
Timu ya Mashabiki wa Arsenal wakishangilia ubingwa wao walioupata kwa ushindi wa matuta katika Bonanza la Castre Beach football lililomalizika jana jioni katika fukwe ya Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.

Nahodha wa Timu ya Mashabiki wa Arsenal akipokea Kombe kutoka kwa Meneja wa Bia ya Castre Lager,Kabula Nshimo mara baada ya kutawazwa ubingwa huo wa Castre Beach Football Bonanza.

Washindi wa pili katika Castre Beach Football Bonanza,walikuwa ni Mashabiki wa Liverpool (Bwawa la Maini) ambao walikabidhiwa vilaji vya Castre lager pamoja na mpira ambao utatumika katika michezo mbali mbali watakayokuwa wakicheza.

Mashabiki wa Chelsea walishika nafasi ya tatu.

Timu ya Mashabiki wa Man City ilijinyakulia nafasi ya nne.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...