Mjomba Ankal,
Hii ni mara yangu ya kwanza kuandika humu, japo ni mpenzi wa kutupwa wa Blog yetu ya jamii ambayo piga ua lakini haina mfanowe. Hivyo usintie kapuni maana mteja ni mfalme nawe ni mtumishi wetu. Sawa bwana? SAWA!
Mie shida yangu ni ndogo tu, na nnaomba wadau wenzangu wanisaidie. Kama ni kwa mawazo, sawa. Kama ni kwa kukosolewa kwa kunoa stepu sawa pia.
Naishi Ughaibuni, kama unavyopenda kuita. Niko Marekani mwaka wa sita sasa. Hali ya maisha si mbaya sana kwani baada ya kula nondozzz zangu hivi sasa napiga boxi kwa kwenda mbele. Msaada ninaoomba ni kutaka kujua je, huko nyumbani kweli mambo ni shwari (napanga kurejea karibuni) maana nikipitia magazeti na hii mitandao yenu nachanganyikiwa. Upande mmoja kwenye hii mitandao nakuta khabari kwamba mambo si safi, kuna shida, hakuna umeme wala maji, usafiri shida na mifoleni hiyoo. Kwa upande mwingine naona watu wanakula nchi, wanfurahi na kila siku minuso kwa kwenda mbele... Sasa nimuamini nani? Kwamba nchi yangu nnayoipenda iko katika shida am raha??
Mniwie radhi wadau. Nauliza hivi kwa sababu boxi limeshanchosha na sasa nataka kurejea nyumbani. Ila kabla ya kufanya hivyo nataka nipate uhakika kwamba mambo ni mabaya ama mazuri ili nijikoki kabisa na kurejea nikiwa najua moja.
Ankal nawasilisha hoja huku nikiomba unilinde dhidi ya waosha vinywa, maana kuna watu humu hawana dogo wala zuri. Wao ni kukatishana tamaa tu. Swali ni je nirejee kula vumbi ama niendelee kubeba boxi????
Mdau Arizona
Hii ni mara yangu ya kwanza kuandika humu, japo ni mpenzi wa kutupwa wa Blog yetu ya jamii ambayo piga ua lakini haina mfanowe. Hivyo usintie kapuni maana mteja ni mfalme nawe ni mtumishi wetu. Sawa bwana? SAWA!
Mie shida yangu ni ndogo tu, na nnaomba wadau wenzangu wanisaidie. Kama ni kwa mawazo, sawa. Kama ni kwa kukosolewa kwa kunoa stepu sawa pia.
Naishi Ughaibuni, kama unavyopenda kuita. Niko Marekani mwaka wa sita sasa. Hali ya maisha si mbaya sana kwani baada ya kula nondozzz zangu hivi sasa napiga boxi kwa kwenda mbele. Msaada ninaoomba ni kutaka kujua je, huko nyumbani kweli mambo ni shwari (napanga kurejea karibuni) maana nikipitia magazeti na hii mitandao yenu nachanganyikiwa. Upande mmoja kwenye hii mitandao nakuta khabari kwamba mambo si safi, kuna shida, hakuna umeme wala maji, usafiri shida na mifoleni hiyoo. Kwa upande mwingine naona watu wanakula nchi, wanfurahi na kila siku minuso kwa kwenda mbele... Sasa nimuamini nani? Kwamba nchi yangu nnayoipenda iko katika shida am raha??
Mniwie radhi wadau. Nauliza hivi kwa sababu boxi limeshanchosha na sasa nataka kurejea nyumbani. Ila kabla ya kufanya hivyo nataka nipate uhakika kwamba mambo ni mabaya ama mazuri ili nijikoki kabisa na kurejea nikiwa najua moja.
Ankal nawasilisha hoja huku nikiomba unilinde dhidi ya waosha vinywa, maana kuna watu humu hawana dogo wala zuri. Wao ni kukatishana tamaa tu. Swali ni je nirejee kula vumbi ama niendelee kubeba boxi????
