JESHI la Polisi nchini limeendelea kusisitiza kuwa halikuwa limefanya makosa kumkamata Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe, kwa kile ilichokitaja kuwa hana kinga ya kumzuia kukamatwa.

Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la
Polisi Kamishna Paul Chagonja

Akizungumza na wanahabari leo hihi jijini Dar es Salam, Mkuu wa  Operesheni wa  Mafunzo ya jeshi la Polisi Kamishna Paul Chagonja alisema kuwa Mbowe kama raia mwingine wa Tanzania yupo chini ya sheria hivyo hakuna kinga yoyote inayomzua kukukamatwa.

Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na jeshi la polisi ni utekelezaji wa amari ya mahakama kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo, kwani mtu yeyote anaweza kukamatwa hisipokuwa Rais pekee ndio mwnye kinga ambaye kukamatwa kwake kuna fuata taratibu.

Kauli hiyo ya Chagonja, inakuja siku mbili baada ya jeshi hilo kumkamata Mbowe ikiwa ni baada ya kupewa amri na mahakama ya Arusha kufanya hivyo, baada ya Mbowe kuiuka amari ya kufika mahakamanio kuhudhuria kesi inayomkabili.

Chagonja alisema kinga ya wabunge inayofahamika kwa wabunge, inafanyakazi pale mbunge anapokuwa katika maeneo ya bunge na akiwa nje ya bunge mbunge anakamatwa bila ya kujali kinga hiyo.

Aliongeza kuwa Mbowe alikuwa amejidharirisha kwa kutokwenda mahakamani alipohitajika, na kwamba jeshi halikumdahirisha kwa kumkamata kwani limetekeleza amri ya mahakama.

Katika hatua nyingine Chagonja alitoa onyo kali kwa watu wote walio na mpango wa kuvunja amani kwa matakwa yao binafsi, kwakuwa jeshi hilo kamwe halitowafumbia macho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    Mbowe alikamatwa ili Kuwasha Mitambo ya Dowans bila kelele kwani attention yote ilihamia kwenye mambo hayo ya kisiasa. HONGERENI SANA!
    Mimi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2011

    Hata Marekani amri ya ya mahakama haina Congressman, Sanator ama Rais. Wanakwenda jela tu! Huo ndio utawala wa sheria. Bahati mbaya wanasiasa wetu wa vyama vyote wakati mwingine wanajisahau na kudhani sheria ni ya watu wadogo tu. Hongera Polisi kwa kutekeleza sheria na kuweka mfano madhubuti. Hapa hakuna siasa hata kama Chadema wangetaka ieleweke hivyo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2011

    Anon wa 06:18:00 PM; Sasa unataka mitambo isiwashwe ili uwashe generata yako? Nchi yetu haiendelei kwa mawazo kama yako ambayo kila siku kupinga wafanya biashara kwa sababu zilezile - wananyonya, makabaila etc. Lazima tuwe na mtizamo tofauti wa kukuza na kuwatia moyo wafanyabiashara wakubwa. Kupata faida zi dhambi kwenye biashara. Mbona tunafurahia umaskini wetu tu!!! Akipata mwingine - fisadi!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2011

    HAKIMU LAZIMA APANDISHWE CHEO BANAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2011

    Hakika tunakushukuru igp pamoja na chagonja kwa kumpeleka arusha na ndege na sio haya magari tuliyoyazoea yakiwabeba watuhumiwa, kweli mmempa heshima yake japo alisindikizwa kama gaidi, natumaini chagonja umesikia aliyoyasema hakimu kuwa muheshimiwa mbowe hakuwa na hatia bali mdhamini wake, IGP MUNGU akupe hekima katika kipindi hiki ili uitende kazi yako kwa uadirifu bila jazba wala siasa

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2011

    NYIE MNAOSEMA UTAWALA WA SHERIA HUYU MBOWE ANGEKUWA NI KIONGOZO WA CCM BUNGENI ANGEFANYIWA HIVI? KAMA JIBU HAPANA BASI HUU SI UTAWALA WA SHERIA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2011

    Sema Kiogozi gani wa CCM kaitwa mahakamani na akakataa?

    ReplyDelete
  8. Jeshi la Polisi nawapa pongezi kwa kazi nzuri mliyofanya. mtu kama mbowe ambaye ni kiongozi mkubwa na kioo cha jamii alitakiwa kuwa mfano wa kutii sheria. sasa yeye anajifanya yuko juu ya sheria. ndio ajue kilichomfanya avunje sheria ndicho kilichomsababanishia yote. sema mimi nilitaka asafirishwe na landrover tena ambayo haina AC ili ajute kudharau sheria za nchi.
    Polisi nawapa big up!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2011

    Ann.wa saa 2;50, ur very right, asingefanyiwa hivyo na watz wanashaikia vile ni wanafiki wako huku na huku hawana msimamo, kweli angekuwa Mbunge wa chama cha mafisadi(ccm) wala hata tusingesikia.
    Ila sisi tuko kama watoto. Ila nawapongeza sana Wanachadema kwa umoja wao. CCM hawana lolote kwa hii mikoa waandike 0.Imagine jana polisi wangeenda na mabomu yao, ingekuwa fujo tupu, ila nimeamini kuwa polisi ndo wanaanzishaga kwa matumizi mabaya ya mabomu, Chadema oyeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2011

    Anon: 02:50:00 AM; Una matatizo ya akili, wewe ni sawa na wale wachochezi wa vurugu nchini. Unajua vizuri lakini sababu za Mbowe kukamatwa? au unatoa comment bila kufuatilia sababu? Acha siasa za kibaguzi, huna la kulalamika acha mahakama na polisi wafanye kazi yao.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2011

    we anonymous wa kwanza hapo juu kumbe umeliona hilo eeh. serikali yetu ni wajanja na amin nawaambia wakirudi makwao mwisho wa siku hutafakari na kumshukuru mungu kwa kufanikiwa kuwafumba macho watanzania hata tukasahau mambo ya msingi tukielekeza fikra na mawazo yetu kwenye hoja zisizo na maana. Mungu anisamehe kama nakufuru ila nawasihi ndugu zangu hata suala la loliondo tuliangalie kwa jicho la "tatu", nalo pia napata hisia limekaa kisiasa zaidi kwa jinsi serikali ilivyoamua kulivalia njuga ukizingatia ni kipindi ambacho mustakabali wa maswali mengi tuliyonayo watz haukuwa ukijulikana na sasa tumeshasahau yote.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2011

    kaka michuzi kama kuna uwezekano wa kuweka like na dislike options.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...