Wafanyakazi wa Symbion Power wakiwa katika mazoezi wakati wa mafunzo ya utaalamu wa umeme kwenye chuo cha kampuni hiyo ya kufua umeme toka Marekani Kilichopo mkoani Morogoro kwa kushirikiana na kampuni ya Pike. Kabla hata ya  kununua mtambo wa Dowans kampuni hiyo ilikuwa inatoa mafunzo kwa  wafanyakazi wake, na imepeleka watatu huko Idaho, Marekani, kupata mafunzo ya juu ili kuja kuwafundisha wenzao hapa nyumbani
 Tizi la kuning'inia kwenye nguzo za umeme
 Mafunzo ya kusimika nguzo za umeme
 Mafunzo ya kuweka nyenzo za umeme kwenye nguzo
 Mtaalamu wa kampuni hiyo akiwapa maelezo kundi la wanahabari lililozuru chuo hicho mjini Morogoro Jumatatu
 Dada Agnes ni mwanamama wa kwanza wa kampuni hiyo kupata mafunzo ya Symbion/Pike 
Dada Agnes katika mafunzo


SAMBAZA UMEME SI UKIMWI


Transmit Electricity, Not AIDS

Kijarida cha ‘SUSU’ - SYMBION POWER 
 

Corporate Council on Africa - CCA - Baraza la ushirikiano wa amshirika ya kibiashara Africa.

·         Corporate Council on Africa (CCA) lililoanzishwa mwaka 1993, liko mstari wa mbele katika kuimarisha na kuwezesha uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na bara la Africa. CCA hufanya kazi zake kwa ukaribu sana na serikali, mashirika ya kimataifa katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kuinua taswira ya Afrika katika jumuiya za kibiashara Marekani.
·         Wanachama wa CCA wanaamini kwamba nafasi ya Afrika katika kufanikiwa siku za usoni hutegemea uwezo wa wajasiria mali na wafanyabiashara kujenga na kuhifadhi utajiri wao kupitia biashara Binafsi. Mashirika ya wamarekani na watu binafsi wanaweza kuchangia kwa ufanisi kwa kujenga ushirikiano kuwafikia wafanya biashara binafsi wa Africa katika maeneo ambayo wamarekani wana uzoefu mkubwa: yaani, biashara binafsi, kuwekeza mitaji na kubadilishana teknolojia na usimamizi.
·         Afisa mtendaji mkuu wa Symbion Power, Paul Hinks ni mojawapo wa wakurugenzi wa bodi ya CCA.
Mpango wa SUSU

·         Shirika la Symbion Power Limeshirikiana na mpango wa Afya wa kupunguza hatari dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI Tanzania la Baraza la ushirikiano wa kibiashara Africa la Marekani liitwalo The Corporate Council on Africa (CCA) katika maeneo ya mradi wa Umeme Tanzania.

·         Shirika la Symbion na CCA lilianzisha mpango wa “SAMBAZA UMEME SI UKIMWI” yaani SUSU kwa kifupi, mbinu bunifu ambayo ni rahisi kwa ajili ya kuratibu na kuendeleza mpango wa VVU/UKIMWI pahala pa kazi na kuzuia maambukizi katika jamii mpango ambao utakuwa mfano wa kuigwa na mashirika mengine nchini katika Nyanja ya Ujenzi na miradi mingine inayolenga kuboresha miundombinu nchini Tanzania na pia kwa ajilia ya taswira ya Shirika kwa siku za usoni katika Afrika.

·         Japokuwa mpango huu sio kigezo cha zabuni, ni sehemu mahsusi inayoonyesha kujitoa kwetu katika kujenga uwezo na kutoa elimu na mafunzo. Symbion inabeba gharama zote zinazoambatana na juhudi hizi.

·         SUSU itatoa mafunzo makini na mbinu muafaka dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI yanayolenga kupunguza kasi ya maambukizi yakilenga jinsia, mienendo na tabia hatarishi kwa maambukizi ya VVU/UKIMWI na kujenga ufahamu wa kuimarisha rasilimali watu kwa ajili ya kuwa na jamii ya watu wenye afya bora kote Tanzania kama Mkakati dhidi ya VVU/UKIMWI maana TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA

·         Kutoa mafunzo na kujenga uwezo wa kuzuia maambukizi ya VVU/UKIMWI ndicho kiini cha mkakati mzima wa SUSU; hasa kupitia waelimishaji rika wanaoishi katika jamii ambamo Symbion inajenga njia za kusambaza Umeme na pia ambapo Shirika litaanzisha waelimisha rika kati ya Wafanyakazi wake.  

·         Hadi sasa waratibu wa mradi wa SUSU wameshafanya mafunzo ya awali kwa kuelimisha wafanyakazi wa Symbion na pia katika jamii zinazo zunguka mradi wa njia za Umeme katika mpango wa REA (yaani Umeme vijijini). Hii ni pamoja na kutoa mafunzo kwa waelimisha rika kwa katika jamii, usambazaji wa Kondomu na vipeperushi na majarida na pia kuandaa sera ya VVU/UKIMWI phalli pa kazi kwa ajili ya Kampuni. Hadi sasa elimu dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI imefikia walengwa zaidi ya 180 ambao ni waajiriwa wa Symbion wakiwemo ma lines men, waendesha mitambo ya kunyanyua vitu vizito na Wafanyakazi kwa ujumla.