Mdau Arizona
Mie nisingependa nimdanganye huyu bwana hapo juu eti kwa kumwambia hali ni shwari, ukweli shilingi huku ni ya kukimbiza tena sana, mzee umesema umekula nondozz zako hivi karibuni, cha msingi ni kwamba ukija hapa bwana tafuta kijibarua chako hata kujiariri mwenyewe tu hushindwi maisha, walijisemea wamachinga hata kwa kuuza maji ya uhai dar unaishi sembuse una nondozz zako bwana!!! Hapa ndio nyumbani, huko ni kwa watu tu jamani hata upige box kivipi bado hailipi utang'aa uso kwa ajili ya hali nzuri ya hewa lakini issue ipo pale pale, ulipe kodi ya nyumba, mara sijui vitu gani na mbaya zaidi mzee ume upate demu akuzalie mtoto hiyo sio dhamira yako lakini ndio inatokea basi si balaa hilo tena, utaambiwa umlipie huduma mtoto na ndio hujajiandaa jamani hebu karibuni nyumbani tupambane na hali hii ngumu ambayo imeshakuwa wimbo wa taifa letu. Ipo siku tutafanikiwa tu jamni cha mtu mavi.Nasema hivyo mie yalinishinda na nipo home navuta maisha japo kimkanda. Ushauri wangu ndugu tuone na kusikia wengine.
ReplyDeletesasa ndugu yangu unataka kuniambia kama kuna izo shida ulizo ambiwa hutorudi kwenu? kwasababu kuna shida kwenu ni kwenu tu hata kama kutakuwa vipi na hasikudanganye mtu maisha mabovu na mazuri wewe mwenyewe jinsi gani umejipanga ndio utaona maisha yalivyo kama ni magumu au matamu kuna watu wanaishi maisha mazuri hafanyi kazi oficini na wala havai tai na kuna wanao vaa tai kubwa na wanaishi maisha magumu kwaiyo usitishike ni wewe mwenyewe jinisi gani utajipanga
ReplyDeletekaka kama ulivyo omba kulindwa na waosha vinywa naheshimu hilo kukusaidia nikwamba pana usemi wa kiswahili una sema AKILI NI?????? uta malizia kila mtu???? sasa nijibu unalo mwenyewe
ReplyDeleteWe mbeba box, kwani huna ndugu zako wakueleze hali halisi? au hukuaga kwenu au uliondoka kwa mbwembwe? rudi home bana wewe mambo ni kama ulivyoacha miaka 6 iliyopita. acha kujidhalilisha huko kwa kubeba mabox. njoo uendeleze kampeni ya KILIMO KWAZA Kinalipa sana.
ReplyDeleteMdau wa Arizona,
ReplyDeleteKwanza nikupongeze kwa kula nondozz! Baada ya hapo nikupe ujumbne kwamba, nyumbani ni nyumbani, hata kama ni kichakani, kurudi utarudi tu hata kama si leo wala kesho. Unayoyasoma ktk blogu na magazeti tando ndo hayo yaliyopo, kuna umasikini wa hali ya juu kwa upande mmoja na utajiri wa kutupwa kwa upande mwingine, kwamba kuna mwingine anakula na kumwaga chakula ilhali nyumba ya jirani wanalala njaa kwa kukosa chakula. Ndivyo maisha yalivyo. Kama unapanga kurejea maskani we rejea tu, ila kama unapanga kulowea na kupiga boksi huko ukimbizini na yenyewe ni sawa tu, ni sehemu ya maisha, ila kumbuka kuwekeza kwenu.
Samahani kwa maandiko mengi.
Mdau wa Mwenge
Maisha si maji na umeme tu, bali ni mkusanyiko wa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuthaminiwa. Huko uliko huna thamani. Kazi unayofanya hata kama ina malipo makubwa ikilinganishwa na Bongo lkn haiendabi na hadhi yako. Unaishi km kwenye nyumba ya kupanga, kuchungulia tarehe ya visa kwisha. Ya nini yote hayo?
ReplyDeleteBongo km una elimu yako maisha ni mazuri maradufu ya ughaibuni. Mimi niko ktk nchi mojawapo za Mashariki ya Mbali na nafanya kazi professional lkn nikimaliza mkataba wangu narejea Bingo kwa maana naona kabisa kuna kitu nakosa ktk maisha yangu. Rudi Bongo kale maisha, achana na mausha ya kudhalilishana hayo.
Urejee kula vumbi ama uendelee kubeba boxi???
ReplyDeleteHuo ni mtizamo au perception uliyonayo kulingana na jinsi unavyolinganisha maisha ya Arizona na Tanzania.
Labda niseme tu, nchi zote zinatofautiana, na unapojaribu kulinganisha nchi kama Tanzania na nchi zilizoendelea, tofauti bado ni kubwa sana, hasa kimaendeleo. Kwa hiyo usitegemee kwamba ukirudi nyumbani utakuta hali kama ya Arizona. Lakini hiyo haimaanishi kwamba ukirudi Tanzania huwezi kuwa na maisha mazuri la hasha. Hiyo itategemeana zaidi na mipangilio yako, jinsi unavyojiandaa kimaisha, kazi unazofanya pamoja na resources nyingine ulizonazo. Wapo watu wengi tu wanaishi maisha mazuri, lakini pia bado tunao maskini wengi sana katika maeneo mbali mbali nchini, hata hapa hapa DAr hali si nzuri kwa kila mtu. Kwa hiyo hizo fursa unazozipata kama ukizitumia vizuri utaishi vizuri iwe hapa bongo au mahali pengine popote.
