JK akisalimiana na winga machacahri wa klabu ya Azam FC na Taifa Stars Mrisho Ngassa siku alipokutana na TAifa Stars Ikulu siku za nyuma. Baadaye leo Ngassa anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwamo katika kikosi cha Seattle Sounders ya Marekani kitachocheza mechi ya kirafiki na Manchester United huko Marekani hivi karibuni. Ngassa, ambaye atakuwa mchezaji mwalikwa, anatarajiwa kutangazwa katika mkutano na wanahabari utaofanyika leo hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam majira ya saa sita
Home
Unlabelled
news alert: mrisho ngassa kucheza katika mechi ya seattle sounders vs man united marekani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
wahusika ,mnaowapeleka vijana kuonana na viongozi wa nchi,wafundeni maadili.Ngasa kusalimiana na Raisi akiwa ameweka mkono mfukoni sijaipenda,hata kiumri tu bado haileti heshima ,hasa ikizingatiwa yeye ni kioo cha jamii.Au wadau mnaesemaje?
ReplyDeleteNakubaliana na Anony wa kwanza kuhusu maadili. Tuwafundishe vijana wetu maadili.
ReplyDeleteNI UKOSEFU WA NIDHAMU
ReplyDeleteNI UKOSEFU WA ELIMU
NI UKOSEFU WA UREFU
NI UKOSEFU WA HESHIMA
NI KUJIONA STAA KUMBE HE IS NOTHING
HAWAKUWAFUNDISHWA MAANA YA PROTOKALI
hata mimi sijapenda, mkono mmoja mfukoni
NIDHAMU CHAFU
ni kweli kakosea kufanya hivyo, au alikuwa anataka kumpa kadi yake ya namba za simu RAIS
ReplyDeleteNi kweli mdau hapo juu i second you..Kusalimiana na mkubwa mkono mfukoni si heshima, All the same I wish him best of luck, thats a big step forward na its a good opportunity for him kujitangaza.
ReplyDeleteNi kweli huwezi salimiana na kiongozi wa nchi mkono umeuweka mfukoni, ni ushamba, ni ujinga, sio heshima, ni kujidharaurisha!! Jamani vijana tujirekebishe. Kupeana mkono na kiongozi wa nchi is a very rare opportunity, Ngassa hukustahili kufanya hivyo kaka.
ReplyDeleteHata sio ujanja!!
swadakta mdau wa hapo juu umenena maana nidhamu ni ndogo kwa vijana wetu na ukilinganisha na matatizoa ya viongozi wao wanashindwa kuwafundisha nidhamu na wahata mavazi yao mara nyingi wanafika ikulu na kandambili
ReplyDeleteOK,mchangiaji wa kwanza hapo juu: ninatambua unachokisema, hata hivyo, IMHO, mimi naona suala la kumsalimia Rais (or any older person for that matter) kwa kumtukuza sana pia si heshima vile vile, ni mambo ya kikoloni na yamepitwa na wakati mno. Katika karne hii ya 21, mtu haonekani kuwa ana "heshima" kwa salaamu za "shikamoo mzee" au kwa kusalimiana kwa mikono miwili, hiyo ni nidhamu ya uwoga na unafiki and it's too old school! Heshima ya mtu huonekana kwa vitendo vyake vya kiungwana, na mchango wake katika jamii. Utamchukuliaje mtu anayesalimia kwa kusujudu sana watu kumbe huku nyuma ni mla rushwa sana mkubwa au mzinzi/mwasherati wa kutupwa?? Je ana "heshima" huyo??
ReplyDeleteMimi sidhani kama Ngassa hapo amemkosea heshima yoyote "mheshimiwa" rais, Ngassa ni sportsman si mwanasiasa au mwanadiplomasia! Psychologically mwanamichezo yeyote huwa wanakuwa laid back/relaxed in their own style, na kama unavyoona kwenye picha, that was a relaxed/laid back environment, i.e. wazee/viongozi na vijana wakicheka (nahisi kama utani pia unarushwa pale unajua tena jamii yetu ya Kitanzania tunavyopenda utani katika occassions), n.k. So nakushauri usiiangalie picha juu juu tu na kuhitimisha kwamba kijana hana heshima - utaharibu sana wasifa wake, badala yake, jaribu kufikiria nje ya box (think outside the box) na uangalie pia mazingira yalivyo.
Mbona hapa UK na hata huko US sports icons wanapokwenda Number 10 na White House respectively kuonana na viongozi wao husalimiana nao wakiwa relaxed na mikono mifukoni na watu hawapigi kelele? Dunia imesha-evolve sana mdau, haya mambo ya kusujudiana sana they are long gone.
