KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (wapili kushoto), akizungumza na kiongozi kutoka chama cha upinzani cha SPD cha Ujerumani ambacho kinaongoza jiji la Humberg nchini humo, Wolfgang Schmidt, (wapili kulia), wakati kiongozi huyo na ujumbe wake walipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam. leo. Wapili kulia ni Stefan Herms kutoka chama hicho.
Nape akiwaonyesha viongozi hao picha za Baraza la Mawaziri walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete baada ya CCM kushinda uchaguzi mkuu uliopita.
Schmidt akimpongeza Nape baada ya mazungumzo yao kumalizika.
Schmidt akitazama Ilani ya Uchaguzi ya CCM baada ya kukabidhiwa na Nape wakati wa mazungumzo hayo. Kushoto ni Herms kutoka chama hicho.
Nape na Schmidt wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa mgeni huyo, mbele ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.
Hiyo picha ya kwanza wanaonekana hawamuelewi kabisa anachokisema. Wameduwaa!!!!!!!
ReplyDeletewaaapiii , wanakubaliana na sera adhimu na uongozi mahiri wa Chama Cha
ReplyDeleteMapinduzi
CCM nawapongeza kufanya urafiki na chama cha UPINZANI ujerumani. Waulizeni jinsi chama kinavyoweza kubalance na kusonga mbele kutoka KUTAWALA hadi UPINZANI. Big up sana tu.
ReplyDeleteAAhh Napegwa.
ReplyDeleteMdau wa kwanza nafikiri uko sahihi, picha haziongopi inaonekana kuna mgongano wa lugha.
ReplyDelete