Mi nakushauri kama ifuatavyo: Kwanza jambo kubwa la kukuvutia kurudi nyumbani ni utulivu uliopo,hakuna vita watu wanaendelea na shughuli zao kama kawa,ingekua unatoka huko unarudi nchi kama somalia hapo ulipaswa kujiuliza mara2 nyumbani ni nyumbani tu, Pili hali ya uchumi kweli sio nzuri sana wala sio mbaya sana ila nchi inasonga mbele. Hayo unayoyasikia na kuyaona kwenye mitandao na magazeti nyingi ni propaganda za wafuasi wa vyama ambao wapo kila kona hata wahariri na waandishi wa habari siku hizi hawana uzalendo tena zaidi wametanguliza interest za wanaowapenda, hakuna jema linalofanywa na serikali wanaloliona kwa sababu vichwa vyao vilishachakachuliwa na wanasiasa wa maandamano. Ajira bado ni tatizo kama ilivyo hali ya uchumi na hilo ni tatizo la ulimwengu mzima jitihada zinafanyika na hii inahitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu kwa kuwa wabunifu na kuacha kuisubiri serikali. Rasilimali ni nyingi za nchi zinahitaji watu wakuzifaidi. Likianza shirikisho la E.Afrika nadhani wakenya watazifaidi sana rasilimali za nchi yetu kwa sababu ni wajasiriamali sana na hawasubiri serikali iwafanyie kila kitu. Kila mtu akiwajibika vilivyo ndipo tunaweza pia kuwajibishana na sio kulalamika tu huku hatutimizi wajibu wetu ktk ngazi mbalimbali na kuendelea kuilaumu serikali.
ReplyDeleteNyumbani ni Nyumbani, Pawe na shida au raha haijalishi!
ReplyDeleteKijana rudi home faster! Kwenu ni kwenu tu no matter what!
Punguza uzungu!
Mdau.
kaka huku tanzania ni kweli hali ngumu na bado watu wanakula bata kila siku yaani mambo ni mchanganyiko,, ila kama kweli boksi umebeba la kutosha basi utakuwa na vijipesa ambavyo unaweza kujawekeza hapa bongo na ww ukajumuika kula bata na wenzako kama kawa, ila kama unataka kuja kutafuta kazi huku sikushauri, labda uwe na godfather wa ukweli... mwisho wa siku lazima utambue "no one part like africans!"
ReplyDeleteur pathetic!unawezaje fikiria mala mbili kurudi kwenu,hata km wanatumia vibatari kwenu ni kwenu,huna uzalendo bakia us watu kama nyinyi hatuwaitaji bongo,
ReplyDeleteWallahi,utajuta ukirudi
ReplyDeleteYote uyaonayo kwenye magazeti/blog ni kati ya mengi yatokeayo bongo...
Umeme hakuna nchi nzima,
maji hakuna,
rushwa inazidi kushika hatamu kuanzia bandarini,airport mpaka mahospitalini
Foleni kila kona 24seven
Barabara mbovu
Hakuna internet ya uhakika full kwikwi nk nk
Nakushauri,bora ubaki huko ughaibuni uendelee kula asali.Kama unaka link cha ufisadi bongo basi fanya hima kurejea maana mambo mswano..
Ni hayo tu kwasasa
Shukrie!!!
SHAKA ONDOA KAKA... KARIBU NYUMBANI MAMBO NI SHWARI KABISAAA HAYO YA FOLENI, UMEME, MAJI NI YA KAWAIDA SANA YASIKUTISHE MAANA WAHENGA WALISEMA "MKATAA KWAO NI MTUMWA" HATA KAMA KUNA SHIDA GANI.. RUDI BRO UJE UTUMIKIE TAIFA LAKO MAADAM NONDO IPO KAZI UTAPATA INSHALLAH.
ReplyDeleteHatuitaji watu wazandiki na wasio wazalendo kama wewe, nakushauri endelea kuwa mtumwa huko uliko acha sisi tuijenge ardhi yetu kwa shida na raha. Sasa wewe unataka nani aifanye nchi iwe nzuri ili urudi kama sio na wewe kuwa miongoni mwao, kwanza wewe ni Mtanzania kweli!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHOME IS HOME MDAU AND ALWAYS THE BEST PLACE TO LIVE! Usiogope kabisa kurudi nyumbani. Hata huku nyumbani kunahabari ambazo tunazisikia kuhusu Marekani na Ughaibuni na hatutamani kabisa kuja huko.
