Banda la NHIF kwenye maonesho ya kimataifa na maadhimisho ya miaka 50 ya wiki ya utumishi wa umma yatakayokuwa yakiendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
Mwanachama akipokea kitambulisho chake kutoka kwa Meneja wa Uanachama Bi. Ellentrude Mbogoro ndani ya banda la mfuko wa taifa wa bima ya afya kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika viwanja vya mnazi mmoja,wanachama wa mfuko wamepewa fursa ya kuwasilisha fomu za maombi ya kupatiwa vitambulisho hivyo wafike pia kwa ajili ya kupatiwa elimu ya msingi kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za NHIF na ile ya Mifuko ya Afya ya Jamii
.Elimu ya Mafao yatolewayo na NHIF ni Msingi Imara utakaomuwezesha wanachama na wadau mbalimbali wa mfuko huu kuelewa vyema umuhimu wa kujiunga na ile ya mifuko ya afya ya jamii kushoto ni Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi.Anneth Hyera akimpatia maelezo muhimu mdau wa nhif kuhusu mifuko hii inavyofanya kazi kwa manufaa ya watanzania walio wengi pembeni timu nzima ya Mfuko ikiwa tayari kuwapatia huduma wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa na maadhimisho ya miaka 50 ya wiki ya utumishi wa umma yatakayokuwa yakiendelea kwenye viwanja vya mnazi mmoja.
Huduma mbalimbali za upimaji wa Afya zinaendelea kutolewa katika banda la mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika maonyesho ya kimataifa ya miaka 50 ya wiki ya utumishi wa umma hapo ni Dr. Shitima kutoka NHIF akimpima uwiano wa uzito na urefu (BMI) Bi Josephine Kayuni na kupewa ushauri wa kitaalam,NHIF umewataka wadau na wanachama kutembelea na kuchangamkia huduma za upimaj wa Afya zitakazotolewa bandani hapo bure.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...