MASHABIKI WA YANGA WAKISHANGILIA MOJA KATI YA MAGOLI YALIYOFUNGWA NA TIMU YAO



Mshambuliaji wa Yanga Davies Mwape akiruka daruga la beki wa  El-Mereikh ya Sudan, Nasr Eldin wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame Castle uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.

PICHA YA PAMOJA YA MANAHODHA WA TIMU ZOTE NA WAAMUZI
MASHABIKI WA SIMBA WAKIIPA SAPOTI EL-MEREIKH
KIKOSI CHA YANGA.
  
KIKOSI CHA EL-MEREIKH YA SUDAN.
Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2011

    Kwa kweli Mechi ya jana ya Yanga ndio ilikuwa ufunguzi. Mechi ya Juzi ni bonanza tu! maana mpira ulipigwa jana si wa mchezo maana ulikuwa ni wa hali ya Juu sana. nawapa pongezi Yanga kwa kiwango walichokionyesha maana wamefanya maandalizi kwa kipindi kifupi lakini wameweza kutupa burudani ambayo kwa wanaojua mpira watakuwa wamefaidi kwa kiassi kikubwa. matatizo kama yapo yatakuwa yanarekebishika kwani hata Roma haikujengwa kwa siku moja. ila kwa kweli mmetupa moyo sana sisi wapenzi wa mpira. Timu nyingine wanabaki kucheza na Rufaa mkononi. Jana mmepata aibu na Rufaa zenu. mngekata nyingine kuwa Refa alikunywa bia 2 za baridi kabla ya mechi haijaanza! maana mnapenda kulalamika ovyo ovyo kama kondakta wa daladala!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2011

    MASHABIKI WA SIMBA MNAONYESHA KIASI GANI HAMNA UZALENDO MECHI KAMA HII ILIBIDI MUWEKE U-SIMBA NA U-YANGA PEMBENI NA KWA PAMOJA MUISHANGILIE YANGA ILI KUWAPA MOYO VIJANA WA NYUMBANI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...