ReplyDeleteCha msingi Mdau kama ilivyo kwa mahali popote jipange; kutokana na hela za mabox hakikisha una kanyumba kako ka kufikia kilichokamilika na kanachojitosheleza. Kutokana na adha ya usafiri wa Dar haitakuwa jambo baya kupata kausafiri au kuandaa hela ya kuja kununua gari huku maana gari sio luxury tena Tanzania.
Na ukiwa na akiba kidogo ya kukuweka sawa wakati unatafuta kazi itakuwa ni jambo lenye hekima. Unaweza kuanza kutafuta kazi au kunusa nusa kazi ukiwa huko pia kwa kuwatumia wadau mbalimbali ikiwemo Glob ya jamii ambayo imetangaza nafasi za kazi za sehemu mbalimbali mara kadhaa.
kwa kifupi kama umekula nondo utapata kazi tu Tanzania. Inaweza isiwe katika kipindi cha mwezi mmoja lakini utapata maana milango ya ajira ya Tanzania ya miaka sita iliyopita wakati unaondoka nyumbani ni tofautiiiiiiii kabisaaaa na mazingira ya sasa. Wigo ni mpana zaidi.
Karibu nyumbani Mdau. Jipe moyo na usihofu!!!
And by the way; America is NOT heaven and IT WILL NEVER BE!!!
Mdau - Mwanza.
Kwanza hongera kuwepo Marekani manake ni wengi wanatamani nafasi kama hizo lkn hawazipati.
ReplyDeleteKuhusu kurudi nyumbani ni vema ujikumbushe mambo yafuatayo.
1. Nyumbani ni nyumbani hata kama kuna vumbi au unyevu hutakiwi upakimbie
2. Maendeleo ya nchi huletwa na mwananchi mwenyewe kama wewe, mimi na wengine. Hivyo wewe pia unapaswa kuchangia maendeleo ya nchi na si uulize kama mambo safi au si safi. Yakiwa safi unapaswa na wewe ujivunie kuchangia maendeleo hayo na yakiwa mambaya unapaswa ujilaumu kwamba na wewe umechangia kuwa mabaya.
3. Kamwe huwezi ukailinganisha Marekani na Tanzania. Hivyo kama ulishatekwa na umarekani, hutaweza kufurahia maisha ya Tz hata kama ni mazuri. Picha ninayoipata ni kwamba hujapachoka marekani ila unataka kulinganisha marekani na Tz ili kama Markn ni kuzuri zaidi uendelee kukaa huko na kama Tz kuko safi urudi.
4. Kutoa mchango wako katika maendeleo ya nchi si lazima urudi home. Unaweza kuendelea kupiga box ukawa unatuma pesa kwa ndugu zako wanafanya mambo ya maana.
Ni hayo tu mdau. Ukiyatafakari kwa kina unaweza kupata jibu
Mimi nimerejea huku after kua UK zaidi ya miaka 15, nimerudi tangu October 2010 yani tuseme nimekulia kule, kurudi huku nilichukulia kwamba itakua rahisi sana, lakini ukweli nikwamba imekua ina changamoto za kila namna, kuanzia TRA mpaka siku kwa siku kazini,nyumbani, ukitaka kuishi hapa na amani na furaha, usije na mbwembwe za nnje mana watu watakua wanazitegemea, ukubali kutengwa na kua labled, just be real and yourself and usiogope kuuliza maswali utachekwa lakini mwisho na wewe utakua mwenyeji kwa fasta. Kitu kilicho nisaidia mimi ni cha kwanza nyumbani ni nyumbani, kuna watu wanamaisha mazuri sana na kuna watu wanamaisha mabaya sana, maji yapo ila sio kama UK au USA kwamba kila mtu anaweza kufungua bomba, umeme ni issue ila kama sikuizi yani you hardly notice. Tofauti ya hapa na huko kwa mimi binafsi ni kwamba watu hapa wana mentality tofauti ya maisha, sawa tuna matatizo ila matatizo yetu yatarekebika ikiwa watu kama wewe na mimi tunarudi home kusaidiana na wenzetu kuijenga nchi yetu. Hapa jamani watu wapo serious vijana wanachapa kazi mabadiliko yanakuja na tena kwa kasi. Piga ua Tanzania ina uziri wa pekee, magazeti ni vyombo vya habari vinatusaidia kurekebisha vitu visivyo sawa so ukitaka picha halisi ya nchi yetu nakushauri urudi uone mwenyewe and please understand it will take time for you to settle lakini mwisho it is worth it, mana nyumbani ni nyumbani na mahali pazuri sana.....Goodluck, siku njema
ReplyDeletekama unataka kurudi nyumbani wewe rudi kusema eti kuna matatizo ya umeme, foreni za magari, maji, cha msingi uwe na malengo utakapo kuja utafanya nini je? uko marekani ni nyumbani kwako rudi ukajenge nchi yako sasa dondoziii ulizo kula zinamfaidia nani mmarekani au mtanzania karibu sana wewe usiogope hayo
ReplyDeletekichekesho, wanichosha, we kaka umezaliwa huko au ni hizo nondoz ndizo zakufanya uchanganyikiwe na kwenu? HUJATULIA HATA KIDOGO !!!