·         Kitovu cha mkakati wa kibiashara wa Symbion, ni uwekezaji mkubwa katika kuendeleza raslimali watu katika maeneo yake ya utendaji. Kama Kampuni yenye ujuzi katika nchi zinazoendelea, Symbion pia inatambua kwamba Afya bora na ukuaji wa uchumi ni mambo yanayokwenda sambamba, katika pahala pa kazi na katika jamii ambako Shirika litapeleka Umeme pia kimsingi kutakuwa na muingiliano kati ya jamii na wafanyakazi.

·         Sambamba na ahadi za Shirika katika kujenga uwezo na ujuzi kwa miradi yake ya Umeme, Symbion inaahidi kuwawezesha watanzania katika vita dhidi ya VVU/UKIMWI.

VVU/UKIMWI katika Tanzania

  • VVU/UKIMWI bado ni tatizo kubwa nchini Tanzania ambapo wastani wa maambukizi kitaifa ni kati ya asilimia 5 – 6.

  • Wafanyakazi wanaohama-hama ni miongoni mwa makundi hararishi kwa maambukizi (kuambukizwa ama kuambukiza) VVU/UKIMWI

Mpango wa UKIMWI pahala pa kazi umethibitishwa kuwa njia bora ya kukabiliana na hatari ya maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa Wafanyakazi.

  • Tathmini ya awali ya mpango wa SUSU kwa waajiriwa wapya kuhusu ufakamu, mwenendo na tabia dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI ilionyesha kwamba wengi wao wanaamini kwamba wamo katika hatari kubwa kwa maambukizi ama kuambukiza VVU/UKIMWI.

Symbion Power


  • Symbion ni Shirika la uhandisi la kimataifa na ni wakandarasi wenye mbinu za kipekee katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya Umeme. Ikiwa na dhamira thabiti ya kuiwezesha jamii husika, Symbioni inaunganisha maarifa na ujuzi katika kufanikisha kazi zake katika mazingira yenye changamoto kubwa za ujenzi duniani.
    • Shirika la Symbion lilianzishwa mwaka 2005 kwa ajili ya kuunda, kununua na kujenga miundombinu ya Umeme iitwayo Turnkey ambayo kwa lugha ya kitaaluma hujumuisha njia za Umeme yaani Transmission lines, Substations, Switchyards na thermal power plant.

  • Symbion imejenga uwezo wa kipekee kuendeleza na kujenga ndani ya nchi. Mafunzo ya haraka na ya hali ya juu kwa waajiriwa wazawa yameendeshwa katika nchi kama Kurdistan Iraki, Afghanistani na sasa kwa kufunguliwa kwa kituo cha Symbion/Pike Power hapa Morogoro, Tanzania kutawezesha kuendeleza mafunzo ya ujuzi kwa mafundi wa njia za Umeme nchini, yaani ma-linesmen.

Mkakati wa Afya wa Corporate Council on Africa (CCA)

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003, mkakati huu unafanya kazi na kuwezesha sekta binafsi kukabiliana na mahitaji ya afya katika Africa ikiwa ni pamoja na tatizo la VVU/UKIMWI kupitia kuanzishwa kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali, misaada ya kiufundi kwa umoja wa kibiashara wa kitaifa na mashirika mengine.


Kwa mawasiliano:
Julie Foster
Symbion Power
Local: 076 733 3583 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2011

    Umemuona dada anavyukwea nguzo hiyo, kitaalamu kabisa. Wakati wakwezi wa minazi mpaka leo wanatumia pingu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2011

    sisi tunataka umeme , hatutaki BLAH BLAH BLAH , ramadhani hiyoo inakuja dalili zinaonyesha tutafuturu KIZAA!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2011

    Haya Tanesco fungasheni virago sasa mmeiba vya kutosha na tumewachoka. Masubiri Mzungu kaingia anatuwekea umeme hata kwenye vibanda na atkusanya kila sent na atahakikisha hata mkulima anpata umeme na pesa yote atapeleka kwao. Kama vile makampuni ya simu za mkononi. Hay kama unakijana mpeleke veta akasomee umeme, kazi za bure hizo zinakuja.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2011

    Halafu tunasema eti tulipata uhuru na tunasherehekea miaka 50 ya Uhuru na bado tunategemea watu watoke nje waje kutufundisha kufunga waya za umeme. tunashushukuru kua mmekubali kwamba we can't do it, pia finally tutapata umeme hata vijijini kusudi watu waliokimbilia mjini kuona taa sasa watarudi vijijini maanake Dar haiwezi kumudu population yote ya Tanzania.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2011

    sasa serikali mkiingiza siasa hapa mtaharibu mambo ni bora mkaa humoo wacheni wenye uchungu wa nchi watusaidie

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2011

    Ama mbwembwe! Kurushiana mipira ndio zoezi kwa ajili ya kurushiana vifaa vya kazi hapo baadaye? Tuyafanye mafupi jama, tunauhitaji mkubwa wa umeme wa uhakika, hay mengine kwetu tunaona mbwembwe tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...