Winga wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23,Jamar Mnyate akijaribu kumtoka beki wa timu ya Mkoa wa Kagera, Juama Nade (kushoto) wakati wa mechi ya robo fainali ya nne ya michuano ya Kili Taifa Cup iliyochezwa leo kwenye Uwanja Sheikh Amri Abed jijini Arusha.
Beki wa timu ya Mkoa wa Kagera,Themi Felix (kulia) akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23,Issa Rashid kushoto wakati wa mechi ya nne ya robo fainali ya mashindano ya Kili Taifa Cup iliyochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abed, jijini Arusha.

TIMU ya Taifa Vijana chini ya miaka 23 imetolewa katika hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Kili Taifa Cup baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa sheikh Amri Abeid,jijini Arusha leo.

Magoli hayo yalifungwa kwa njia ya penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 2-2 na kupelekea Mwamuzi wa mchezo huo, Israel Nkongo aamuru zipigwe penati ili kuamua nani mshindi katika mchezo huo.

Kipa wa timu ya Mkoa wa Kagera,Msafiri Davo ndiye shujaa wa mchezo huo kwa kuweza kupangua penati tatu zilizopigwa na wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana na kufanikiwa kupata penati moja.

Wachezaji waliokosa penati hizo kwa upande wa timu ya Taifa Vijana chini ya miaka 23 ni Khamis Mcha,Issa Rashid na Salum Telela wakati aliyepata penati katika timu hiyo ni Awadh Juma.

Wachezaji wa Kagera waliopata penati ni Ibrahim Hassan, Juma Nade na Themi Felix.

Mchezo kwa ujumla ulikuwa mkali baada ya wachezaji wa timu zote kufanya mashambulizi kadhaa na kufanikiwa kupata magoli 2-2 katika dakika 90 za mchezo.

Katika mchezo huo mchezaji Juma Abdul wa timu ya Taifa ya Vijana amejinyakulia kitita cha sh.100,000 baada ya kuibuka mchezaji Bora wa mchezo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...