Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba le amemkaribisha Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Ofisini kwake Dar es Salaam. Spika Makinda alifanya ziara hiyo kwa lengo la kupanua mjadala wa maudhui ya kuundwa tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya. Kulia kwa Mufti ni Katibu Mkuu wa Bakwata Alhaji Suleima Lolilya na kushoto kwa Spika ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Angela Kairuki. Aidha Spika Makinda pia alikutana na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania kwa mwaliko wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa lengo la kupokea maoni na ushauri kuhusu uundwaji wa chombo hicho cha kukusanya maoni. Pichani juu Mufti Mkuu akiendesha Dua maalum kabla ya mjadala kuanza.
Spika Makinda akiushikuru uongozi mzima wa BAKWATA na kuwaahidi kuwa maoni na ushauri wao vitazingatiwa
Viongozi wa BAKWATA wkifuatilia mjadala.
Spika Makinda (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania katika Hotel ya Courtyard, Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekit wa Baraza na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza.
| Wajumbe wa Baraza la siasa wakifuatilia mjadala Picha zote na mdau Prosper Minja wa Bunge |


Hapa pasisahaulike kuwa sheria ya ubaguzi lazima ianzishwe. Wale waliozoea kubagua watu katika ajira na huduma za serikali wakipate.
ReplyDeleteHatuwezi kuamini tuu viongozi kuwa watasimamia kutokomeza ubaguzi ili hali wao nao waweza kubagua. Iwepo sheria na mwongozo maalum. Hii ni nchi inafuata sheria. Au kufuata sheria kutahatarisha amani.