ReplyDeleteNdugu Mdau, salaam sana. Huku nyumbani mambo ni shwari na hakuna la kutisha. Umefanya vema kupanga kurudi kwani mwenda kwao sio mtumwa.
ReplyDeleteUnaweza kuja kutumia ujuzi uliouata huko Ughaibuni. Panga jambo ambalo unapenda kufanya. Kuwa mbunifu na kutoa ajira kwa wenzako Wazalendo ambao hawajapata kuona yalivyo huko nje, yaani Ughaibuni.
Ukiwa na mtaji, wekeza nyumbani Mdau. Chumia juani huko Arizona na urudi kutumia kivulini huku Tanzania.
Foleni zipo sio uongo. Umeme unakatika katika sio uongo. Lakini tupo na tunajitahidi mwanangu. Mawazo mabaya ya rushwa hayo piga vita popote. Njoo tusaidiane kutoa michango katika kuijenga nchi yetu, maana hakuna mjomba. Wewe na mimi na wenzetu wengineo turudi Tanzania kuiendeleza kwa kila hali na kuboresha maisha kwa wote. Usije na mawazo ya ukabaila au ubwenyenye au kuchukua mapema mapema kama waliotangulia. Njoo na mawazo ya kuleta mabadiliko yenye manufaa kwako, kwa wengineo pia. Pamoja tutafanikiwa nchini mwetu.
Karibu Mdau nyumbani Tanzania.
AEM
I have commented and I think its fine.
ReplyDeleteRUDI HOME KAMA HOME ILI UKAIJENGE NCHI YAKO ILA UKIRUDI KWA KUTEGEMEA TAMBARARE YA BONGO UTAJUTA MARA ELFU KUMI KWA NINI ULIRUDI LABDA UWE UMEJIANDAA KWA NAMNA ZOTEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
ReplyDeleteHabari Kaka!
ReplyDeleteNyumbani ni nyumbani tu mi nachotka kukwambia rudi tu huku full raha mi nilikuwa UK NIMEKULA NONDOZ NIMERUDI BONGO NINA KAZI YANGU NZURI WALA SINA TABU MANAKE UTAENDELEA KUPIGA BOX HADI LINI?MANAKE KAZI NYINGI ZA ULAYA HAMANA KITU HABARI YA FOLENI SIO VILE NA UMEME KWELI MGAO HUPO LAKINI UTAZOEA TU ILA BONGO KAMA UJASOMA CHAMOTO UTAKIPATA MANAKE KAZI ISHU ILA MI NAKUSHAURI URUDI UNAVYOCHELEWA NDO UNAZIDI KUPOTEZA MDA NA WENGI WASIOTAKA KURUDI BONGO HAWAJASOMA,VISA IMEKWISHA SO ANAONA AKIRUDI MMH PAGUMU WE RUDI.
kama ushakula nondo na unajia mini unang'ang'ana na mabox ya nini?
ReplyDeleteBongo ni kujipanga tu,, ukija kichwa kicjhwa na uzungu mwingi bila mipango we jua tu utakula vumbi...
Bongo kwa namna moja hali si shwari kwa idadai kubwa ya watu kiuchumi,, but those with life strategy,, ah si haba,,, wanapata chakuwasitiri.. haya kazi kwako.. miaka sita kwa watu?! yatosha sasa njooni tuijenge Tanzania mpya sasa.. mwe!
Inategemea unarudi nyumbani kufanya nini Boss? Kujiajiri au kuajiriwa? na umeplan kukaa mji gani? Dar, Arusha, Mwanza, etc? In reality kwa watu wastaarabu mji kama Dar es salaam ni kero tupu day in day out. Vitu kama foleni na vijikero vingine vingi vimeshakuwa part ya maisha yetu, asubuhi jioni cku inapita.Mambo hapa home ni mazuri kiasi ukiwa na ngawira za kusafishia jina otherwise mbona utalikumbuka boksi siku si nyingi.
