Wananchi wa Dar es salaam wakiwa na wasiwasi makutano ya barabara ya Morogoro road na mtaa wa Samora Avenue katikati ya jiji mnamo saa sita kasorobo. Hakukuwa na madhara ya aina yoyote 
 Watu wakishangaa barabarani huku wakisikilizia kama kitalia tena
Askari na walinzi wakiwa tayari kwa lolote jengo la PPF House mtaa wa Samora Avenue. Picha na mdau JP


JIJI la Dar es Salaam leo limetikiswa na tetemeko dogo la ukubwa wa richta 4.8 na kusababisha wakazi katika majengo marefu katikati mwa Jiji hilo kuyakimbia.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma alisema jana kuwa tetemeko hilo lilitokea saa 5: 28:13 katikati ya Bahari ya Hindi katika kina cha kilometa 10.

Alisema eneo hilo liko usawa wa latitude 7.080 na longitude 39.628 na umbali wa kilometa 52 Kusini Mashariki wa Jiji na kilometa 105 Kusini Mashariki mwa Zanzibar na mtikisiko wake ulienea hata Rufiji na Kusini mwa visiwa vya Zanzibar.

Hii ni mara ya pili ndani ya miezi sita kwa Dar es Salaam kukumbwa na tetemeko la ardhi.
Alisema huenda tetemeko hilo likawa limesababishwa na sehemu ya ardhi kuteleza katika mipasuko ya ardhi iliyopo katika pwani ya Tanzania.

Profesa Mruma aliitaja baadhi ya mipasuko ya ardhi kuwa ni bonde la Ruvu, bonde la Mzinga linalotenganisha kati ya Mbagala na Dar es Salaam, mkondo wa Bahari ya Hindi eneo ilipo bandari na unaotenganisha Wazo Hill, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na milima ya Pugu. 




Aidha, aliwahadharisha wananchi kuwa makini hususan kwa wanaofanya shughuli za uvuvi na watumiaji wengine wa bahari kutokana na kutojulikana kama litaendelea.

“Kuna matetemeko ya aina tatu, ambayo yanaanza taratibu na hufuatiwa na makubwa na kasha mengine yanamalizia … kuna uwezekano wa kujirudia kutokana na chanzo cha tetemeko lenyewe.

“Mara nyingi matetemeko kama haya huambatana na mawimbi makubwa ya tsunami, ni vema wavuvi, vyombo vya usafiri na watumiaji wengine wa bahari kuwa waangalifu,” alisema.

Katika hali isiyo ya kawaida, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Aloyce Tesha, alisema mtikisiko huo haukutokana na tetemeko, bali na mabomu yaliyokuwa yakilipuliwa Gongo la Mboto.

“Wananchi walipewa hadhari ya kulipuliwa kwa mabomu, hata wakati ule wa mabomu waliopata mtikisiko ni wale waliokuwa kwenye majengo marefu, angalia tovuti ya jeshi wamelieleza hili.”

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema: “Tumepata taarifa ya kuwepo tetemeko la ardhi, lakini hakuna taarifa ya uharibifu wa mali na vifo na hali imekuwa shwari.”





Chanzo: HABARI LEO
--------------------------------------------------------------------------
Magnitude 4.8 TANZANIA 
Friday, June 10, 2011 at 08:28:13 UTC 
Magnitude 4.8 
Date-Time Friday, June 10, 2011 at 08:28:13 (UTC) - Coordinated Universal Time 
Friday, June 10, 2011 at 11:28:13 AM - Local Time at Epicenter 
Time of Earthquake in other Time Zones 
Location 7.08S 39.63E 
Depth 10.0 kilometers 
Region TANZANIA 
Distances 52 km (32 miles) ESE of DAR ES SALAAM, Tanzania
105 km (65 miles) SSE of Zanzibar, Tanzania
230 km (142 miles) SSE of Tanga, Tanzania
713 km (443 miles) SSE of NAIROBI, Kenya

Location Uncertainty Error estimate not available 
Parameters Nst=0, Nph=0, Dmin=0 km, Rmss=0 sec, Gp=0 degrees 
Source USGS NEIC (WDCS-D) 
Event ID usc000440z 


SOURCE: http://earthquake.usgs.gov/earthquakes/eqarchives/last_event/world/world_tanzania.php 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2011

    Haijafika bado ile zilzala yenyewe ambayo ingewafanya watu wajiulize ina nini hii ardhi leo, hako ni kamstuo tu mungu anawakumbusha wajibu wenu kwake

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2011

    Endeleeni kufanya ngono tu hio mungu kawa pib tu, wabongo roho juu, sasa nyinyi endelezeni zinaa tu, mutaona kwani nchi zote zinazopata mambo kama hayo ni zenye kuendekeza laana, kama india, japan nk hizi nchi zote zinamkufuru mungu sana ukitaka kujuwa lana gani uliza, na sisi wabongo tumezidi tumeacha mila zetu na tunaiga za watu ..........sasa hio ya leo ni kubipiwa tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2011

    Mkiambiwa mtunze mazingira amuelewi. Sasa tetemeko na Tz wapi na wapi. Haya jengeni barabara serengeti muoni mabadiliko ya tabia nchi kwa vitendo si kusoma vitabuni

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2011

    Subhanna Allah
    We thank Lord there was no loss of life.But man is reminded that:
    whosoever does good equal to the weight of an ant will get his reward, and whosoever does evil even equal to the weight of an ant, shall equally see it Quraan hakim

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2011

    Kweli Zambi Zimezidi Tanzania. Ni Mafisadi kila kona. Viongozi, Matrafiki, Madaktari. Ukienda Petrol Station wanachanganya mafuta, TRA wanawasubua wafanyabiashara kutaka rushwa, kiongozi ana account huko dubai ya mamilioni, Trafic anatafuta kosa .hata kama halipo...Zambi ni nyingi..Na WARNING ya MUNGU ndiyo hiyo! Tubadilike Watanzania. Tuwe tunafuata yalioandikwa kwenye vitabu vitakatifu..Kuna kufa, kiyama...Tubadilike!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 10, 2011

    NI HATARI! Kama mdau alivyosema. 4.8 sio mchezo. Lakini hamna kiongozi mpaka saa hii hajatamka chochote hata mamlaka zetu. Je maafa yakitokea tuna uwezo wakukabiliana nayo?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 11, 2011

    Yashangaza wakazi wa DSM wakiegemea kuta za majengo wakisubiri tetemeko lingine kama litatokea. Je tetemeko ambalo lingefuatia na kuwa la kipimi cha ritcha 8 wangepona hao waegemea ukuta wa majengo?

    Nadhani elimu itolewe nini cha kufanya likitokea tetemeko la ardhi, mfano watu waambiwe wakusanyike eneo la wazi mbali na majengo.

    Mdau
    Turkey.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 11, 2011

    Poleni watanzania na mwenyezi mungu atuepushe maana maafa yamezidi duniani.Hebu ingieni ktk youtube halafu taipu neno "haarp".Kuna mambo mengi tuna weza kuyajua tafadhalini na yanatisha na pengine tunaweza kuangamia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...