Mkurugenzi Kiongozi wa Filamu ya White & Black kutoka Shirika la UNDER THE SAME SUN,Jean Francois (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari juu ya Filamu hiyo inayoelezea ukatili unaofanyika kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini,katika ukumbi wa hoteli ya Seyyida Hotel,Zanzibar.Kulia  ni Afisa Mipango wa Shirika la UNDER THE SAME SUN,Christopher Andendekisye na katikati ni  Mtendaji wa Shirika hilo,Seif Kondo.

FILAMU iliyobeba ujumbe kuhusiana na unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini ya ‘WHITE & BLACK’ imeingia kwenye Tuzo ya Osmane Sembene, zinazotarajiwa kutolewa Juni 26 kwenye tamasha la Filamu za nchi za Majahazi maalufu kama ZIFF.

Akiongea na waandishi wa habari jana mjini hapa, Afisa Mipango wa shirika la Under the Same Sun, Christopher Andendekisye alisema kuwa filamu hiyo iliyotengenezwa kwa njia ya makala maalum iliyomhusisha mwandishi wa habari za uchunguzi nchini, Vicky Ntetema imeingia katika tuzo hizo na itaendelea kuonyeshwa sehemu mbali mbali ili kufikisha ujumbe kwa jamii nzima juu ya unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi na ikiwezekana kukomesha kabisa ukatili huo utokanao na imani potofu.

Katika filamu hiyo, imeonyesa matukio halisi ya picha zilizotokea kwa walemavu hao huku kila mmoja aliyeshuhudia filamu hiyo wakiwemo waandishi wa habari walisisimka na kujawa na huzuni.

“Tanzania na sehemu nyingine za Afrika Mashariki, waganga wadanganyifu wamekuwa wakitumia viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi katika tiba zao, wakiamini kuwa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi huleta bahati na mafanikio hii si kweli tunaomba wanahabari kufikisha ujumbe huu ilikokomesha kabisa” alisema Andendekisye.

Ndani ya filamu hiyo, Ntetema anaonekana kufatilia hatua moja baada ya nyingine kwa waganga wa kienyeji na sambamba na wauaji wa watu hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2011

    Huwa wanasema "BLACK AND WHITE"!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...