Wananchi wa Dar es salaam wakiwa na wasiwasi makutano ya barabara ya Morogoro road na mtaa wa Samora Avenue katikati ya jiji mnamo saa sita kasorobo. Hakukuwa na madhara ya aina yoyote
Watu wakishangaa barabarani huku wakisikilizia kama kitalia tena
![]() | ||
| Askari na walinzi wakiwa tayari kwa lolote jengo la PPF House mtaa wa Samora Avenue. Picha na mdau JP JIJI la Dar es Salaam leo limetikiswa na tetemeko dogo la ukubwa wa richta 4.8 na kusababisha wakazi katika majengo marefu katikati mwa Jiji hilo kuyakimbia. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma alisema jana kuwa tetemeko hilo lilitokea saa 5: 28:13 katikati ya Bahari ya Hindi katika kina cha kilometa 10. Alisema eneo hilo liko usawa wa latitude 7.080 na longitude 39.628 na umbali wa kilometa 52 Kusini Mashariki wa Jiji na kilometa 105 Kusini Mashariki mwa Zanzibar na mtikisiko wake ulienea hata Rufiji na Kusini mwa visiwa vya Zanzibar. Hii ni mara ya pili ndani ya miezi sita kwa Dar es Salaam kukumbwa na tetemeko la ardhi. Alisema huenda tetemeko hilo likawa limesababishwa na sehemu ya ardhi kuteleza katika mipasuko ya ardhi iliyopo katika pwani ya Tanzania. Profesa Mruma aliitaja baadhi ya mipasuko ya ardhi kuwa ni bonde la Ruvu, bonde la Mzinga linalotenganisha kati ya Mbagala na Dar es Salaam, mkondo wa Bahari ya Hindi eneo ilipo bandari na unaotenganisha Wazo Hill, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na milima ya Pugu.
Chanzo: HABARI LEO -------------------------------------------------------------------------- |
Friday, June 10, 2011 at 08:28:13 UTC
Magnitude 4.8
Date-Time Friday, June 10, 2011 at 08:28:13 (UTC) - Coordinated Universal Time
Friday, June 10, 2011 at 11:28:13 AM - Local Time at Epicenter
Time of Earthquake in other Time Zones
Location 7.08S 39.63E
Depth 10.0 kilometers
Region TANZANIA
Distances 52 km (32 miles) ESE of DAR ES SALAAM, Tanzania
105 km (65 miles) SSE of Zanzibar, Tanzania
230 km (142 miles) SSE of Tanga, Tanzania
713 km (443 miles) SSE of NAIROBI, Kenya
Location Uncertainty Error estimate not available
Parameters Nst=0, Nph=0, Dmin=0 km, Rmss=0 sec, Gp=0 degrees
Source USGS NEIC (WDCS-D)
Event ID usc000440z
SOURCE: http://earthquake.usgs.gov/





Haijafika bado ile zilzala yenyewe ambayo ingewafanya watu wajiulize ina nini hii ardhi leo, hako ni kamstuo tu mungu anawakumbusha wajibu wenu kwake
ReplyDeleteEndeleeni kufanya ngono tu hio mungu kawa pib tu, wabongo roho juu, sasa nyinyi endelezeni zinaa tu, mutaona kwani nchi zote zinazopata mambo kama hayo ni zenye kuendekeza laana, kama india, japan nk hizi nchi zote zinamkufuru mungu sana ukitaka kujuwa lana gani uliza, na sisi wabongo tumezidi tumeacha mila zetu na tunaiga za watu ..........sasa hio ya leo ni kubipiwa tu
ReplyDeleteMkiambiwa mtunze mazingira amuelewi. Sasa tetemeko na Tz wapi na wapi. Haya jengeni barabara serengeti muoni mabadiliko ya tabia nchi kwa vitendo si kusoma vitabuni
ReplyDeleteSubhanna Allah
ReplyDeleteWe thank Lord there was no loss of life.But man is reminded that:
whosoever does good equal to the weight of an ant will get his reward, and whosoever does evil even equal to the weight of an ant, shall equally see it Quraan hakim
Kweli Zambi Zimezidi Tanzania. Ni Mafisadi kila kona. Viongozi, Matrafiki, Madaktari. Ukienda Petrol Station wanachanganya mafuta, TRA wanawasubua wafanyabiashara kutaka rushwa, kiongozi ana account huko dubai ya mamilioni, Trafic anatafuta kosa .hata kama halipo...Zambi ni nyingi..Na WARNING ya MUNGU ndiyo hiyo! Tubadilike Watanzania. Tuwe tunafuata yalioandikwa kwenye vitabu vitakatifu..Kuna kufa, kiyama...Tubadilike!
ReplyDeleteNI HATARI! Kama mdau alivyosema. 4.8 sio mchezo. Lakini hamna kiongozi mpaka saa hii hajatamka chochote hata mamlaka zetu. Je maafa yakitokea tuna uwezo wakukabiliana nayo?
ReplyDeleteYashangaza wakazi wa DSM wakiegemea kuta za majengo wakisubiri tetemeko lingine kama litatokea. Je tetemeko ambalo lingefuatia na kuwa la kipimi cha ritcha 8 wangepona hao waegemea ukuta wa majengo?
ReplyDeleteNadhani elimu itolewe nini cha kufanya likitokea tetemeko la ardhi, mfano watu waambiwe wakusanyike eneo la wazi mbali na majengo.
Mdau
Turkey.
Poleni watanzania na mwenyezi mungu atuepushe maana maafa yamezidi duniani.Hebu ingieni ktk youtube halafu taipu neno "haarp".Kuna mambo mengi tuna weza kuyajua tafadhalini na yanatisha na pengine tunaweza kuangamia.
ReplyDelete