Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifafanu jambo kwa ufasaha mapema leo asubuhi kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa kitabu cha Kilimani Sesame Kampeni ya Elimu ya Malaria,hafla hiyo imefanyika kwenye viunga vya ofisi za WAMA,jijini Dar.Kampeni hiyo inajumuisha matangazo manne ya kuelimisha jamii jinsi ya kuzuia Malaria (kwa TV&Radio) kwa Kiswahili,Matangazo yatakayokuwa yakirushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Clouds TV.Aidha katika hafla hiyo idadi kubwa ya Watoto walipata nafasi ya kufika ofisi za WAMA,jijini Dar na walipata nafasi maalum ya kusomewa na Mke wa Rais,Hadithi mbadala ya chandarua  salama (safe Nets) iliyosambazwa nchi nzima ili kuunga mkono PSAs.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,Mh Jordan Lugimbana akiwasalimia wageni waalikwa pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi wakiwemo na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa Kilimani Sesame Kampeni ya Elimu ya Malaria mapema leo asubuhi.
Pichani kulia ni Mama Sadaka Gandi ambaye ni mtaalamu wa masula ya mawasiliano na Afya wa Kampeni ya Zinduka Malaria Haikubaliki akiwa ameambatana na mgeni  rasmi,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya WAMA mapema leo asubuhi,kwa ajili ya kuzindua Kilimani Sesame Kampeni ya Elimu ya Malaria.
Baadhi ya Wageni waalikwa .
Pichani ni baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye  maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika,ambapo pia Mke wa Rais wa Tanzania,Mama Salma Kikwete alizindua Kilimani Sesame kampeni ya Elimu ya Malaria,kwa kushirikiana na Sesame Semina,Watayarishaji wa Kilimani  Sesame,WAMA na Malaria No More.Hafla hafla hiyo imefanyika mapema leo asubuhi kwenye viunga vya ofisi za WAMA,jijini Dar.
Mama Salma Kikwete akikata utepe mbele ya baadhi ya watoto na wageni waalikwa waliofika kwenye ofisi za viunga vya WAMA,kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Kilimani Sesame kampeni ya Elimu ya Malaria.
Mama Salma Kikwete akipiga makofi pamoja na watoto mara baada kuzindua rasmi kitabu cha Kilimani Sesame kampeni ya Elimu ya Malaria.
Pichani ni Wageni waalikwa mbalimbali waliofika  katika  maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika,ambapo pia Mke wa Rais wa Tanzania,Mama Salma Kikwete alizindua Kilimani Sesame kampeni ya Elimu ya Malaria,kwa kushirikiana na Sesame Semina,Watayarishaji wa Kilimani  Sesame,WAMA na Malaria No More.Hafla hafla hiyo imefanyika mapema leo asubuhi kwenye viunga vya ofisi za WAMA,jijini Dar.
Mgeni rasmi,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni hiyo,iliyofanyika mapema leo asubuhi kwenye viunga vya ofisi za WAMA,jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...