ReplyDeleteSalaams,
ReplyDeleteNyumbani ni nyumbani, ila wakati mwengine ni bora ugenini! nyumbani Tanzania kuna sura mbili, unaweza urudi ufanikiwe kimaisha na ukajiuliza miaka yote ulikuwa unasubiri nini, na unaweza ukarudi ukajuta ujiulize kwanini ulirudi. Ushauri mimi nilio nao ni kwamba, kabla hujarudi hapa Tanzania lazima ujitengenezee njia kwanza , yaani uhakikishe una kajumba cha kuishi na una vyeti vizuri nikimaanisha nondoz na vijipesa vya kuanzia maisha wakati unatafuta kazi. Tanzania ya sasa hivi sio ya juzi, ukiwa na nondoz zako nzuri basi kazi ni nyingi hasa kwenye investment fields kama mabank na mashirika ya umma, ushauri mwengine kuna kampuni nyingi za kutafuta kazi zipo kama radar recruitment na kuna nyingine, jiregister kule kwanza wakuite unaweza hata kufanya interview ukiwa huko , kaka ukishapata kazi rudi ! USIRUDI KAMA HUNA MUELEKEO WA MAANA! UTAJUTA! nyumbani kama huna kazi ni kugumu! na nionavyo mimi sehemu yeyote kama huna kazi ni pagumu! kwahiyo PANGILIA MIPANGO YAKO VIZURI, uwe na kijumba chako! kijigari na kijikazi chako! utakula bata tu ! na once ukishapta kazi na nyie mlio nje mna exposure ya hali ya juu basi unaweza kugombaniwa kama mpira wa kona, na ukizingatia sasa hivi watanzania tunapewa nafasi kubwa kwenye ajira nchini kwetu! ila chonde chonde pangilia mipango yako vema kabla hujarudi ! kama huna muelekeo NAKUSHAURI UKAE HUKO UBEBE BOX !
Mdau , Dar es Salaam ...kwenye maraha ....
MDAU MIMI NADHANI UNATAFUTA KUTUKANWA NA WENYE JAZBA SHAURI YAKO.HUKO UGHAIBUNI UMEKAA MIAKA 6 TU NA UNAONA DHIKI YA NYUMBANI HUIWEZI.MIMI MBEBA BOXI NA NIPO EUROPE MIAKA 11 NA KILA KUKICHA NAFIKIRIA KURUDI TU HATA KAMA HAKUNA UMEME N.K.HAPA MIMI NAJIPANGA TU NAKUWEKEZA VIMTAJI VIDOGO ILI NIKIRUDI NIWE NA SHUGHULI ZANGU BINAFSI.HILO NDIO LA MSINGI LAKINI USINIAMBIE ETI UMEME,FOLENI..HAPO UTAKUWA UNAFUJA KWASABABU TUMEZALIWA KTK MAZINGIRA HAYO NA HALI HIYO INATUHITAJIA WOTE TUKACHANGIE ILI TUONDOKANE NAYO.
ReplyDeleteunavyosoma magazeti ndugu yangu sio kwamba ndio tanzania ilivyo rudi nyumbani hakuna lolote ni unafiki tu wa miandiko humu hakuna hatari wala nini maisha tambarare tu ila uwe unajenga tabia ya kuja kwenu kukaa nje miaka yote hiyo du niroho ngumu hata minipo nje lkn kila baada ya miezi sita huwa naenda home
ReplyDeleteDU POLE SANA KWANI NILIZANI UKO NDIO MAISHA POA KUMBE NAFUU TENA KWETU
ReplyDeleteKama kweli umekula nondo una ujuzi toka kwenye chuo kinachotambulika duniani sio zile short coz,-nammanisha una proffessional maalum karibu Tz kazi zipo tele wewe tu na ufahamu wako wa kujiuza ili upate kazi au ujiajiri maana yote yanawezekana.
ReplyDeleteKaribu sana home mambo si mabaya kwa walioenda shule mpaka sasa...! jiandikishe kwenye kampuni za kutafuta ajira kwa Tz, check magazeti na ujipe angalau miezi sita ya kutafuta. Inshaallah
Mdau Arizona,
ReplyDeleteKama ulivyosema wewe ni Mtanzania na siku zote utakuwa mtanzania, ukipenda lakini maana hiyo ndo asili yako na ndugu, jamaa na marafiki wako huku.
Uwamuzi wa kurudi ni ZAIDI wako binafsi kama unapenda kurudi na kujiunga na watanzania wenzio kujenga nchi yetu.
Nchi yetu ni nzuri lakini kama nchi zingine zozote zinazoendelea na hata zilizoendelea zinamatatizo, nadhani unajua na kuona maandamano na machafuko.
