

Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR –Mageuzi) akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde (CCM) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Balozi wa Vietnam nchini Tanzania Bw. Nguyen Duy Thien akizungumza jambo wakati wa mkutano kati ya viongozi wa Bunge la Vietnam na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama leo mjini Dodoma.

Naibu waziri wa Filamu na Sanaa za Maigizo wa Iran Bw. Javad Shamaqdar (wa kwanza kulia) akimkabidhi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi mkoba wenye kazi za wasanii kutoka nchini Iran leo mjini Dodoma. Anayeshuhudia ni mshauri wa masuala ya Utamaduni wa Ubalozi wa Iran nchini Bw. Morteza Sabouri. Picha na MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...