Ujumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tanzania Bara Mhe. Pius Msekwa, (kulia), Naibu Katibu Mkuu Taifa Capt. John Chiligati (katikati) na Katibu Mwenezi wa Chama Bw. Nape Nauye wakiwa katika ofisi ya Spika wa Bunge leo. Huu ni mwendelezo wa mjadala wa kupata tume ya kuratibu mchakato wa katiba mpya.
Mwenyekiti wa DP Mchungaji Christopher Mtikila akitoa msimamo cha chama chake kwenye mchakato wa kuunda tume ya kukusanya maoni. DP inasisitiza kwamba Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezekani ila ya Tanganyika tu.
Viongozi wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala wakifuatilia mjadala kwa makini. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Pindi Chana, Makamu Mwenyekiti Mhe. Angela Kairuki na Mjumbe wa Kamati Mhe. Musa Ally Kombo, Mb.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na kumkaribisha ofisini Mwenyekiti wa TLP Mhe. Auugustine L. Mrema (Mb) alipowasili ofisini hapo kuhudhuria mjadala wa maboresho ya muswada wa Tume ya kuratibu mchakato wa Katiba mpya leo.
Ujumbe uliondamana na Mhe. Mrema ukimsikiliza Mhe. Spika. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine L. Mrema, Katibu wa Chama, Mkurugenzi wa Utwala…. Na Katibu wa Wanawake TLP Taifa Bi Nancy Mrikaria.Picha na Prosper Minja-Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2011

    Asante sana Mtikila kuonesha masimamo wako. Tanganyika irudi. Tunataka Serikali 3.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...