Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya viongozi wenzake kutoka nchi mbalimbali wakati akishiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi unaofanyikajijini New York jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisalimiana na mtangazaji wa Redio ya Umoja wa Mataifa (UN) Flora Nducha, wakati mtangazaji huyo alipofika kwa ajili ya kufanya mahojiano naye kuhusu maudhui ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi uliofanyika jijini New York, na unatarajiwa kumalizika Juni 10, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mahojiano na mtangazaji wa Redio ya Umoja wa Mataifa (UN), Flora Nducha, muda mfupi baada ya kuhudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu masuala ya ukimwi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaofanyika jijini New York
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na mshauri Mkuu wa ufundi na Asasi ya Viongozi wa Afrika inayohusika na vita dhidi ya Malaria, Dkt. Melanie Renshaw (wa pili kulia) na Balozi wa Tanzania wa Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue (kulia) na Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa inayohusika na vita dhidi ya Malaria, Saleemah Abdul-Ghafur (kushoto), wakati walipomtembelea Makamu wa rais jijini New York Juni 9 na kufanya mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Tacaids, Dkt. Fatma Mrisho (kushoto) na Mkurugenzi wa Tume ya Ukimwi Zanzibar, Dkt. Omari Shauri (kulia) wakati walipomtembelea Makamu wa rais jijini New York Juni 9 na kufanya mazungumzo. Picha na Muhidin Sufiani-OMRMakamu wa raisi azungumzia muitikio wa
Kudhibiti UKIMWI Tanznaia-UN Radio - 10 june 2010
Na Glory Mziray -New York
Makamu wa rais ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mohammed Gharib Bilal amesema Tanzania ni kati ya Nchi zilizofanikiwa kujizatiti katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutahadharisha kuwa tusibweteke na mafanikio tuliyopata ila tuendeleze vita hii ili kufikia malengo ya milenia.
Makamu wa rais amesema Mkakati mpya wa ulimwengu wa kutokomeza UKIMWI kwa mpango wa sifuri 3 ambazo ni maambukizi mapya sifuri, vifo vya magonjwa yanayohusiana na UKIMWI sifuri na unyanyapaa sifuri unaenda sambamba na kaulimbiu ya Tanzania bila UKIMWI Inawezekana na Mpango wa Tanzania kuanzisha mfuko wa UKIMWI ili kukidhi mahitaji ya afua za udhibiti na kufikia Lengo hilo na kwa kufanya hivyo tunakuwa tumejibu mpango wa milenia lengo namba 3,4, na 5 ambao unataka mama mjamzito na mtoto kupata huduma zote za afya zinazohitajika.
Akijibu swali la mtangazaji wa radio UN bi Florah Nducha aliyetaka kufahamu mpango wa dawa unavyoleta ahueni na hivyo kusababisha maambukizi zaidi Makamu wa Rais amesema dawa inafubaza makali ya virusi vya UKIMWI hivyo kupunguza kasi ya kuambukiza ukilinganisha na mgonjwa aambaye hatumii dawa.
akifafanua zaidi kuhusu dawa Makamu wa Rais amesema ushirikiano uliopo na nchi wanachama wa Umoja wa mataifa umetoa mwanga zaidi kwa nchi zilizoendelea kuonesha nia ya kutengeneza dawa za aina ya kupunguza makali(generic) ili kuwezesha watu wote kupata tiba kila inapohitajika na kwa asilimia mia moja.Amezitaja nchi hizo kuwa ni Brazil, India na Thailand.
Akizungumza awali Bw. michele Sedibe, Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia UKIMWI amesema haitavumilika kuona watu wa baadhi ya Nchi wanapata dawa zenye madhara mengi wakati baadhi ya nchi wanapata dawa zenye madhara machache au zisizo na madhara kabisa.
akizungumzia kuwasaidia wanawake kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI mh. makamu wa rais amesema tafiti mbalimbali za masuala ya kuwasaidia wanawake zinaendelea na Tanznaia ina nafasi bado ya kutumia kukinga maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto njia ambayo mpaka sasa inatumika kwa asilimia 53 tu japokuwa tuna nafasi ya kutumia kwa asilimia 100 .
kauli hii imeungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia UKIMWI- UNAIDS Bw. michele Sedibe ambaye alisema watoto 400,000 wanazaliwa na virsi vya UKIMWI kila mwaka bara la africa wakati mabara mengine hakuna mtoto anayezaliwa na virusi vya UKIMWI.
nia ya Makamu wa rais ya kuwasaidia wanawake katika kudhibiti UKIMWI inaenda sambamba na ari iliyotolewa na Katibu wa Umoja wa Mataifa alipokuwa akifungua mkutano wa wake za marais alisema wanawake wakiumwa tunapoteza silaha nambari moja inayotupatia chakula kwa watoto na familia.


Radio ya UN inabidi waende kisasa zaidi..
ReplyDeleteSiyo kumsogelea karibu namna hiyo mheshimiwa kwa ajiri tu ya kukosa wireless microphone za mahojiano.
Mnatuangusha jamani.. pigeni hatua!