Mwanafunzi Eunas Akimu ambaye anadaiwa kutoroshwa na watu wasiofahamika

BAADA ya mwanafunzi wa kike katika shule ya msingi LIvingstone Njombe kutekwa na kuchinjwa na watu wasiofahamika ,mwanafunzi mwingine wa shule ya sekondari JJ Mungai aliyekuwa kidato cha kwnza Enaus Akimu (14) anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha .

Mwanafunzi huyo ambaye ni mtoto wa katibu wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Hakimu Jackson ametoweka huku zikiwa ni siku tatu zimepita toka mwanafunzi huyo wa shule ya Msingi Livingstone kutekwa na kuuwawa kinyama.

Akizungumza na mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com baba wa mtoto huyo Hakimu Jackson alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 8 majira ya saa 2 asubuhi wakati binti huyo alipokwenda kumsindikiza mama yake mzazi stendi .

Alisema kuwa kutokana na mtoto huyo kutoonekana kwa muda wa siku nzima alilazimika kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi ambako baada ya uchungizi zaidi walimkamata mwanamke mmoja ambaye anadaiwwa kufanya njama za kumtorosha binti huyo na kwa ajili ya kumsafirisha kwenda kusiko julikana.

"Ninawaomba wasamaria wema ambao wanajua alipo binti yangu kuweza kunipigia simu kwa namba0715604957 kwani nimefanya jitihada mbali mbali za kumtafuta ila bado sijampata mwanangu na hadi sasa polisi kuna taarifa na nina RB yenye kumbukumbu namba MFG/1671/2011 "

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi jana majira ya saa 6.41 mchana ili kujua undani wa tukio hilo simu yake ilipokelewa na msaidizi wake na kuwa kamanda alikuwa katika kikao kwa wakati huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...