Pichani ni kundi liitwalo Mwanza House of Talent likiwa na washabiki wake jioni ya leo mara baada kuibuka na kutajwa ndio washindi wa shindano la msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta dansi 2011,lililofanyika kwenye kiota cha maraha cha Lips Club ndani ya Isamilo,jijini Mwanza na kuhudhuriwa na watu kibao.Aidha kufuatia ushindi wa kundi hilo,limefanikiwa kujiunga na makundi mengine kadhaa kutoka mikoa mbalimbali kama vile Tanga,Arusha,Mbeya pamoja na Zanzibar,watakutana siku ya kilele cha msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta jijini Dar hapo baadaye.
Mmoja wa majaji wa mchakato wa kumpata mshindi wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta dansi 2011,Hamis Mandi a.k.a Bdozen ambaye pia ni mtangazaji wa redio ya Clouds FM akitoa pointi kwa moja ya kundi lililoshiriki jioni ya leo ndani ya Lips Club,Isamilo jijini Mwanza,anaefuta ni Mratibu wa shindano hilo Fatma Hassan a.k.a Dj Fetty,Mdau wa Dansi la Fiesta,Jaji Mr Simple pamoja na jaji mwingine aitwaye Issakwisa Thomson ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Clouds TV kupitia kipindi cha Step Up Player.
Pichani ni kundi liitwalo Nsuma house of talent wakisubiri maoni kutoka kwa majaji mara baada ya kumaliza kubanjuka dansi la fiesta.
Wadau mbalimbali waliojitokeza kushuhudia msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta dansi 2011, jioni ya leo kwenye ukumbi wa Lips Club,ulioko Ismilo jijini Mwanza.
Kundi la NBN likionyesha umahiri wa kucheza kwenye shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta dansi 2011,ndani ya ukumbi wa Lips Club,Isamilo jijini Mwanza,jioni ya leo.
Kundi la Mwanza house of talent likibanjuka jukwaani kwa satili ya kipekee kabisa.
Moja ya kundi lililoshoriki kwenye mchakato wa kulisaka kundi bora ndani ya msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta dansi wakionyesha umahiri wao wa kucheza mbele ya umati wa watu (hawapo pichani) ndani ya ukumbi wa Lips Club,Isamilo jijini Mwanza wikiendi ilopita. Picha na Michuzi Jr.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...