Diamond akiwa studio. Aliwasili Italy siku ya jumatano na kuanza kazi moja kwa moja katika studio za  SEE RECORDS iliyopo Napoli

 Mkurugenzi wa SEE RECORDS ndugu Salim A. alisema anawakaribisha wasanii wote wa Kitanzania hasa wa Bongo Flava  kufanya kazi na SEE RECORDS, na kuwa kila mwaka watachaguliwa wasanii wawili ambao watapewa nafasi ya kurekodi nyimbo moja na video kwa gharama za SEE RECORDS hii ni kwa ajili kuwapa nafasi zaidi wasanii wa Kitanzania kuonekana kimataifa. Diamond ni msanii wa kwanza katika mpango huo. 

Diamond ambae anaondoka leo kuelekea Ugiriki Athens  ambako anaendelea na show baada ya Sweden na Holland anategemea kurudi tena mwezi Agosti mjini Napoli kwa ajili ya kutengeneza video ya nyimbo hiyo inayotwa KIZAIZAI.

SEE RECORDS.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...