Hello!  I'm happy to announce that my documentary Twiga Stars: Tanzania's Soccer Sisters has finished touring film festivals and is finally up online and available for all to see at: www.twigastars.com

If you go to the website, you can also donate to help the team on their way to the All-African Games this September. Thanks to everyone for all of your support, and please pass on the link and spread the world!

Keep in touch!
Nisha
-------------------------------------------------------
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) imeingia kambini Juni
24 mwaka huu kwenye hoteli ya Itumbi iliyoko Mwembechai, Dar es Salaam kujiandaa
kwa michuano ya wanawake ya COSAFA itakayofanyika jijini Harare, Zimbabwe.

Twiga Stars inayofundishwa na Kocha Charles Boniface akisaidiwa na Nasra Mohamed
imeingia kambini ikiwa na wachezaji 25 na inafanya mazoezi katika viwanja vya
Tanganyika Packers ulioko Kawe na Karume.

Michuano hiyo ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika
(COSAFA) inashirikisha timu nane na itaanza Julai 2 hadi 9 mwaka huu. Twiga
Stars ambayo pia inajiwinda kwa michezo ya All Africa Games itakayofanyika
Septemba mwaka huu jijini Maputo, Msumbiji inashiriki kama timu mwalikwa.

Timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo ambayo mechi zake zitachezwa katika
viwanja vya Rufaro na Gwanzura ni Zimbabwe, Lesotho na Botswana. Nyingine ni
Afrika Kusini, Zambia, Msumbiji na Malawi.

Twiga Stars ambayo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Zimbabwe, Lesotho na
Botswana itacheza mechi yake ya kwanza Julai 2 mwaka huu dhidi ya Botswana
kwenye Uwanja wa Gwanzura.

 Siku inayofuata itacheza na Lesotho kwenye Uwanja wa Rufaro kabla ya kumaliza
mechi za makundi Julai 5 mwaka huu kwa mechi dhidi ya wenyeji kwenye Uwanja wa
Gwanzura.

Hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itafanyika Julai 7 mwaka huu. Kila kundi
linatoa timu mbili kuingia katika hatua hiyo na nusu fainali zote pamoja na
fainali zitachezwa Uwanja wa Rufaro.


Boniface Wambura
Ofisa Habari


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...