Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akimvalisha medali mshindi wa kuogelea mita 100 katika mashindano ya klabu bingwa Tanzania kwa washiriki chipukizi Agnes Kimimba.
Waogeleaji wa timu ya KMKM kutoka Zanzibar kutoka kushoto Ally Hamiss,Omary Abdallah na Othman Ally wakibusu medali zao za dhahabu mara baada ya kutangazwa washindi wa klabu bingwa Tanzania kwa upande wa watu wazima,mashindano hayo yamefanyika Funkys masaki jijini Dares salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Katibu Mkuu wa TSA Noel Kiunsi akiwaangalia waogeleaji Ankitu Bhatt(15)na Macayla Buchanan(15)wa timu ya Stingray klabu ya jijini Dares Salaam wakishangilia ushindi wao mara baada ya kutangazwa washindi wa kuogelea katika mashindano ya klabu bingwa Tanzania kwa waogeleaji chipukizi,mashindano hayo yalifanyika Funkys jijini Dares salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Katibu Mkuu wa TSA Noel Kiunsi(kushoto)na Ofisa mkuu mwendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Correia wakiwakabidhi kombe timu ya KMKM kutoka Zanzibar waliochukua ushindi wa mashindano ya klabu bingwa Tanzania kwa upande wa watu wazima,Mashindano hayo yalifanyika Funkys jijini Dares salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...