Halafu pia suala jingine ninalotaka kusema hapa - ambalo liko kisiasa zaidi ya kimaadili (more political than ethical), ni kuwa wakati mwingine mtu anapokwenda kuonana na public figures kama rais, body language yake na mvuto wake kwake pia kunategemeana na jinsi gani huyo rais anam-influence kivitendo (performance). Kwa mfano, huwezi ukategemea vijana wakutetemekee na kukusujudu wakati uongozi wako unaelements za uozo na unakumbatia corruption, I wouldn't! Nikupe mfano mmoja, Wakati Hayati Mwl. Nyerere akiwa Rais, uliona vile uwepo wake ulivyokuwa unaheshimika?? Mtu ulikuwa unapopata chance ya kusalimiana naye unajivuna ati - you really feel proud!! Lakini viongozi wetu hawa wa siku hizi ndo hivyo tena - sijui kama umenielewa hapo, hope you do.
Sorry kwa comment ndefu, and I hope you are not offended, mimi huwa ni nadra sana ku-comment humu, lakini nimeona hapo juu umetaka maoni yetu na hili suala la kimaadili (socio-ethics) likanigusa kwani ni moja ya vitu ninavyodeal navyo hapa chuoni.
Dennis B.
UK.
NAKUBALIANA SAWA NA ABBAS KONDORO ALIVYOWEKA MIKONO WAKATI WABABU WATU WAZIMA WAMEZIBA BARABARA KUTAKA HAKI ZAO AKAANZA KUONGEA NAO HUKU MIKONO YAKE MFUKONI.
ReplyDeleteHata mimi dogo kaniboa. Hana heshima hata kidogo. Nidhamu ni msingi wa maendeleo. Hawa vijana kama hatutawafundisha maadili hawatafika popote wataishia hapa hapa. Embu angalia mtu mzima anamsalimia kwa mikono miwili yeye mikono kaweka mfukoni??? Hii haikubaliki hata huko marekani anakokwenda. I am living in europe na ninaona watu wana manners when it comes to official events.
ReplyDeleteMambo ya EKSPOSHJA hayo ndugu yangu. Msimlaumu sana. Eksposhja ndogo.
ReplyDeleteNdege yenyewwe wameanza kuzipanda wakatiu wanaenda kwenye mechi za kimataifa.
Daah! Noma kweli!
Kwani kuweka mkono mfukoni kuna tatizo gani? Hapo sikubaliani na mtoa maoni wa kwanza.
ReplyDeleteAnony wa 10:55am, kuna mambo mengi sana hawa celebrities wetu wanatakiwa kujifunza. Ila haihitaji degree mtu kujua jinsi ya kusalimiana na mkubwa wako haswa raisi wa nchi. sasa hawa wachezaji wetu sijui ni bangi ndo zinawaharibu manake hata mimi nimeshangaa kuona mkono mfukoni ilhali raisi kampa attention yote. ndo maana wakienda nchi za nje huwa wanapigwa kibuti haraka manake discipline ni zero..
ReplyDeleteWewe mdau wa juu,,mimi nakushangaa kabisa!! kwani unataka watu waendelee kuishi kama enzi za kikoloni??Mbona huku ulaya hata rais wa Ujerumani akitembelea mwananchi wachini wanasalimiana au wanaongea kama mtu wa kawaida tu?au akienda kuhemea sokoni anakaa kwenye foleni kama wengine?,,mimi sioni kosa lolote kwasababu rais nikama watu wengine tuu.Heshima sio kunyenyekea au kutoa hiyo shikamo yenu.
ReplyDeleteNi kweli kabisa mdau. Heshima si kunyenyekea wala kutoa shikamoo. Inabidi ifikie wakati na sisi Watanzania tuamke kama nchi zilizoendelea na tutambue kwamba rais ni mtu kama watu wengine, ni mtumishi wa umma na SI mtawala!! Mambo ya "utemi" "uheshimiwa" na "ukuu" yalikuwa zamani. Sasa hivi society imeadvance, tunaishi katika jamii huru na ya kidemokrasia where everyone is allowed to be himself alimradi huvunji sheria. Dogo Ngassa anamheshimu kama binadamu mwenzie - si lazima amnyenyekee kihivyo. Tuamke jamani Watanzania ndio maana sisi tunanyonywa na mafisadi wala hatusemi kitu Kama mataifa mengine e.g. Kenya, sababu tumerithishwa nidhamu ya uwoga toka enzi za ukoloni! Kazi kweli.
ReplyDeleteJamani msimulaumu ni muislamu.
ReplyDeleteTatizo letu Watanzania, kila jambo tunalifanya la kisiasa. Hata kama angemsalimia kwa mikono miwili, watu wangetafuta sababu nyingine, eti kwa nini hakuvaa suti! People, you need to think out of the box. Acheni kufanya kila jambo ni la kisiasa. Inaudhi sana. Rais ni mtu kama mwingine tuu. Hatuna mtukufu Rais Tanzania.
