![]() |
Bwana Adhallah SinganomMkuu wa masoko na mawasiliano benki ya Stanbic akijaribu uwezo wake wa kufukuza upepo na wanariadha wetu wa Special Olympics |
![]() |
Kikosi chetu cha Special Olympics |
Benki ya Stanbic Tanzania leo imetoa msaada wa Sh milioni 3 ili kuwezesha timu ya Tanzania kushiriki katika michezo ya olimpiki maalum (Special Olympics) huko Athens Ugiriki mwaka huu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya fedha hizo yaliyofanyika katika ofisi za Special Olympics Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Stanbic Abdallah Singano alisema fedha hizo ni sehemu ya misaada ya jamii ya benki hiyo.
“Benki yetu inafurahishwa kuweza kuunga mkono chama hiki cha Olympiki maalum, tunawapa pongezi kwa juhudi zao zinazowezesha timu ya Tanzania kushiriki michezo hii kila wakati. Vile vile tunafurahia zaidi kuweza kuwasaidia wanamichezo hawa maalum na tunawatakia heri na mafanikio katika mashindano hayo,” aliongeza Singano.
Michezo ya olimpiki maalum huko Athens itafanyika kuanzia tarehe 25 Juni hadi Julai 4 na inategemewa kuleta wanamichezo zaidi ya 7,000, kutoka nchi 185 duniani kote, makocha 3,000, wasaidizi wa kujitolea zaidi ya 25,000, maelfu ya familia na watazamaji kuwashangilia wanamichezo hawa.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya chama hicho cha Olimpiki Mkurugenzi wa Taifa Frank Chacha alitoa shukurani zake kwa benki ya Stanbic kwa msaada huo utakaowezesha timu hiyo kushiriki katika michezo hiyo hivi karibuni.
“Tanzania ni katika nchi 200 ambazo zinashiriki katika programu hii inayotoa mafunzo mwaka mzima kwa washiriki mbali mbali watoto na watu wazima ambao wana ulemavu wa akili. Tunatuma timu ya wachezaji 11 na maafisa wane. Hii ni mara ya saba kwa Tanzania kushiriki katika michezo hii yenye nia ya kuboresha afya, kufurahi na kushirikiana katika vipaji na zawadi mbali mbali kwa wana michezo hawa maalum,” alielezea Chacha.
Benki ya Stanbic Tanzania inaamini katika kujihusisha katika biashara yake na pia katika kusapoti jamii katika program mbali mbali zinazoleta maendeleo. Benki hii ina msimamo sio katika kukuza uchumi tu bali katika kuimarisha taasisi za kiraia na jamii kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...