Gramafoni (gramophone) ni chombo cha muziki cha kwanza kutumia sahani za santuri kupigia muziki?  Chombo hiki, kiisichotumia umeme bali kinaliza muziki ulio katika santuri  kwa kujaza kwa kuzungusha hendeli,  kilitambulishwa  miaka ya 1877  na kuendelea kutumika dunia nzima hadi miaka ya 1980. Wakati Gramafoni inaundwa kwa jina la 'His Master's Voioce,  kilikuwa ni chombo cha kuchezea santuri na pia kurekodia muziki.  Alikuwa ni mjasiriamali na fundi wa Kimarekani Thomas Edson ambaye alikuja kuwa supa staa baada ya kutengeneza Gramafoni iliyotumia sahani kubwa ya santuri iliyoweza kutengenezwa kwa wingi na kufanya kuwa kifaa kipya cha kuuzia muziki duniani na kuifanya gramafoni kutamba katika karne ya 20 kabla ya nafasi yake kuchuliwa na compact disc na kasha vifaa vingine vya kurekodia na kuchezea muziki vyenye kutumia teknolojia ya digito. 

Hata hapa nyumbani gramafoni za ‘His Master’s Voice’ zilizokuwa maarufu kwa picha ya mbwa anayechungulia kipaaza sauti, zilikuwepo na inaonesha bado zipo japo kama pambo tu la vitu vya kale. Gramafoni moja ipo sehemu za mapokezi ya Double Tree hotel kule Masaki jijini Dar es salaam, kwa wasiowahi kuiona.
 Gramafoni ya 'His Master's Voice'
Ankal na Gramafoni hiyo katika mapokezi ya Double Tree at Hilton hotel jijini Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2011

    Marehem babu yangu alikuw nayo,, kule tukuyu kiwira karibu na stand ya mabus kwa wale waliokuwa wanamfaham mzee simon... kwa unoko alikuwa namba one pamoja na mzee mwamtobe

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2011

    Michuzi
    Ahsante kwa kumbukumbu ya utoto wetu.
    Nyumbani kwetu tulikuwa na santuri kama hiyo hapo juu, na katika sikukuu ya Eid watoto wote wa ujirani walikuwa waja kwetu na tunafanya dansi, nafikiri ni kama vile disco za sasa.
    Jambo jingine ni kwamba nilipomtembelea brother wangu kule Kingston Upon Thames, nilikwenda kwenye benki ya Lloyds na ukiingia kuna kisahani cha shaba kinachosema kuwa huyo mbwa kwenye santuri alikuwa anaitwa NIPPER na alikufa na kuzikwa hapo 1895

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...