Mwaka 2000, Ivan Marovic na rafiki zake waliongoza harakati zisizo na mapigano au vurugu ambazo hatimae zilimwondoa madarakani dikteta wa Kiserbia, Slobodan Milosevic.
2011, Marovic alishiriki kama profesa Narco News School of Authentic Journalism ambako alifundisha wanafunzi toka sehemu mbalimbali duniani kuhusu ya mkakati wa“dilemma action” unapokabiliana na dola.
Wanafunzi na Maprofesa toka kwenye kundi la video, lililohusisha Nathan Mpangala, Katie Halper, Daryn Cambridge, Leslie Askew, Kevin Mwachiro and Maria Dayton walitengeneza video hii. Video hii inathibitisha kwamba, pingamizi za kijamii(ambazo zinaripotiwa kwenye vyombo vya habari) zinaweza na zinabidi ziwe na ucheshi ndani yake!
Kazi ya sanaa ya mkono inayooonekana katika video hii ni ya mchoraji katuni za kisiasa toka Tanzania, Nathan Mpangala, aliyekuwa mmoja wa wanafunzi wa School of Authentic Journalism, 2011
Ankal umevutiwa nini hasa na hii video?
ReplyDeleteNaona inajirudiarudia