa mtu wa kula dawa kila siku, maisha yako yote? Mwone Doctor wako akuondoe kwenye dawa polepole manake hizo dawa ukiacha ghafla basi utazidiwa zaidi. Hamna mchawi wowote na kama una imani yako kaa nayo hiyo hiyo usiende kwenye kanisa lingine kabisa. Mwombe Mungu wako huyo huyo hao wanaosukuma na kukwambia una mapepo don't listen ndio watakuzidishia. Sali na fuata hayo hapo utapona. Mimi niliugua lakini waliwahi kwa hiyo nilipona ila Mimi nilikua siongei mwenyewe nilikua na wasiwasi tu na nikiwa kwenye sehemu ya watu wengi naona kila mtu kama ananiangalia mimi tu. Mara naona kama moyo unaenda mbio kumbe hamna chochote. Yaani nilikua napata panic attacks kishenzi. Nikilala mwenyewe naona kama sitaamka asubuhi hivyo nakaa macho usiku mzima. Nikilala na mtu niko safi....
ReplyDeleteUnaujua tanzania hatuzungumzii haya mambo kwa vile watu wanaona ni aibu kwa familia kuonekana kuwa kuna mental disease lakini meantal deseasess zipo zaina nyingi tu sio depression tu. Na depression inarithi huyo anayesema sijui watu hawana wa kuongea naye hiyo ni solution lakini kama huna genes za depression unaweza kukaa mwenyew na wala usipate shida na kama una genes za hiyo basi kitu kidogo kiki trigger. Mim i masomo niliyokua nasoma nilikua sipendi lakini wazazi walikua wanataka nisome. Nilikua siwezi kudeal na wagonjwa kabisa manake kila mtu anayeumwa najiuliza kwanini yeye . Etc etc ..Nilivyotibiwa na kubadilisha masomo nimepona kabisa...
Ndio hivyo ondoa mawazo yasiyo na maana