Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani akimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema mara baada ya waziri huyo kumalizia kufungua mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi la ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali unaofanyika katika Hoteli ya Giraffe Ocean View jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Sheria Hamis Msigala akimkabidhi risala ya wafanyakazi Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani huku Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju akishuhudia. Waziri Kombani alifunga leo mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi la ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali unaofanyika katika Hoteli ya Giraffe Ocean View jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kufunguliwa kwa mkutano wao mkuu. Watatu kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani akifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema na watano kutoka kulia ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju
(Picha na Anna Nkinda wa Maelezo).

Na Ismail Ngayonga,Dar-Es-Salaam

WAFANYAKAZI katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wametakiwa kuheshimu kanuni za fedha na kuweka sawa hesabu ili ketekeleza mikakati iliyopo kwa ufasaha na ukamilifu.

Kauli hiyo imetolewa jana (leo) na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani wakati alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali uliofanyika katika ukumbi wa Giraffe Jijini Dar-Es-Salaam.

Waziri Kombani alisema ni wazi kuwa rasilimali fedha haitoshi, hivyo ni wajibu kwa wafanyakazi kuwa na vipaumbele vya matumizi ya rasilimali za Ofisi ili kuhakikisha kuwa wanayafikia kwa wakati mafanikio waliyojipangia katika maeneo yao ya kazi.

Aliongeza kuwa Baraza la wafanyakazi linawajibu wa kutambua na kujadili vipaumbele vya Ofisi ili kuhakikisha kwamba fedha za kutosha zinatengwa kulingana na vipaumbele ili kuboresha huduma na kuondoa kero za wananchi wanaowatumikia.

‘Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi mnapaswa kutoa mwongozo na ushauri katika kutatua matatizo yanayojitokeza katika utekelezaji wa mambo yaliyo ndani ya uwezo wenu” alisema Waziri Kombani.

Kwa Mujibu wa Kombani alisema ni vema Menejimenti ishirikiane na Baraza la Wafanyakazi pamoja na Wafanyakazi kwa ujumla katika kujadili na kufikia maamuzi yanayohusu maslahi yao, utendaji wao wa kazi na maandalizi ya Bajeti.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) katika tawi la Ofisi ya Mwanasheri Mkuu wa Serikali, Bw. Hamisi Msigala alisema tatizo la miundombinu mipya ya utumishi halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu kwani kilio kilichopo ni ile hali ya kuonekana kuwa uzoefu kazini haupati thamani inayotakiwa.

Akitolea mfano alisema muundo mpya wa mtumishi wa kada ya ukarani amewekewa ukomo wa kiwango cha daraja E katika mshahara wake (TGS.E) na anapofikia hapo atabaki hata kwa miaka 20 mingine na vinginevyo abadili kazi.

Ni kweli utaalamu wa mtumishi aliyesoma hauwi sawa na asiyesoma. Lakini uzaofu na elimu kwa maoni yetu vyote ni muhimu katika sehemu za kazi na si elimu ya shuleni ikaonekana ndio mhimili na uzoefu si muhimu” alisema

Aidha Bw. Msigala alizitaja changamoto zilizopo katika Ofisi hiyo ni pamoja na tatizo la

muda mrefu la usafiri kwa watumishi, hivyo kuwafanya Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kutegemea usafiri kutoka Ofisi jirani ya Wizara ya Mambo na Ushirikiano wa Kimataifa, ambapo hata hivyo kupelekea kero mbalimbali ikiwemo kuchelewa kurudi majumbani kwao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...