Kwa sasa ukipata kazi nzuri au kuiwa na biashara yako na nidhamu ya kufanya kazi na mwaminifu utafika mbali. na tofauti ni kubwa kati ya miaka sita iliyopita na sasa, 2011.
Unaweza pata kiwanja, ukajenga na ukaishi unavyotaka hapa hapa tanzania bila hata kuiba cha mtu. na ukasafiri nchi yoyote unayoitaka.
Kila la kheri na Mungu akujalie kufanya maamuzi sahihi.
Ndugu yangu Bongo ni tambarare kama una mshiko wako, nyumba na kausafiri kako utaenjoy sana bongo kushinda sehemu yoyote ile, lakini kama huna hivyo vitu bongo utaichukia bora wewe beba box zako huko huko kwa Obama.
ReplyDeleteAnkal naona nashindwa kucomment, kuna mdau kaweka kuhusu suala msaada kwenye tuta, nashindwa kucomment moja kwa moja tafadhali muweekee hii coment - so long haitachafua hali ya hewa
ReplyDeleteNaomba niombe radhi kwa kuchangia kwa mtindo huu, haya mambo ya kuuliza kwamba ni kuzuri kwa sasa au kubaya kwa sasa ni mawazo fulani finyu.
hakuna tofauti na mzee mmoja omba omba (kwa heshima yake jina kapuni) alitakiwa kurudishwa kwa nguvu kwao na serikali, akasema ya kuwa atarudi tu pale atakapohakikishiwa kuwa kuna chakula cha kutosha.
na wewe unayeulizia unadhani nani hilo vumbi (kama lipo) unadhani anatakiwa kuliondoa? [naaamini kwa ujumbe huu message imekuwa delivered clearly]
Hivi tunapozungumzia nyumbani ni Dar es salaam pekee?foleni zipo Dar tu mdau wa ughaibuni hivyo usijali kuna opportunity nyingine ya kuishi mikoa mingine kama Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na hata Rukwa kama foleni nayo ni tatizo kubwa. kimsingi serikali inajitahidi kujenga barabara japo si kwa fedha zake lakin hali si mbaya kwani sehemu kama Mwanza toka Dar ilikua unatumia muda wa siku 2, kwa sasa ukiondoka alfajiri unafika siku hiyo hiyo saa 2 usiku. Kwahiyo usihofu matatizo mengine ni jukumu letu kama wananchi kuyaondoa. HIVYO BASI USIFIRIE KUWEKEZA ZAIDI DAR KWANI KUNA SEHEMU ZINGINE PIA
ReplyDeletendugu yangu Rudi kwenu, hata kama ujasoma we rudi tu kwani nini bwana, utapata kazi tu tena unajua kimombo utafanya hata kazi ya utalii , Nenda Arusha / Moshi Marangu ukatembeze watalii mlima kilimanjaro ule bingo wewee sio unaishi ugaibuni hakuna hata anaekuthamini. ahahahahaha umenikumbusha ule usemi,,,
ReplyDeleteBora kuzaliwa ulaya kama mbwa wa ............ kuliko kuzaliwa bongo .......
barabara ni nzuri sana, umeme upo 24hrs, hakuna foleni za magari yani maisha ni burudani. Ila kama huna gari yako utaipata! umeme uwe na generator yako I mean! na nyumba yako sio kupanga, kama utabeba box ushindwe kujenga nyumba yako bongo wewe utakuwa huna akili ya kutosha unless unabebea box anasa tu. Zaidi ya hapo no shida. Karibu nyumbani.
ReplyDeleteMdau wa Arizona, suala lako ni zuri na lina mtazamo mwingi. Kabla hujarudi nyumbani lazima ufikiri mambo yafuatayo.
ReplyDelete1) Je wewe huko USA unaishi vipi (kihalali)
2)Kama unaishi kihalali basi rudi bongo uangalie hali kama imekuridhisha baki na kama haijakuridhisha rudi tena USA.
3) Kama unaishi isivyohalali basi ukirudi ujuwe ndio umerudi kwahivyo ujipange vizuri sana. Kujipanga ni kuwa uwe na kijimtaji cha kuanzia maisha, ikiwezekana ni kuwa uweze kununua nyumba, gari, kuanzisha biashara japo ndogo wakati unasubiri ajira. Hii ni kwa mtu mwenye nondozz. Kwa mtu asiye na nondozz basi arudi na fani (skill) ambayo italenga katika kujiajiri mwenyewe.
4)Mtu mwenye nondoz 1 atachukua muda wa miezi mpaka miaka kupata kazi isipokuwa fani ambazo zina upungufu kama vile udaktari, uhandisi na nyenginezo.
