![]() |
Dr Mukwege na tuzo yake |
Dr Mukwege ameshinda tuzo ya kimataifa kutoka ufalme wa Ubeligiji kwa mchango wake wa kusaidia jamii. Hospitali ya Panzi inahusika na kuwapokea, kuwatibu, kuwapa ushauri nasaha, kuwasaidia na kuwawezesha wanawake waliobakwa Jamhuri ya Kimokrasia ya Congo na inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na wahisani mbalimbali wanaopinga ukatili dhidi ya wanawake na hasa ubakaji.
Amezungumza na mwandishi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa mjini Bukavu Mseke Dide kuhusu tuzo hiyo iliyoambatana na kitita cha fedha dola za Kimarekani zaidi ya laki mbili, kuhudu tuzo yenyewe, anachokifanya hospitali ya Panzi na malengo yake ya baadaye.
Kusikiliza mahojiano haya bofya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...