Mkuu wa Chuo cha Michezo Malya, Bw. Allen Alex (aliyenyosha mikono) akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Sethi Kamuhanda (wa pili kushoto) alipotembelea chuo hicho kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hosteli ya Wanafunzi mwishoni mwa wiki iliyopita. Kulia ni Afisa Utumishi wa chuo hicho, Bw.Said Kitinga na wa kwanza kushoto ni Afisa Tawala na makazi chuoni hapo, Bw.Eliufoo Nyambi.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Sethi Kamuhanda akiwaonyesha jambo watumishi wa Chuo cha Michezo Malya alipotembelea chuo hicho mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hosteli ya Wanafunzi. Jengo linaloonekana pichani ni hosteli mpya ya kisasa ya wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Sethi Kamuhanda akizungumza na baadhi ya watumishi wa Chuo cha Michezo Malya alipotembelea chuo hicho mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hosteli mpya ya Wanafunzi. Katikati  ni Mkuu wa Chuo hicho Bw. Allen Alex, kulia ni Afisa Taaluma wa chuo hicho,  Bw. Joachim Maganga na nyuma kabisa ni Afisa Utawala chuoni hapo Bw. Said Kitinga. Picha zote na  mdau Concilia Niyibitanga, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...