5)Mtu mwenye nondoz 2 atachukua miezi mpaka mwaka isipokuwa hizo taaluma za hapo juu.
6)Mtu mwenye nondozz 3 huyu anatafutwa na mishahara mizuri na atakuwa na maisha mazuri.
7)Kama utaweza kurudi na $50,000 basi maisha hayatokuwa mabaya kwako hata kama huna nondoz.
8)Pia usiache kumcha Mwenyenzi Mungu, yeye ndie atoae riziki.
Jambo jingine la kuangalia maisha TZ ni mazuri kwa kila mtu anayejituma. Kama utakuwa mvivu basi utaishia na simanzi na kusingizia ccm na wanasiasa kumbe ni wewe mwenyewe. Hii sio tu kwa TZ hata huko USA kuna watu wavivu na wanasingizia wageni wanachukua kazi zao. Popote unapokuwepo ni kuwa ufanye kazi kwa bidii ili upate mafanikio. Nimewasilisha.
KAKA YANGU, WASWAHILI WANASEMA MKATAA PAO NI MTUMWA
ReplyDeleteHOME IS HOME MY DEAR BROTHER HATA KAMA KUNA SHIDA KIASI GANI. WEWE USHAPATA NONDOS ZAKO INSHALAH MUNGU YUPO UTAPATA KAZI
KWANI ULIPOENDA HUKO ULIKUWA NA UHAKIKA KWAMBA UTAFANIKIWA? SI ULIJARIBU TU? NA HUKO SIO NYUMBANI KAMA HUKU NA MUNGU AMEKUFANIKISHA MPAKA UKALA NONDOS ZAKO NA BOX UKALIPIGA MPAKA LEO? RUDI NYUMBANI
KAKA WANASEMA NYUMBANI NI NYUMBANI.LAKINI WEWE MWENYWEWE ULINGANISHE MAISHA ULIOKUWA UNAISHI KABLA HUJAENDA US.KAMA WEWE MWENZETU NI MTOTO WA WAZIRI WA FEDHA WA TANZANIA RUDI,LAKINI KAWEWE NI AKINA SISI MJOMBA BEBA BOX KWA HAMU KUBWA.WEKA MAMBO SAWA HUKO YAANI SUBIRI MPAKA UPATE STAY YAKO ILIUKIRUDI BONGO MAMBO YAKIWA MAGUMU UNARUDI ZAKO US.TUMEKULA NONDO WENGI KAZI ZA SHIDA HATA UKIIPATA HAILIPI,WEWE ZAMA HUKOHUKO.MDAU EUROPE
ReplyDeletewasikudanganye wa2 we zamia hukohuko,bongo kumenuka maisha wanayo mafisadi na watoto zao,mie mwenyewe napiga maktaim nikipata mchongo bongo bye bye and nimeswear i will never come back, coz its better kuwepo jehanum than kuish bongo,ukirudi utakumbuka advice yangu.......luc
ReplyDeletekwa kweli kaka mimi nimekuchujia majibu ambayo naona yatakufaa, kuna mdau huko juu anaitwa maimuna tafuta jibu lake na wadau waliocomment fri jun 17 03:30 na june 17 8:35 nadhani hao ndio wamesummarize vizuri ushauri niliotaka kukupa kila la kheri
ReplyDeletemdau mimi nipo UK napiga nondoz yangu ya mastazi ila nikimaliza tu safari ya TZ ..bongo kama umesoma hushindwi maisha na kama ni kuajiriwa hukosi kazi angalau uwe na mastazi...ila kama degree moja kidogo utasota..maana degree moja zipo tele labda kama uwe na kitu tofauti na wengine..mi nakushauri jipange rudi ..huo muda uliokaa ukirudi utashangaa wenzako mliosoma wote enzi hizo walivokuacha mbali .utajuta kwa nini ulikaa USA miaka yote hiyo...rudi TZ nna mifano hai ndio mana nakushauri urudi..porojo za magazeti ni siasa tu ila hali si mbaya kama inavyosemwa...huku UK wasiosoma wengi ndio hawataki kurudi na wanalinda maduka na kufanya kazi za ajabu( zaidi ya box) ila wanadanganya wenzao bongo kuwa huku maisha mazuri wakati wanapata shida tupu kufanya kazi nne nne ...ukizingatia hawajasoma bongo sio sehemu ya kurudi kwa wao((sina lengo la kukashfu))....ila pia hata ukiwa na masters kwa hapa UK wewe kama mgeni huwezi kupata kazi ya maana kama ambavyo unaweza ku win bongo... mdau jipange urudi
ReplyDeletemdau reading UK