Na Bujo Ambosisye

Naibu Waziri wa Maji Mhe,Mhandisi Gerson Lwenge ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa kazi ya upanuzi wa chanzo cha maji cha Ruvu Chini na kusisitiza kuwa jiji la Dar es Salaam linakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji hivyo kumtaka Mkandarasi aongeze kasi ya utekelezaji wa kazi hiyo.

Mhe.Naibu Waziri Lwenge ameyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea chanzo cha maji cha Ruvu chini wilayani Bagamoyo siku ya Jumatatu (tarehe 23 Mei, 2011)ikiwa na lengo la kujionea hatua iliyofikiwa katika kazi ya upanuzi wa chanzo hicho.

Akimkaribisha Naibu Waziri pamoja na watendaji wengine waliofuatana naye baada ya kuwasili katika ofisi za chanzo hicho cha maji Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi, Archad Mutalemwa baada ya kufungua mkutano wa ziara hiyo na utambulisho mfupi alimtaka Mkurugenzi wa Miradi ya Sekta ya Maji iliyochini ya MCC (Millennium Challenge Cooperation, Mhandisi. William Christian atoe taarifa fupi ya utekelezaji wa upanuzi wa chanzo hicho.

Katika maelezo yake Mhandisi Christian amemweleza Naibu Waziri kuwa upanuzi wa chanzo hicho unalenga kuongeneza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 190 hadi kufikia lita milioni 280 kwa siku. Mhandisi. Christian aliongeza kuwa kazi hiyo inapaswa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 24, kinachoanzia Machi 4, 2011 hadi Machi 3, 2013.

Aidha, Mhandisi Christian amemweleza Naibu Waziri kuwa kwa sasa kazi hiyo ipo katika hatua za awali za uandaaji wa jengo la ofisi za Mkandarasi pamoja na usanifu wa michoro. Hatua hizi za awali zitagharimu dola za kimarekani milioni 37 na zimepangwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi minne inayoishia mwezi Juni 2011.

Naye Naibu Waziri alimpatia nafasi ya kuuliza swali Afisa Bonde wa Wami/Ruvu, Bi. Praxeda Kalugendo ambaye aliomba afahamishwe kiasi kamili cha maji yanayotolewa Mto Ruvu kupitia kupitia chanzo hicho. Bi. Kalugendo alisisitiza pia umuhimu wa kufunga mita zitakazo onesha kiasi cha maji kinachotolewa katika mto huo kupitia chanzo hicho.

Hata hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa DAWASCO Mhandisi Jackson Midala alimtoa wasiwasi Bi. Kalugendo kwa kumueleza kuwa tayari kuna mita moja inayotumika kufuatilia kiasi cha maji yanayotolewa.

Mhandisi Midala aliongeza kuwa wako mbioni kuongeza mita nyingine ili kuimarisha ufuatiliaji wa kiasi cha maji yanayotolewa mto Ruvu kupitia chanzo hicho.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri alifuatana na Afisa Mkuu Mtendaji wa DAWASA, Mhandisi Archard Mutalemwa, Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASCO, Mhandisi Jackson Midala, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO, ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Elmamry pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Maji, DAWASA, DAWASCO na Bonde la Wami/Ruvu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...