ReplyDeleteNadhani kipimo cha Ngasa siyo wanaoishi nje ya Tanzania.Wala siyo suala la kwenda na wakati. Nisuala la kubadilika kuendana na mazingira unayoishi na kwa kuzingatia tukio husika.Fanya tathmini fupi tu yako wewe mwenyewe kukutana na baba yako mzazi, baba mkubwa, mjomba nk kisha usalimiane nae ukiwa umeweka mkono mfukoni!!! Pengine ni mwalimu wako aliekutoa kamasi na kukafanikiwa kufika hapo ulipo. Nadhani pamoja nautandawazi hali kama hiyo ilikuwa nadra sana hata wakati wa Mwalimu Nyerere anayetolewa mfano na baadhi ya wadau hapa. Kwa ufupi kijana anahitaji ushauri. wanaomtetea pia wanahitaji ushauri.
ReplyDeleteMdau kutoka Bondeni
Anony wa 07.10.00PM, dini inahusu je hapo. Na kwa taarifa yako waislamu hawavai suruali na wakisalimiana wanapeana mikono miwili na kuombeana salama kati yao. Na yule mdau wa UK anayesema huko hawaangalii unyenyekeaji hiyo siyo kweli. mUK kwa mUK mwenziwe ndio haangalii hayo lakini ukiwa wewe siye basi lazima unyenyekee ndio mambo yako yatakapofanikiwa. Kwani wewe uliye siye huna haki sawa na wao.
ReplyDeleteHello ankal nani hii, wachangiaji wote hapo juu nawapa hongera kwa maoni yao.Wengine kwa ukali,na wengine kwa kutusi kabisa. Lakini huyo dogo hana kosa kwasababu ndivyo alivyofunzwa tena hata field yake inamruhusu kwa hivyo.
ReplyDeleteNyie wote sikilizeni, dogo Ngassa na watoa hoja. Mungu anasema nini kupitia neno lake..... Warumi 13:1-7..... anaestahili heshima apewe heshima, anaestahili hofu, apewe hofu. Tena wote tuzitii mamlaka kwa sababu hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu. Nduli wa Uganda,Farao wa Misri na wengine wengi waliitwa ni watumishi wa Mungu. Aliwatumia kutiisha watu, nao walipojisahau na kujiinua aliwaadhibu.
Hivyo mkubwa ni mkubwa tu, haijalishi anatabia gani. Anastahili kupewa heshima bila subira au kikwazo chochote. Rais aheshimiwe popote hata akiwa mzinzi,mlevi,fisadi,mwizi,tapeli nk. Sheria ndiyo imwondoe na kumpa mwingine na siyo mtu binafsi kwa mtazamu/msimamo wako. Vinginevyo waweza itwa muasi/opposer/mpinzani/unt gov.
Anony wa 07:10:00p.m, unamaana waislam hawana adabu? Kama huna LA KUSEMA bora unyamaze maana unaweza ukawachefua watu!
ReplyDeleteHeshima ni kitu cha bule,siyo kwasababu ya Rais tu,Je baba yake anaweza kumsalimia huku ameweka mkono mfukoni?Au mtu mzima yeyote anaweza kumsalimia huku ameweka mkono mfukoni?Hiyo si heshima kabisa.Nyinyi mnaokubali alivyofanya ni sawa, basi nyinyi ndiyo wale wale mliokulia barabarani.
ReplyDeleteHATA MIMI SIONI KOSA KUSALIA NA MKONO MMOJA KAWEKA MVUKONI HIZI SIO ZILE NYAKATI ZA UKOLONI HIZI NI ZAMAUWAZI NA UKWELI HAKUNA KUMSUJUDIA BINADAMU MWENZAKO KAMA YEYE NDIYE ALIYEUMBA MBINGI NA NCHI NI Mungu peke yake anafaa kusujudiwa na sio mwanadamu sisemi amdharau lakini watu wengine wanadhani heshima mpaka umpigigee mtu magoti ndio uonekane unaheshima sana zimepitwa hizo wandugu
ReplyDeleteafu watu wengine bwana kweli empty vichwani mwao.. sasa wewe anonymous wa
ReplyDeletemon jun 20,07 07:10:00 PM uislamu unaingiliana vp hapo??? kila kitu mnaleta inshu za dini.. kama unashindwa kuishi pamoja na waislamu na wanakukera sasa basi si uhamie jupiter..
Confidence ya wanaume ipo mfukoni.ndiyo maana mtu akiongozana na mwanamke wake huwa anaweka mkono mmjoa mfukono.au hata mtu akiwa anapresent mada huku anaogopa mara nyingi anaweka mkono mfukoni.Dogo alikuwa anatafuta confidence rais ni kitu kingine.
ReplyDeleteni nidhamu ndogo tena ndogo sana. yaani inaonyesha dharau kubwa iliyopitiliza mbali ya kwamba huyu ni raisi pia ni mkubwa kiumri yaani ni baba yake. kusalimia wakubwa hakuhitaji shule ni malezi. hakuna suala la confidence, uislamu wala ukoloni, ni TABIA MBAYA TU!!!!
ReplyDelete